Rais Samia ameanzia Mwanza Kujenga Hekalu letu: Tayari kamaliza msingi, kuta na linta, bado kuezeka

Rais Samia ameanzia Mwanza Kujenga Hekalu letu: Tayari kamaliza msingi, kuta na linta, bado kuezeka

Hapana, that's a wrong approach. Approach hiyo ndiyo inatufanya tuwe tujisifu hata tusivyostahili.

Bigger picture - linganisha mwaka # 1 tulikuwa wapi na mwaka # 60 tuko wapi. Period.
Hizo "performance metrics" hapo kati pretty much zinaji even out zenyewe (in my opinion there are more negatives than positives).

By the way, ninatumia jina la "Chadema" nilidhani ungeelewa - kama hujaelewa nimeitumia katika context gani then hata hii discussion ni kupotezeana muda tu.
Mosi, contextual meaning is always ambiguous.

Hivyo, lazima wewe kama mwandishi uweke bayana unalokusudia pale una=oandika neno "Chadema."

Pili, unasema: "Hizo performance metrics hapo kati pretty much zinaji even out zenyewe, in my opinion there are more negatives than positives."

Katika debate, kauli hii haiwezi kukupa score.

Unapaswa kuweka ushahidi mezani ili kuilinda.
 
Nami Mama Amon naipokea rejea yako ya hoja ulizozitoa kwenye bandiko kuu na hii inayojibu hoja zangu.

Ilani ya CCM inaweza kuwa na mapungufu kwa kuwa inahusu Sera za Chama za kuielekeza Serikali yake mwelekeo wa nchi Kijamii, Kisiasa, Kiuchumi na Kitejnolojia. Ilani hiyo imekuwa ikitayarishwa kutokana na malengo yaliyomo kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa, 2025 (Development Vision 2025). Kwa kuwa hiyo Dira haijarejewa, bado ni mwongozo halali wa maendeleo ya nchi hii.

Serikali uwajibika kuandaa na kutekeleza Mpango unaojibu Sera zilizomo kwenye Ilani ya Uchaguzi. Kabla ya kila bajeti, Wizara ya Fedha na Mipango huandaa mpango wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha unaofuata, ambao ndio huwa mwongozo wa bajeti husika.

Umetoa hoja kwamba kuna umuhimu na uharaka wa kukamilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano ambao unafafanua ilani, na kuweka msingi wa mipango ya mwaka mmoja mmoja na bajeti zake. Naamini umepata na kupitia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2021/22 - 2025/26, nakala ambayo nimeiambatanisha. ITAPENDEZA kupata maoni yako.View attachment 1820638
Asante kwa kiunganishi cha Rasimu ya FYDP III.
Narudi hapa hapa na review kamili very soon.....
 
Njaa na vilio kila kona , mafuta juu, mchele juu, serikali haina pesa , miradi inajiendea kwa kusua sua, Hakuna shift za 24hr.
 
View attachment 1819542
Rais Samia Suluhu Hassan akiwa Mwanza akitafakari juu ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2021/22 hadi 2025/26

Tangu serikali ya wamu ya sita, chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ilipoanza kazi nimekuwa najiuliza maswali yafuatayo, kama sehemu ya kazi yangu ya utafiti:

  1. Serikali ya awamu ya sita inasema kwamba kwa sasa mwaka 2021 sisi kama Taifa tuko wapi?
  2. Serikali ya awamu ya sita inataka sisi kama Taifa tuwe tumefika wapi ifikapo mwaka 2025?
  3. Serikali ya awamu ya sita inataka tutekeleze kazi/miradi gani ili sisi kama Taifa tuweze kufika huko?
  4. Serikali ya awamu ya sita inataka tutekeleze vipi kazi/miradi husika ili sisi kama Taifa tuweze kukamilisha safari yetu?
  5. Serikali ya awamu ya sita inasema kuwa safari yetu sisi kama Taifa tangu 2021 hadi 2025 inahitaji rasilimali/fedha kiasi gani?
  6. Serikali ya awamu ya sita inafikiri kwamba sisi kama Taifa tutajuaje kuwa tumefika mwisho wa safari yetu ya miaka 5?
Nilikuwa nasubiri kwa hamu Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2021/22 hadi 2025/26 ili kuona majibu ya maswali haya. Lakini, kabla mpango huo haujazinduliwa, naona maswali haya yameanza kujibiwa kwa kina kupitia hotuba za Rais.

Tayari Rais Samia amemaliza ziara ya kikazi mkoani mwanza alikokaa kwa siku tatu. Alisema kuwa Kanda ya Ziwa ni Ukanda wa Kiuchumi utakaoitumia Mwanza kama kituo kikubwa cha biashara katika nchi za Maziwa Makuu.

