Rais Samia amerithi nchi iliyofilisika kifedha na kiuchumi

Sasa wewe mpuuzi unashindwa nini kuelewa kuwa falsafa ya Uncle Magu ilikuwa ya kutumia alichokikuta tu na kujizolea Sina hebu Taja mkamkati wake wowote wa uzalishaji? Afadhali wenzake walijaribu kilimo kwanza, mkurabita, mikopo ya wajasiriamali, big results now nk yeye sisi matajiri huo utajiri umetoka wapi hakujiuliza
 
Uwe unaficha ujinga wako...Bi Mkubwa kakopa Tirioni 10 ndani ya mwaka mmoja, mbona hili hulisemei? Huoni kwa rate hii mama atamchukua mama miama miwili mpaka mitatu kuvunja record ya Mtangulizi wake?
Tatizo lenu mwendazake masalia ndio hapo mnapokosea!!ndio maana jk aliwaambia wenzenu wanaleta hoja wajibuni kwa hoja ila nyie mnakimbilia marungu!! Hiyo trilioni 10, umeitoa wapi nenda ukaangalie hadi leo hii deni na taifa ni shilingi ngapi, toka lile aliloliacha KAMBALE!!ndio uje na hiyo hoja yako kuwa mama ameshakopa hizo trilioni 10!!
Jaribuni kuwa mnatofautisha sio kila pesa inayotoka kwa beberu ni mkopo, Hivi prof.macho kodo yupo wapi, "sisi hatutishwi na mabeberu Tz, ni nchi huru" daa ila ki ukweli KUENDESHWA NA WAPOLIPOLI, tuliona mengi sana!!zito bwana, eti nchi imekabidhiwa kwa washamba!!!
MUNGU FUNDI
 
Serikali ya awamu ya tano na ya sita ni ileile( Ni zao la uchaguzi wa 2020).
RAIS aliyeweka uchumi wa Tanzania vizuri ni BENJAMIN WILLIAM MKAPA( Alilipa Sana DENI LA TAIFA, angalia takwimu). KIKWETE NAYE aliongeza pia ukubwa wa deni la Taifa. sifa za wakati wa KIKWETE ni maisha yalikuwa rahisi , watu Walikuwa wanafuraha, Kuongeza wigo wa utoaji elimu, kujenga miundo mbinu ya barabara, kukuza demokrasia, kutaja machache.
Naona umemtaja ZITTO KABWE( kama mshauri wa uchumi, kuwa ilimpasa Magufuli amsikilize). Kwanini, usimtaje Profesa. Ibrahim Haruna Lipumba( full bright professor), au CAG mstaafu( Prof.MUSSA ASAD), kama hawa wanazuoni hawakusilizwa ZITTO KABWE ni nani hata asikilizwe?
Pia, kumsikiliza ZITTO KABWE ni sawa na kutafuta taarifa kwenye mtandao ambapo inabidi uwe vizuri kichwani(lasivyo, unaweza ukapata hitimisho lisilo sahihi)).
Sasahivi, Kuna watu wanakatwa Kodi mara mbili kabla hela hawajapata lakini ZITTO KABWE simsikii akilalamika( Je, malalamiko yake yanatokana na ukiukaji wa sheria za uchumi au vinginevyo?).
 
Hakika hapa nachojifunza NI kuwa hatuna ushahidi wa Nini kilifanyika hasa katika uchumi wakati wa JPM na Sasa ila tunakwenda na biti za watu wachache.,.. Navyojua hapa maisha halisi ya kitaa ndiyo yanaonyesha Hali halisu ya hawa watawala wetu . Tuliona wakati wa JK Hali ilivyokua na hata Sasa tupo tunaona nchi hii inakosa wachambuzi na wadadisi wa Mambo hivyo kwenda na tune au biti za watawala Hapa ndiyo kusema AKILI ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO. Tunuache aliyepita tungange na yaliyopo na yanayokuja . Utawala uliopo uje na majibu ya Hali ya kitaa na sio kuja na sababu za aliyepita aliwahi kusema mzee Ruksa KILA KITABU NA ZAMA ZAKE. JPM aliandika chake na Sasa zamu ya Mama anaandika chake.
 
Kikwete was the best, angeongoza miaka 20, Taifa lingekuwa mbali Sana, kiuchumi na kisiasa.
 
Baada ya kuweka tozo pesa ipo sasa mbona hatuoni hayo maajabu yakifanyika.

Kila siku mnasingizia marehemu tu.
 
Takataka za kijinga kuziba hoja za kushwinda vibaya kwa bibi yenu. Mkubali tu Bi tozo anatuumiza sana wananchi. Sana hakuna biashara inashamiri kila kitu kimekufa.
 
