The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,541
Honestly, mimi sijakuelewa....Mimi niliuona uongozi wa Rais Samia kinabii nikauona ni uongozi unaoelekea kuanguka ila watu wasiomtakia mema walimsifu na kusema anaupiga mwingi kumbe walikuwa wanampoteza
Rais Samia kabla ya kujijenga kisiasa alitakiwa kwanza awe mtulivu atengeneze urafiki na wapiga kura wake awafariji waliofiwa walau atulie kwa muda hata wa mwaka mmoja ndipo aanze mabadiliko ndani ya serikali yake lkn hawakumshauri vizuri badala yake akaanza visasi kwa kiwango cha hali ya juu
kwa sasa anaona Pamevuja anaona nguvu ya chuki dhidi yake inaongezeka lkn it's too late
Nasisitiza kuwa, kugombea Samia 2025 ni anguko kuu la CCM
Hoja yako inabebwa na sentensi moja tu, "Alikosea toka mwanzo, hawezi kurekebisha tena"
Bahati mbaya hujaichambua ili ilete ushawishi na kutufanya tuelewe utakacho tuelewe kwa urahisi...
Sasa kwa mifano halisi isiyo na shaka na ya wazi, hebu eleza alikosea nini na kwa namna gani...?
Na je kwa uelewa wako, unadhani alipaswa afanye nini badala yake..?