Akiwa huko alizindua miradi kadhaa ikiwemo mradi wa maji, mradi wa reli ya kimataifa, mradi wa chelezo ya meli, mradi wa daraja la Ziwa Viktoria, na miradi ya kuwawezesha vijana kunufaika na fursa za ajira 8,000,000 zinazotengenezwa na serikali kwa ajili yao.

Rais alitaja sekta zifuatazo kama vyanzo vya ajira za vijana hawa: mradi wa umeme wa mwalimu Nyerere, Miradi ya Ujenzi wa Barabara, na Mradi wa bomba la mafuta. Pia alitaja miradi ya kilimo, miradi ya ufugaji, miradi ya uvuvi, na miradi ya TEHAMA inayotekelezwa kupitia ubia wa serikali na sekta.

Kuhusu suala la ajira, RC Kafulira alimwahidi Rais Samia kwamba mkoa wake wa Simiyu unakusudia kuchangia 2.5% ya ajira zote, yaani ajira 200,000, kutokana na kuzalisha ajira kupitia minyororo ya ongezeko la thamani ya huduma na bidhaa zilizoko katika sekta mbalimbali mkoani humo.

Kwa mujibu wa hotuba ya jana ya Waziri wa Tamisemi, Ummy Mwalimu,
asilimia baki ya ajira itazalishwa nchini kote katika maeneo yafuatayo: wilaya 126, halmashauri 184, kata 3,956, vijiji 12,319, vitongoji 64,384, na mitaa 4,263.

Na kwa mujibu wa
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Florens Luoga, katika mwaka 2019, pato la Kanda ya Ziwa lilikuwa TZS bilioni 34, sawa na 25.9% ya Pato la Taifa.

Aidha, Luoga anasema kuwa Kanda ya Ziwa huzalisha zaidi ya 90% ya dhahabu yote nchini, 50% ya pamba na kahawa na zaidi ya 95% ya mauzo ya samaki ndani na nje ya nchi.

Ziara ya Rais Samia huko Kanda ya Ziwa Viktoria ni mwendelezo wa pilika zake za kujipambanua kama mjasiriadola wa kike kwa kukutana na makundi mbalimbali ya kijamii ili kuwaeleza ndoto aliyo nayo kuhusu Tanzania mpya chini ya serikali ya awamu ya sita.

Kwanza alikutana na wazee kupitia wazee wa Dar es Salaam, kisha akakutana na kina mama kupitia kina mama wa Dodoma, na leo amekutana na vijana kupitia vijana wa Mwanza.

Nimesikiliza hotuba zake zote tangu Dar es Salaam, Dodoma hadi Mwanza. Ni hotuba nzuri kwa ajili ya kueleza ndoto aliyo nayo juu ya Tanzania mpya.

Kutokana na kauli zake nilizozisikia mpaka sasa, Rais anayo majawabu yafuatayo, kwa maswali yaliyotajwa hapo juu:

