Rais Samia alishiriki filamu ya Royal Tour bila kinga ya heshima ya nchi. Tunashuhudia makosa ya kudhalilisha nchi

Rais Samia alishiriki filamu ya Royal Tour bila kinga ya heshima ya nchi. Tunashuhudia makosa ya kudhalilisha nchi

Tatizo unafanya personofication badala ya kuangalia mantiki ya hoja na nini implication yake kwa taifa letu.

Ukiangalia ile picha hata utamaduni wetu watanzania uliwekwa rehani. Imagine mtu baki anamshika Mama yetu pasi staha, kweli!

Yaani mimi nilijisikia vibaya sana kuona mtu kama mama yangu anashikwa na libaba nisilolifahamu...Kwakweli hili jambo limenisononesha mimi kama mtanzania moja, sijui wenzangu.

Lakini kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi, dhamira ya Rais wetu pengine ilikuwa njema ila tu hakujua ita imply nini kwa raia...Na mimi nauliza kweli Rais wetu analindwa? Mpambe wake kwanini alikubali haya? Je inaruhusiwa mpambe kuondoka nyuma ya Mh. Rais iwe kwa namna yeyote ile?

Mkumbuke bado hatuja pona kwenye vidonda vya Rais wetu kuaga dunia akiwa katika kazi ya urais na kwa wiki nzima haikujulikana alikuwa wapi, kisha baadaye wanaibuka watu ambao wana chuki isiyokifani tena wanakiri hadharani kuwa walikuwa wanamchukia...Hivi tunapata somo gani hapa?

Tujitafakari kama taifa!
Nongwa za kijinga hizi, kama ni mtu wa umri wa Mama yako hutakiwi hata kumjadili.
 
Wivu tena? Yaani rais kukumbatiwa kwenye film? Hata Reagan ali-act akiwa hajawa rais. Rais aliyeko madarakani huwa nafasi yake inachukuliwa na actor!
Umewahi kujiuliza kwa nini film ya Rise and fall of Idd Amin, nafasi ya Amin ilichezwa na mtu mwingine wakati yuko hai?
Umeshawahi kujiuliza Netanyahu akiwa kiongozi mkuu wa Israel alipata vipi muda wa kuwa actor akitengeneza filamu kama hii hii ya Royal Tour?. Hoja za kitoto kama hizi ni za facebook.
 
Mapicha picha tyuu ,sorry but in my Faith and Bealive Wemen wher not ment to be Leaders sio kanisan sio msikitini Hii kitu Impact yake in futer ni kubwa sana , mungu ibariki tanzania yangu nakupenda sana my Tz....
Wanaume ndio wanaandika kingereza broken kama hicho?. Hawafai kuongoza nchi basi.
 
Ila yule babu mtangazaji wa cbs news kapewa uhuru uliopitiliza..
Huyu mama anahitaji kuwekwa chini na kufundishwa taratibu..
Ana uzungu flani uliochanganyika na uswahili wa pwani..
Hili kosa lisirudiwe.
 
Hili linatafakarisha, japo watakuja wale wa kusema Muacheni mama afungue nchi na blah blah nyingine.

Anafungua nchi ndio, lakini ajitazame na ashauriwe, asikimbie mbio mpaka akapiliza kwako (kwake).

NB: Agents wapo kazini (Conspiracy theory)

US hana urafiki usio na faida kwake.
Ni kweli taasisi ya uraisi iheshimiwe
 
Umeshawahi kujiuliza Netanyahu akiwa kiongozi mkuu wa Israel alipata vipi muda wa kuwa actor akitengeneza filamu kama hii hii ya Royal Tour?. Hoja za kitoto kama hizi ni za facebook.
Alikuwa anashikana "arms akimbo" na director wa kike kama babu "pila" alivyoachiwa ?
 
Ku’act Movie [emoji327] au Filamu umeelewa maana ya hilo neno??? Litafakari kwanza mkuu
 
Vinchi vyetu hivi vidogo vidogo vinafahamika siku zote mpaka Ikulu na mataifa yenye nguvu. Kwa hiyo hakuna cha kuficha,wakati siku zote tupo uchi. Tuendelee tu kukaa uchi tena kwa Sasa tumekaa uchi ili tuingize pesa

[emoji3][emoji3][emoji3]na mm naongezea hatuna sababu za kupambana wala uwezo wa kushindana nao hatuna sasa ya niniii!!!