Binafsi siipendi sisiemu ila ukweli ndio huu. Mama analaumiwa bure ila alieharibu ni yule mwamba
 
Huu ni utumbo mtupu mods naomba fita hii takataka..futaaa..Yani umeona watanzania wooote wajinga...hahaha..kwahiyo unataka wafuate mawazo yako..jomba sijui dada
Wewe ndio takataka. Tuliza hasira soma tena huenda ukaelewa. Jamaa katoa uchambuzi mzuri sana
 
Kwahiyo mana yako Ndio anarekebisha Kwa kuwapa watu maisha magumu ?! Kwa kuwaongezea mshahara elf 20 then kawapandishia bei vitu asilimia 200 [emoji16][emoji38][emoji38]
Sasa unataka hela atoe wapi?
 
Watu wameshasahau kuwa hata mishahara tulikuwa tunapokea tarehe ya 45 ya mwezi....Kuwa na heshima kwa marehemu angalau kidogo!
 
Huu uzi uko sawa sana ila MaCHADEMA yakuja hara humu tubaki na shombo tuuu
 
Kuna kundi la vijana wengi wewe ukiwa mojawapo ambao mnatumika aidha kwa kulipwa au kwa ushabiki maandazi kuongea na kuandika taarifa na habari potofu ambazo huwa sielewi huwa mnatoka nazo wapi ila ukizisoma unajiuliza haya mnayoandika huwa mnayatoa wapi maana mnaandika vitu as if sisi wengine hatupo nchi moja na ninyi au sisi wengine tunaishi china.

Kimsingi hizi taarifa au huu uzi wako umejaa upotoshaji wa hali ya juu. Pengine wewe ni mtoto mdogo wa juzi tu kuzaliwa na umeyapata haya kwa mzazi wako au ndugu yako au umesoma sehemu bila kujua unasema kitu gani. Sisi wakubwa zako ambao tumekimbiza mwenge tokea enzi za mwinyi haya mambo unayoyaongea kishabiki tumeyashuhudia na kuona kila jambo kwa ushahidi wa macho bila kuhadithiwa.

1. Si kweli kwamba enzi za Mkwere ajira zilitolewa rasmi bali kulikuwa na idadi kubwa ya wafanyakazi hewa kwenye taasisi za kiserikali ambao walijichomeka aidha kwa kuingizwa na ndugu zao au kufanyiwa connection za kulipana kwa kukatana kwenye mshahara kama kodi bubu kwa mtu aliyekupa mchongo wa kukupachika. Hawa watu mimi ninawafahamu wengi sana. Walikuwapo mahakamani, ATCL, bandarini, TRA, MUHIMBILI, IKULU, BUNGENI, na taaisisi mbali mbali za serikali.

Si hapo tu bali hata ugawaji wa tenda ulikuwa ni wa kujuana na usiozingatia taratibu za tenda za serikali hivyo watu waliokuwa katika meza za maamuzi waliweza kugawa tenda kwa ndugu, jamaa, au marafiki wazi wazi kabisa na kuweza kujipatia tenda kwa njia za upendeleo hata kama hizo kampuni hazijakidhi vigezo. Unakumbuka ile skendo ya Mkurugenzi wa Tanesco kuunda kampuni ya stationary inayosimamiwa na mkewe na kujipatia tenda ya bilioni 400,unakumbuka tenda ya Rada,unakumbuka manunuzi ya ndege ya raisi,unakumbuka, manunuzi ya vitu mbali mbali kupitia kivuli cha taasisi za kiimani,kielimu na hata kupitia wizara na ofisi ya raisi?!

Hii hali ukitazama ilitoa ajira kwa raia wengi sana ila kiuchumi na kisheria haikuwa sahihi sababu ilikuwa inaruhusu ufujaji mkubwa wa fedha za uma na kufanya raia kuwa na pesa mifukoni na kuharibu uwiano kati ya pesa ya hazina, mzunguko wa pesa, nguvu ya mamlaka za serikali na taasisi zake mzunguko wa pesa.

Kwa wanaliosoma uchumi wanajua impact ya hili jambo kama haujui pia naomba uulize maswali nitakuelekeza hapo kuna mengi sana ya kukuelekeza unaonekana haufahamu impact ya kiuchumi raia wakiwa wana access na fedha ya uma bila utaratibu wa kisheria.