  1. Serikali ya awamu ya sita inasema kwamba kwa sasa mwaka 2021 sisi kama Taifa tuko wapi? Serikali inasema kuwa hapa tulipo kuna
    • magonjwa,
    • ujinga,
    • ikolojia duni,
    • ofisi za utawala zinazosuasua katika kutoa huduma kwa watu,
    • na uchumi usiojali maslahi ya pamoja kwa ajili ya makundi yote ya watu.
  2. Serikali ya awamu ya sita inataka tuwe tumefika wapi ifikapo mwaka 2025? Serikali inataka kuona kila Mtanzania akiwa na maisha yanayoendana na kipato cha uchumi wa kati , kwa maana ya kipato kinachoweza kuchochea upatikanaji wa
    • afya bora,
    • elimu bora,
    • ikolojia bora,
    • ofisi zinazotoa huduma kwa kasi, kwa usawa na kwa wote, katika namna inayoendana na imani ya jamii ya kitaifa ambayo ni msingi wa ujenzi wa jamii ya amani.
    • na uchumi unaojali maslahi ya pamoja kwa ajiliya makundi yote ya watu.
  3. Serikali ya awamu ya sita inataka tutekeleze kazi/miradi gani ili tuweze kufika huko? Serikali inasema kuwa kazi zifuatazo lazima zitekelezwe:
    • Kuchochea maendeleo ya rasilimali watu, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa makundi yote ya watu wakiwemo vijana, wanawake, wazee, watoto, wajane, yatima na walemavu;
    • Kuchochea utajiri wa Taifa kupitia uvunaji wa maliasili, uzalishaji mali, kubuni na kukuza kanda za kiuchumi;
    • Ujenzi wa taasisi za kiuchumi, kisiasa na kijamii zinazotoa huduma bora kwa kasi, kwa usawa na kwa wote ;
    • Kuimarisha usalama wa nchi na mahusiano ya kimataifa yaliyo bora zaidi;
    • Kutunza mazingira na kufanya menejimenti ya mabadiliko ya tabianchi;
    • Kujenga imani ya jamii na jamii ya amani kwa kukuza na kuhami mila, maadili na tunu za Taifa;
    • Kuweka mipango ya maendeleo yenye kuonyesga bayana vigezo vya ufanisi, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wake.
  4. Serikali ya awamu ya sita inataka tutekeleze vipi kazi/miradi hii ili tuweze kukamilisha safari yetu? Serikali inataka kutekeleza miradi yake kwa
    • kusimika uongozi bora,
    • kujenga mfumo wa sheria unaoruhusu utoaji wa haki,
    • kujihusisha na ujenzi wa miundo mbinu wezeshi kama vile upatikanaji wa nishati na maji,
    • kukusanya rasilimali fedha,
    • kuchochea ushirikishwaji wa makundi yote ya kijamii, na
    • kusimamia uwajibika wenye tija na kasi.
  5. Serikali ya awamu ya sita inasema kuwa safari yetu tangu 2021 hadi 2025 inahitaji rasilimali/fedha kiasi gani? Kiasi cha rasilimali zinazohitajika ni Shilingi trilioni 115 ambazo ni
    • bajeti za miaka 5,
    • Bajeti za wizara zote,
    • Bajeti za Halmashauri zote,
    • na bajeti za mawakala wote wa serikali.
  6. Serikali ya awamu ya sita inataka tujueje kwamba tumefika mahali ambako serikali inataka kutufikisha? Kuna vipimo vya ufanisi vinaandaliwa kwa ajili ya kupima kasi na ufanisi wa
    • kila wizara,
    • kila Halmashauri,
    • kila wakala wa serikali,
    • na kwa kila mwaka.
Hivyo, kusudi kauli za Rais zipate msingi imara wa usimamizi na ufuatiliaji, namwalika Waziri wa Fedha kufanya haraka ya kukamilisha uandaaji na uzinduzi wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa 2021/22 hadi 2025/26.

Waraka huu unapaswa kujibu maswali yote haya kwa kina, Hivyo ni muhimu zaidi kuliko Ilani ya Uchaguzi kwani utafafanua mambo haya kwa kina katika njia inayoruhusu usimamizi na ufuatiliaji. Ilani ya chama ni muhimu, lakini inapaswa kubaki kama "kiambatanisho" kwenye andiko hilo muhimu.

Kwako Waziri Mwigulu Lameck Nchemba: Kasi ya Rais Samia ni kubwa kuliko kasi ya Ofisi yako. Kuna kitendeakazi muhimu kinakosekana mikononi mwa Rais--Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (21/22-25/26). Huu ndio waraka pekee unaopaswa kujibu maswali yote hapo juu kwa urefu na upana wake.

View attachment 1820640
Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Kwa hiyo basi, changamka kuziba pengo hili ambalo ni kinyume cha mazoea bora ya kiutendaji yanayotutaka kuanza utekelezaji baada ya kukamilisha mipango.

Nilichojifunza hapa wewe ni meandishi mzuri ila sijaona jipya ni kama risala ilioandikwa kwa ustadi.

Baada ya awamu ya Mkapa na JK CCM haijawahi kuwa na mipango yenye tija ya muda mrefu kwa nchi hii.

Bahati mbaya sana Mwendazake hakuwa muumini wa long vision plan, aliacha makovu ambayo Mama Samia anapambana nayo sasa mpaka yaje yakae sawa itachukuwa muda kidogo
 
Nilichojifunza hapa wewe ni meandishi mzuri ila sijaona jipya ni kama risala ilioandikwa kwa ustadi.

Baada ya awamu ya Mkapa na JK CCM haijawahi kuwa na mipango yenye tija ya muda mrefu kwa nchi hii.

Bahati mbaya sana Mwendazake hakuwa muumini wa long vision plan, aliacha makovu ambayo Mama Samia anapambana nayo sasa mpaka yaje yakae sawa itachukuwa muda kidogo
Hivi mkuu kweli unaweza kusema Kikwete alikuwa na long term plan kumzidi Magufuli? Yaani katika nchi hii ni rahsi sana kutawala maana wengi ni mazo...bi. Magufuli atabaki kuwa ndo Rais aliyeangalia mbali sana kuliko hao wanaohangaika kufurahisha watu.
 
