Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu nadhani sote tumeendelee kusikia kile kinachojiri huko mkoani Kilimanjaro ambako Mh. Rais wetu yupo huko. Ndugu zangu ukimfuatilia Mh. Rais wetu hata kabla ya kuwa Rais wetu ni kiongozi aliyekuwa akipenda kuona haki ikitendeka kwa watu wengine bila kujali hali zao.
Hali hiyo na tabia hiyo ya Mh. Rais wetu bado anayo, bado ulimi wake unahubiri haki. Bado anahitaji kuona kila kiongozi aliyepewa dhamana ya uongozi anatenda haki. Anataka kuona kila mwenye dhamana ya kuamua haki kwa mujibu wa sheria anatoa haki kwa haki. Anataka kuona watu wasikae magerezani wakibubujikwa machozi kila siku kwa sababu tu walionewa na kunyimwa haki.
Mh. Rais wetu anataka kuona na amedhamiria kuona haki inatamalaki kila eneo na kila mhimili wa dola, anataka kuona mikono ya viongozi inakuwa safi, anataka kuona watu wanakwenda jela kwa haki na hata wakiwa jela iwe ni sehemu ya kufundishwa na kurekebishwa tabia huku haki zao na utu wao ukilindwa vyema.
Mikono ya Mh. Rais wetu hakika Ni misafi, kinywa cha Rais wetu kimejaa hekima na busara kubwa sana, kifua cha Mh. Rais wetu kimetamalaki upendo kwa watu wote. Ni kiongozi wa kuigwa, kupigiwa mifano na ambaye huwezi ukawa na Shaka naye juu ya dhamira yake katika kuwatumikia wananchi.
Hii ndio sababu huwezi ukaona sasa hivi kiongozi akimdhalilisha mtumishi wa umma mwenye familia hadharani kwa makosa yasiyo yake. Ndio maana huwezi ukaona mambo ya kuvunjiana heshima na kushushiana heshima maana wateule wa Mh. Rais wameshatambua kuwa Mh. Rais wetu ni mtu wa haki kimaneno na kimatendo.
Hakika Mwenyezi Mungu anatupenda sana watanzania, hajawahi kutuacha wapweke wala wakiwa. Mama Samia ni Joshua wetu anayetupeleka Kanaan, hatuna budi kuendelea kumuunga mkono Mh. Rais wetu mpendwa. Tuendelee kumuombea afya njema na maisha marefu.
Tuendelee kumuombea ili Mwenyezi Mungu amjalie nguvu za kututumikia. Mimi kama kijana ninaiona Tanzania inayomekameka katika uongozi wa Mama yetu. Kesho yetu ni njema sana watanzania, Tanzania ni salama na ipo katika mikono salama sana. Mikono ya Rais wetu ni safi, kinywa cha Mh. Rais wetu ni safi, ulimi wa Mh. Rais wetu ni safi na Tanzania ni safi, kazi iendelee.