So sio kweli kwa ajira zilikuwa rasmi zilikuwa ni ajira bubu, watu walikuwa wanapata nafasi serikalini bila taratibu za kisheria. Kuna watu wamepata nafasi kwa vyeti vya kughushi, kwa vyeti vya watu wengine, kwa vyeti halali ila bila kupitia mamlaka ya utumishi huku wenye sifa wakiwa mtaani etc. Sijui sasa kama hili unalijua namna unasema kuwa Mkwere alitoa ajira sijui hizo ajira unazosema wewe zilikwenda kwa utaratibu upi?

2. Si kweli kuwa kipindi cha Mkwere kulikuwa na ulipaji wa kodi mzuri au biashara ziliflorishi kwa uzalishaji mzuri kwasababu kuna kampuni kama Azam kipindi Magu anaingia ilitakiwa kuilipa serikali zaidi ya tsh Bilioni 7 kama malimbikizo ya kodi kwenye kiwanda chake cha Dar baada ya TRA kuikadiria malipo ambayo hayakulipwa kipindi cha nyuma. Kampuni nyingi hazikuwa zikilipa kodi isipokuwa zilikuwa zikilipa hongo kwa viongozi wakubwa na wadogo ili zipate ulinzi na kutosumbuliwa na mamlaka ambazo zinawaghasi na malipo yasiyoeleweka. Kuna kampuni kama KIOO inayotengeneza chupa. Nenda pale kapeleleze utapewa stories za viongozi wakubwa kwenda kupewa mlungula. Tungeweka hapa details ila ni mambo ya siri. Kuna kampuni. Kimsingi kodi zilililipwankadiria ya wahusika walipojisikia ila hakukuwapo na ulipaji ule unaotakiwa. Sisemi kuwa alipoingia Magufuli kodi ililipwa sawa sawa ila nasema kodi kipindi cha Mkwere haikukusanywa vile namna umeandika hapa as if kulikuwa na makusanyo halali na yaliyosawa sawa, si kweli.

3. Kuhusu mapato ya serikali pia umepotoka sana. Kwa mara ya kwanza tokea awamu zote kuingia madarakani, ni kipindi cha awamu ya Magufuli pekee ndipo kulitanuliwa wigo wa makusanyo ya mapato kwa wingi kihistoria. Tafakari jambo moja, halimashauri, taasisi na idara zote kuwekewa control number hapa nazungumzia Tanesco, idara za maji mikoa yote Tanzania, halimashauri, hospital, vituo vya polisi, askari barabarani, na makampuni yote kuwekewa utaratibu hela zote ziende hazina bila mtu yoyote kugusa hata mia. Yaani unaponunua umeme kule hazina wameshajua kuwa umenunua umeme wa buku na makato ya serikali ni tsh fulani.

Wewe unadhani Magufuli alipata wapi jeuri ya kununua ndege mfululizo, kuanzisha mamiradi makubwa ni kwasababu alishakaba kila mia ya hii inchi kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa kila malipo yanaonekana hazina, je unajua ni pesa kiasi gani ilikuwa inakusanywa kwa mwezi, au unasikiliza hizi story za vijiwe vya kahawa kuwa Magufuli alikuwa anakopa ndio anafanya matumizi?

Si kila jambo uambiwe as if hauna macho mengine jaribu kutumia akili yako yaani tumia ufahamu wako na upeo ukiambiwa hili ni chungwa na hili ni chenza basi tumia milango yako ya ufahamu kunusa, kulamba ujue ladha, kutazama na hata kusikiliza ujue kweli hiki ninachoambiwa ni chenyewe.

Pesa ya ndani ilikuwa ni ya kutosha sana na iliweza kuendeleza miradi midogo na mikubwa. Ni kweli Magufuli pia alikopa ila alikuwa ameshatathimini kiwango cha mapato ambacho kingeweza kuyalipa hayo madeni ya riba ndogo ambayo masharti yake ni nafuu.

Nakupa homework nyingine, fuatilia aina ya mikopo aliyokopa Magufuli na masharti yake halafu tazama mikopo ya awamu ya mkapa, na kikwete na hii ya sasa utaona nyuma yake kuna nini. Kukusaidia mikopo ya taifa kama marekani ni mikopo mibaya sana sababu unakuja na masharti ya kutaka kukushika kimaamuzi na inalekeza kabisa nenda kafanye ABC. Huo ni mkopo sasa au kitu gani?!

Mchina unamwambia naomba mkopo yeye anatazama tu kama utaweza lipa kwa viwango vyako vya mapato na rasilimali kama huwezi ana adjust au anakuwekea sharti la collateral kuwa ukishindwa mradi atashika yeye hadi deni liishe, mifano ni kama pale sri Lanka (kasome history ya ule mradi wa bandari utaona.