Hivi mkuu kweli unaweza kusema Kikwete alikuwa na long term plan kumzidi Magufuli? Yaani katika nchi hii ni rahsi sana kutawala maana wengi ni mazo...bi. Magufuli atabaki kuwa ndo Rais aliyeangalia mbali sana kuliko hao wanaohangaika kufurahisha watu.
Hamna kitu mnamahaba tu na mwendazeke, hakuwa na chembe ya sifa za uongozi.
 
Tanzania Bora haitakuja kwa hotuba nzuri tu. Kama hotuba nzuri zipo zile za baba wa Taifa. Nchi zote mahitaji vitendo katika kutatua keto zinazowakabili vijana wetu, badala ya maneno matamu ya kisiasa. Wanasiasa waache kukwepa kushughulikia keto muhimu. Idadi kubwa ya vijana hawana ajira, serikali ije na suruhu ya Hilo, badala ya kuhadaa watu eti wanaweza kujiajiri. Wapi? Wapi? Lazima miradi na uwekezaji mkubwa ufanyike kuwapa ajira watu. Nchini Afrika ya kusini, mazingira ya uwekezaji wa kampuni za kichina wanajenga viwanda na kutatua tatizo la vijana kukosa ajira angalau hata Kama haliishi kabisa. Ebu tuache upambe usiosaidia. Labda Kama lengo lako no kupewa wadhifa serikalini
Niseme mawili.

Kwanza, hotuba nzuri per se sio kosa. Lakini niongeze kusema kuwa, hapa siongelei hotuba nzuri pekee. Naongelea hotuba na mipango ya utekelezaji inayotekelezwa tangu sasa kwa mujibu wa hotuba husika katika ziara ya Rais Samia.

Sayansi ya matendo yenye ufanisi (praxiology) inatufundisha kuwa nadharia, utendaji, na tathmini (theory, action, review) vinakwenda pamoja. Kwa hiyo, hotuba nzuri ni mwanzo mzuri unaopapswa kusifiwa, labda kama unachuki binafsi na mtoa hotuba. Hivyo, baada ya hotuba nzuri, sasa yafaa tuongelee haya mengine bila kuziponda au kuponda mleta hotuba: utendaji na tathmini.

Pili, unaongelea lengo la "kupewa wadhifa serikalini" kana kwamba hii ni dhambi. Kiu ya madaraka ndiyo kanuni pekee inayosukuma gurudumu la maisha katika sekta zote za maisha ya watu.

Kuna madara ya kiuchumi, madaraka ya kisiasa, madaraka ya kidini, madaraka ya kijamii, madaraka ya kimaarifa, madaraka ya kimapenzi, na orodha inaendelea. kwa hiyo, by itself, lengo la "kupewa wadhifa serikalini" haliwezi kuwa dhambi.

Madaraka ni matamu, na ndio maana wakati mwingine yanatafutwa kwa "kupenyeza rupia," kama unavyojua vizuri. Kinachotofautisha wenye madaraka ni jinsi walivyoyapata na jinsi wanavyoyatumia, basi.
 
Nami Mama Amon naipokea rejea yako ya hoja ulizozitoa kwenye bandiko kuu na hii inayojibu hoja zangu.

Ilani ya CCM inaweza kuwa na mapungufu kwa kuwa inahusu Sera za Chama za kuielekeza Serikali yake mwelekeo wa nchi Kijamii, Kisiasa, Kiuchumi na Kitejnolojia. Ilani hiyo imekuwa ikitayarishwa kutokana na malengo yaliyomo kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa, 2025 (Development Vision 2025). Kwa kuwa hiyo Dira haijarejewa, bado ni mwongozo halali wa maendeleo ya nchi hii.

Serikali uwajibika kuandaa na kutekeleza Mpango unaojibu Sera zilizomo kwenye Ilani ya Uchaguzi. Kabla ya kila bajeti, Wizara ya Fedha na Mipango huandaa mpango wa utekelezaji kwa mwaka wa fedha unaofuata, ambao ndio huwa mwongozo wa bajeti husika.

Umetoa hoja kwamba kuna umuhimu na uharaka wa kukamilisha mpango wa maendeleo wa miaka mitano ambao unafafanua ilani, na kuweka msingi wa mipango ya mwaka mmoja mmoja na bajeti zake. Naamini umepata na kupitia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa 2021/22 - 2025/26, nakala ambayo nimeiambatanisha. ITAPENDEZA kupata maoni yako.View attachment 1820638
Mkuu,
Salama? Ombi lako nimelifanyia kazi, na majibu yangu yanapatyikana hapa: Uhakiki wa Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Serikali
 
Back
Top Bottom