Kwanza Kabisa..., kuendelea kama nchi tusiwe na nchi ya Samia, Mwendazake, Jakaya, au Yoyote atakayekuja kesho au keshokutwa.....
Kama taifa na kwa kuhusisha wadau na wataalamu lazima tujue ni wapi tunataka kwenda na kwa kutumia njia gani Sio kwa miaka kumi tu..., bali kwa miaka 50 mpaka 100 inayokuja..., yoyote atakayekuja madarakani ni kuhakikisha ile master plan ya nchi tuliyopanga inafuatwa (kwa mujibu wa wataalamu na sio wanasiasa) na kuendelezwa... Vipaumbele vidogo vidogo viwe ni kuweka nyufa na kuimarisha long term plans...
Kilichopo sasa ni muendelezo wa bandika bandua anzisha, acha kila kukicha... Siasa zinakuwa nyingi..., ukiangalia hata kero hazijabadilika ni zile zile miaka nenda rudi.., ila kila mtu akija ni kupapasa papasa tu... ili aonekane mimi nilifanya hiki au kile...
Na hii tabia ya kuhusisha maendeleo ya nchi na mtu au Chama fulani ( ni kuwatenga baadhi ya watu ambao nao ni nguvu kazi) Maendeleo yawe inclusive na yawahusishe wadau wote no matter Chama chao au itikadi zao....