Rais Samia amesahau hili la umeme ni yeye amelileta, tumkumbushe

Sioni tatizo hapo,Yuko sahihi rais wetu,yeye ndo Yuko jikoni anajua Nini Kiko kwenye chungu,hebu chukulia yeye Kama mpishi anawaambia walaji kuwa leo jioni kila mtu atakula vipande vitatu vitatu vya nyama,na baadae anagundua kuwa mahesabu yake hayakuwa sahihi hivyo anaamua kubadilisha mauzi na kuamuru kila mtu atakula kipande kimoja kimoja Cha nyama,so utampinga kisa tu alikuahidi kuwa utakula vipande vitatu?

Yeye ndo anajua kwenye chungu Kuna nini,hivyo lazima aamue kipi kifanyike,piga kazi mama!!!
 
Kazi ya serikali ni kutoa huduma, na pale inapobidi huduma hushushwa kwa wananchi na serikali hujazia. Kama mwananchi atatakiwa kulipia actual price ya huduma husika mbona mafuta ya petrol na diesel hawauzi kwa bei halisi waliyonunulia huko nje plus usafiri mpaka bandarini?
 
lkn miondombinu ya mjin ni rahisi kufikika kwa mteja,kuna uwepo wa barabara zinazopitika na pia mabonde ni machache ukilinganisha n vijijini..

Imetumika method gan kuweka bei kubwa kwa mtu aliepo ubungo karibu na station alipe kwa bei elekezi alafu yule wa nanyumbu akalipe kwa 27000??
 
Umeme na sukari nchi hii ni masuala magumu Sana.
 
Ebana huyo wa mwisho hiyo sauti kama katekenywa vileπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Huyu mama ni hatufai kamweee,sijui ni kwanini watanzania hatuelewi ,kama leo wamekata umeme tangia saa 12 asubui mpaka sasa saa 10 na nusu bila bila utafikiri familia zetu zinaenda kula milo mitatu ikulu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…