Magari tunayotumia,vifaa kwa ajili ya kujilinda vya technology ya leo pia kwao

Sometimes ukiwa mpinzan sana unapoteza maana na unapoteza wafuasi
 
Mapicha picha tyuu ,sorry but in my Faith and Bealive Wemen wher not ment to be Leaders sio kanisan sio msikitini Hii kitu Impact yake in futer ni kubwa sana , mungu ibariki tanzania yangu nakupenda sana my Tz....
Tuwe tunatumia Kiswahili badala ya kuharibu lugha za wengine bila sababu za msingi.
Bealive= believe
Wemen= women
wher= were
ment= meant
futer= future.
 
Kwa mlio bahatika kuona hiyo filamu na mmekerekwa kwa kiasi kikubwa namna hii basi tukubali kwamba Taifa limeachwa uchi kupitia filamu hiyo ya kipuuzi.
 
Wa-TZ wenzangu!

Wakati wa Wikileak nilitambua walioendelea na hasa US wanatumia maafisa wa ubalozini ili kuzifahamu nchi walimo. Balozi zao zinatumika sana kuwaelewesha tabia za viongozi wetu; uwezo na udhaifu wao.

Ina maana Peter Greenberg alikuja akiwa director wa film lakini naaamini kupitia ubalozi wake alishafahamu tabia za rais wetu hadi mambo ya ndani, na ukiangalia film hii, rais alichotwa akili hadi akamuona ni rafiki kuliko hata sisi wa-TZ.

Ukiangalia Film ya Royal Tour kiutu uzima, (Siyo kama mtoto anayefurahia wanyama) inatia kichefu-chefu jinsi rais wa nchi alivyopunguziwa thamani hadi kufikia kuwa mcheza film akiwa ikulu. Walifikia hatua ya kuitana majina kama wana mahusiano ya ziada. Peter! Mama Samia!

Haya yangeondolewa wakati wa ku-edit! Nadhani yaliachwa makusudi na naamini kwa uhusiano huu Peter sasa atatumika kiurafiki kuwasiliana na rais moja kwa moja.

Kule twitter Maria Sarungi kaibua jingine nami nimethibitisha. Wamasai wanaitwa ni 'PRIMITIVE' na huyo director wa film na ikaachwa kama sehemu ya maelezo ya film ya Tanzania! Yaani tuna raia PRIMITIVE! Rais Samia anaambiwa Magufuli alipatwa na COVID anakubali, Yeah! wakati wa-TZ hatujawahi kuambiwa jambo kama hilo. Kwa nini haya yote yametokea?

Ikulu yetu haina usalama. Namaanisha watu wanaostahili kumulazimisha rais aendane na matakwa ya taifa na siyo uamuzi wake, hawapo na hawana nguvu hizo. Ina maana rais mzembe anaweza angamiza taifa. Tabia zake binafsi zinatambaa na anazungukwa na watu wa aina yake bila kizuizi.

Very, Very Sorry!
Nikama vile Jiwe alivyotaka kuliangamiza Taifa. Ila swala la Jiwe kupata Corona usingelisikia hata kidogo kwani kwenye usukani walikuwepo Sukuma gang. Jiwe kafa kwa corona sababu ya kuamini ushirikina kuliko science
 
Wivu tena? Yaani rais kukumbatiwa kwenye film? Hata Reagan ali-act akiwa hajawa rais. Rais aliyeko madarakani huwa nafasi yake inachukuliwa na actor!
Umewahi kujiuliza kwa nini film ya Rise and fall of Idd Amin, nafasi ya Amin ilichezwa na mtu mwingine wakati yuko hai?
Hivi kweli Idi Amini angeweza kucheza maisha yake yale yaliyoigizwa? Labda upande mwingine wa maisha yake.
Tahadhari tafuta mfano mwingine.
 