Marekani anakukopesha halafu anakupangia upeleke eneo Fulani yaani kahela anakupa kwanza kidogo halafu kanakuja na mkataba wa utekelezaji na anajua utekelezaji hautakufaidisha hata kidogo in the future ila utabakia na deni ambalo atalitumia kuku bully kiuchumi, kisiasa na kijamii siku zijazo. Nenda kasome mikataba ya miradi ya ufadhili na miradi ya misaada au mikopo kutoka mataifa ya magharibi kama US.

Jambo lingine ni vema kuwa makini sana na watu wanaojiita wapinzani si wote ni watu wazuri. Tazama enzi za Kikwete hawa mabwana walikuwa wakibweka pale maslahi yao yalipoguswa ila wakipata kipozeo wanakaa kimya kama vile ilivyo sasa. Sidhani kama unamuona Zitto akiongea lolote na ameweka ukaribu sana na serikali ya bi mkubwa hii inakwambia jambo gani?

Wanao ongea ni wachache sana na tunawaona ila wale wazee wa press wamepotea kabisa sasa ila nikuulize hali ni nzuri mtaani ewe mleta uzi? Kihistoria kiuchumi tukitoa kipindi cha nyerere kipindi kile cha njaa, hakuna wakati mfumuko wa bei umekuwa haueleweki kama wa sasa. Kumekuwa na Creeping effect ya mfumuko wa bei kwa maana kila sehemu kumekuwa na ongezeko la gharama ambazo ukizijumlisha unagundua pesa haitoshelezi kubajeti matumizi binafsi au ya familia.

Kwa mara ya kwanza maisha yanakuwa ni magumu bila sababu za msingi ukiuliza inasingiziwa vita ya Ukraine. Hivi unatakiwa kuwa mjinga kiasi gani ushindwe kutofautisha hali ya uchumi ikiwa kuna watu wanatuchezea akili ili wao wachukue na kutapanya pesa ya uma na kama kweli hali si nzuri kiuchumi kila mtu anateseka?!

Nenda huko nje ya mji katazame watu walikuwa wamesimama ujenzi wa mabangaloo na mahekalu wameanza tena kuyafumua na kuanza ujenzi upya tena kwa kasi ya radi. Hizo ajira za kupeana zimerudi sasa kwa kasi watu wanachomekana humo mawizarani na kulipana nje ya payroll. Sensa ndio hiyo unaambiwa bajeti ni bilioni 600 na zaidi ila ukijaribu kukokotoa kwa kichwa matumizi yake kutokana na ripoti tunazopewa na wadau unakuta pesa haiwezi tumika hata kwa 70% kuna upigaji mkubwa.

So ndugu, nina mengi ya kukuhoji na kujadili ila nafasi haitoshi. Ila acha kupotoka na kupotosha wengine kwa kutoa taarifa batili au ambazo hazina uhalisia.

Mikopo inayokopwa sasa mingi anabambikiwa au atabambikiwa Magufuli ili yeye abebe msalaba wa lawama ila ukweli ni kuwa hazina imekuwa inapokea pesa nyingi sana na Magufuli alikuwa haweki wazi sababu ya aina ya wapinzani waliokuwa wamemzunguka lakini pia alikiwa anaficha taasisi kubwa za ulaya ambazo zimekuwa zikimtazama kwa jicho la hofu kama lile walilomtazama Gaddafi wa Libya, Saddam Hussein wa Iraq na wengineo ambao wameonyesha maamkizi ya kutaka kutoka katIka mikono ya mataifa ya ki imperialist kama US.

Hebu uwe unajifunza na kutafiti kisha observe kwa akili yako. Acha kulishwa matango pori halafu unakuja kuongea kwa confidence hapa as if haya mambo ni ya kuhadithiwa na yametokea watu tukiwa na akili timamu na tupo hapa hapa mjini tukijionea nyeusi na nyeupe.

Mnyonge nyongeni ila haki yake mpatieni.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magu alikuwa kafilisi nchi, yeye na wachina na waturuki
Miradi mingi iliyofunguliwa na inayoendelea kufunguliwa sasa na ambayo imesimama ni matokeo ya makubaliano ya kibiashara na mataifa hayo.

Sasa ngoja uone US ambaye amerudi kuwa mdau wa maendeleo kama kuna kitu kipya mtamfanya hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameongea upuuzi mwingi hadi aibu nimeona mimi. Kimsingi kijana amepotoka vibaya.

Ni mawili , aidha ni wale watu wanaotumika kupotosha jamii ili kuwapumbaza na kutaka kusaidia serikali ya sasa ionekane haina dosari.

Au ni mtu ambaye hajui anachokisema amebakia kuropoka tu mambo asiyoyajua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…