Rais Samia amefanya vizuri ndani ya miezi saba madarakani

 
Amefanya vizuri kuzuia demokrasia?!
 
Nakubaliana nawe kwa kiasi kikubwa. Maeneo aliyo-fail kabisa:

1) Kuruhusu polisi kuendelea kuwa kundi la kigaidi linalobambikia watu kesi

2) Kushindwa kutambua kuwa jaki ya vyama vya siasa kufanya mikutano ni haki ya kikatiba na wala siyo utashi wa Rais.

3) Kurithi baadhi ya maelekezo ya kijinga ya Rais mtangulizi wake yanayokiuka katiba wakati akitambua wazi kuwa Rais mtangulizi wake au alikuwa dikteta au ni kweli tatizo la afya ya akili, kuna wakati lilikuwa likimrudia.

4) Tozo kubwa kwenye miamala bila ya kuzingatia ukweli kuwa, kama ilivyo serikali, na wananchi nao wapo kwenye hali ngumu za kiuchumi.

5) Kutofanya au kuanza mchakato wowote wa kufuta sheria gandamizi zilizoasisiwa na marehemu Magufuli.

6) Kikiri kuwa polisi wanafanya kazi kama genge la wauaji, na hivyo kuua watuhumiwa wakiwa mikononi mwao lakini bila ya kuchukua hatua dhidi ya uongozi wa jeshi la polisi.

Mazuri mengine uliyoacha kuyaweka:

1) Kutengua uwaziri wa baadhi ya mawaziri waongo na wapenda sifa kama Kalemani na Chamuriho.
 
😻
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😻
 
Tangu ashike madaraka sasa ni miezi Saba lakini tumeona mafanikio makubwa kwa aliyo fanya, rais alianza na kurejesha mahusiano na majirani uhusiano ambao ulikuwa umedora kwa kiwango kikubwa mno, sasa hivi wafanya biashara Wana peleka biashara zao kwenye nchi tunazo pakana nazo bila ya vipingamizi vyovyote.

Makusanyo ya Kodi yameongezeka tena Kodi isiyo ya dhuluma na kazi zake tayari zimeanza kuirudia jamii kwenye nyanja za elimu, madarasa yana jengwa nchi nzima, zahanati zinajengwa na kuboreshwa nchi nzima, ajira zime endelea kutolewa, wafanyakazi wamepandishwa madaraja, Barabara Zina endelea kujengwa nchi nzima, miradi yote iliyo anzishwa na awamu ya tano yote inaendelea.
Uhusiano kimataifa umerejea, tulitengwa mpaka tuka Baki kujipendekeza kwa wachina na kuwasifia Sana.

Kwa kweli mama Samia kwa muda mfupi amefanya mengi na bado tutarajie mengi.
Hongera Ila Kuna ka kikundi kadogo kenye mfumo dume ambako bado aka amini juu ya kuongozwa na mwanamke Hako ndo kanaona Kila analofanya rais sio zuri kwao sambamba na hao pia Kuna wenye ukabila ambao walidhani kuwa huwenda kabila lao lingetawala milele.

HONGERA KWA RAIS WETU.
 
i. Kubadilisha mwelekeo wa nchi kuhusu ugonjwa wa korona- kwamba upo, na Tanzania inahitaji kuungana na dunia kupambana na tishio hili kwa njia za kisayansi.
2. Kukubali kutoa taarifa WHO
3. Kukubali chanjo ya korona
4. Kufanya kazi na IMF, kupata economic stimulus package ili kuthibiti makali ya UVIKO 19
5. Rural infrastructures
6. Fedha za madarasa
7. Kurudisha mahusianao ya Kimataifa
 
Umetumia kipimo kipi ili kuja na hili bandiko la sifa?
 
Kaupiga mwingi kwa upande wako unaye nufaika na kupata shibe
 
Kwakuwa unaajira ya kudumu, machinga walahoi walikuwa wamekuzuia pakupita
Uvccm wenye ajira wapo kama vipofu maana hawasikii wala kuona shida za wenzao
 
Mkuu naona unampigia mbuzi gitaa
 
Kichwani mwako ni empty,hata unayemsifia anakuona wewe ni bogus! kabisa
Omtiti siku hizi naona umeamua kutuliza akili hasa baada ya kuondokewa na jiwe.
 
5. Kuimarisha Demokrasia, hii bila kusahau hotuba yake Umoja wa Mataifa.

6. Uhuru wa kuzungumza na vyombo vya habari.

HAPA BADO !
Kuchagua kutukamua kupitia miamala
 
Haya masifa alikuwa anayapenda Mwendazake, sidhani kama huyu wa sasa yupo interested nayo! Moja ya matabia ya hovyo kabisa aliyoyaacha jamaa ni kutengeneza waimba MAPAMBIO kama wewe, awamu hii hata upambe vipi hupati kitu!! Muulize Sabaya (Alienda kupiga mapambio Clouds kilichomtokea na kinachomtokea haamini), Muulize Musiba pia na Tanzanite lake (Both Kijarida and TV)!
 
Wewe leta hoja hapa ndio zitaamua kama wewe ni great thinker au la, usilazimishe vyeo. Pia, kama hujui mipango ya hii nchi ina maana hata bajeti ya nchi hauijua na huo u great thinker wako sijui umeupataje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…