Hivi wew kilaza lini utakuwa na akili!!???
Vijisent kidogo tu tiali ushaiuza nchi yako na ndugu zako..
Filamu ni mali ya mtu binafsi sasa raisi alicheza kama mtu binafsi au raisi!???
Hiyo hati miliki ya movie ni ya hao wafadhili au ni ya serikali!??
Kama kacheza hiyo movie ilikuwa ni sehemu ya majukumu ya raisi kwa siku 14
mbona haina hati miliki ya serikali???
Nimemaliza vilaza kama ninyi sina hamna nafasi ya kuendelea kujibizana na nami
pengine akili zitawarudi kwenye pumzi zenu za mwisho.
Wazee wa legacy mpo!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Usimsingizie Jpm, Magufuri hawezi kuchagua kilaza hawe makamu wake,huyu aliletwa na akina Kikwete, Magufuri mwenyewe anakili kuwa chaguo lake lilikuwa Hussein Mwinyi,ila alizidiwa nguvu na hakina Kikwete
Jiwe alikuwa bomu tena likateguka kabisa. Bora mama kuliko lile uaji mara 100
 
Huoni kuwa kutangaza utalii wa Tanzania kungeweza kufanywa na wizara husika na taasisi zenye uhusiano na utalii bila kumhusisha moja kwa moja mkuu wa nchi binafsi?
Wewe kinakuuma nini? Au ulitaka ukaigize wewe? Nyamafu, hizi ni akiri kama za Jiwe
 
Ati kuna Mwarabu alitaka kuwekeza eneo hilo wakati wa Awamu ya Tano lakini akanyimwa. Awamu hii amekubaliwa na anagharamia ujenzi wa makazi mapya ya hao Wamasai wanaohamishwa huko.

Kama ni kweli lengo lake ni kumilikishwa Hifadhi ya Ngorongoro, kwa jinsi hiyo, hakuna shaka hifadhi zote zitabinafsishwa kwa waliochangia utengenezaji wa filamu ya "Royal Tour" kwa kisingizio cha kuboresha na kuimarisha Utalii
Msukuma gang mnapata tabu sana, si kuna ile ya burigi? Polen sana lakini kikubwa kilichopelekea kushindwa kwenu ni ushamba wenu wa kuzaliwa
 
Ila hao jamaa wa Ikulu wote ukiwasikiliza ni hongera tu! Kumbuka wengine ndo maisha yao wameweza kufika US. Ukiwauliza mafanikio ya Royal Tour ni kufika US.
Mbona kama una wivu sana na watu waliofika Us kupitia Mama? Jiwe aliishia kuwapeleka chato
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Baraza la sanaa halikuipitia hii movie na kumpa adhabu huyo Beberu Peter?
Hoja nyingine sky eclat ni za kitoto sana zinaletwa hapa kwaiyo watanzania wanataka waonyeshwe jinsi gani usalama walivyokuwa Wana muongoza mama hivi uhalisia ungetokea wapi au wanataka waleteww behind the scenes jinsi peter alivyokuwa anakaguliwa anaongozwa ndio akili ziwatulie

Yule maria naye stress zinampeleka pabaya eti neno primitive limepigwa marufuku, hivi anajua maneno gani katika lugha yamebadilishwa matumizi ila bado yanatumika kama yalivyozoeleka yani wanaleta hoja za kitoto kwa watu wazima, yani wanajigeuza Wana linguistics kisa wanaongea kingereza

Hivi sehemu zile hatarishi kwenye movie mmeona mama anathubutu kushiriki mmeona mama kaingis shimoni merelani, mmemuona mama kapanda Lili limwamvuli Ile scene ya mwisho Serengeti au tunajitoa akili yani mama kushikwa mkono tu eti tunahatarisha hivi mnajua uyo peter alivyokuwa anaongozwa

Au mletewe behind the scenes ya kipindi mama anavua samaki muone usalama ulikuwa unazingua kile chombo tuache ushamba inatakiwa tujue Ile ni movie editing imefanyika na matendo mengine yamefanyika kuleta uhalisia

Mbona hawasemi tundu lisu au mbowe kipindi anaongea na mama hawakuhatarisha maisha maana video tunawaona wawili tu wanacheka wanaongea ila ya peter imekuwa nongwa😂😂😂😂
 
Miaka 60 ya uhuru tuliyoshindwa kuleta maendeleo yanayolingana na rasilimali zetu, ndiyo yanadhalilisha nchi siyo hiyo filamu.
 
Back
Top Bottom