Rais Samia amesahau hili la umeme ni yeye amelileta, tumkumbushe

Rais Samia amesahau hili la umeme ni yeye amelileta, tumkumbushe

Sioni tatizo hapo,Yuko sahihi rais wetu,yeye ndo Yuko jikoni anajua Nini Kiko kwenye chungu,hebu chukulia yeye Kama mpishi anawaambia walaji kuwa leo jioni kila mtu atakula vipande vitatu vitatu vya nyama,na baadae anagundua kuwa mahesabu yake hayakuwa sahihi hivyo anaamua kubadilisha mauzi na kuamuru kila mtu atakula kipande kimoja kimoja Cha nyama,so utampinga kisa tu alikuahidi kuwa utakula vipande vitatu?

Yeye ndo anajua kwenye chungu Kuna nini,hivyo lazima aamue kipi kifanyike,piga kazi mama!!!
Huyuhuyu wa dollar billion elfu sita, wa teuzi fake na mipasho? Bado hujanishawishi.
 
Hapo wanamtuhumu Kalemani wakati ilikiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM na wao wakainadi..Sasa wakati CCM wanashusha hawakujua kuwa hawanahera?

Fedha umma zinaliwa na wizara ya fedha, nadhani zinazobakia hazitoshi.
 
Ukweli nikwamba kuunganishiwa Umeme kwa 27 elfu ni hasala kwa Tanesco,maana lazima tujue kwamba hivyo vitu vina nunuliwa .
.
Hata hivyo inafaa kuweka Bei nafuu kiasi ,mfano nguzo si sahihi mteja kulipia sawa na mteja kulipia miundombinu ya simu ,Kama simu hatulipi inafaa na Tanesco kuondoa gharama hiyo .

Pili Meter luku isizidi tsh 150,000\=
unaijua maana ya REA
 
Suala la umeme ni gumu sana, sijawahi ona hawamu yoyote iliyoweza kuleta suluhu kwa wananchi, leo wanakwambia mara elfu ngapi mara laki ngapi lakini kuna watu hata tuambiwe milioni tatu tuko tayari kulipia ili tupate huduma ya umeme lakini kila ukienda TANESCO wanakuzungusha tu yaani binafsi naona hili shirika libinafsishwe
 
Kwasasa watanzania tutaona viroja sana na inawezekana ndio tukawa sasa watu wa ajabu zaidi duniani & huyo hangaya ni tatizo tena kubwa kwa taifa maana hana maamuzi anamtegemea mtu nyuma yake
 
Meter imeandikwa ni Mali ya Tanesco ,lakini mtumiaji na mwangalizi Ni mteja husika, ndiyo maana hata ikisumbua anaye hangaika kuhakikisha inafanya kazi ni mteja.
Bahati mbaya serikali haijaweka mazingira sawa ju ya maswala ya Umeme .

Inafaa Sasa iruhusu kampuni binafsi ziwekeze kwenye sector hii. Ili kuondoa ubabaishaji na unyonyaji unao fikiriwa na wananchi!
Hatuhitaji kampuni binafsi bali tunahitaji uwajibikaki kama aliokuwa anaweza kuufanya magufulo
 
Hakika pale TANESCO panajambo gumu. Samia hajapajua vizuri, naamimi ipo siku atakuja kujichanganya tena.

Mwaka jana June 2021 Rais Samia mwenyewe akiwa katika ziara zake alisema yafuatayo.

Rais Samia : Lakini pia upande wa umeme si ndio?
Wananchi: Ndioo!
Rais Samia : Umeme tumeshusha bei ya kuunganuisha umeme.
Wananchi: wakapiga ndelemo na makofi!
Rais Samia : Mulikuwa Munaunga umeme kwa laki ngapi?
Wananchi: Laki tatu wengine taki nne!
Rais Samia : Tumeshusha mpaka shiling elfu 27.
Wananchi: wakapiga ndelemo na makofi!
Rais Samia : Hiyo ndio kazi ya serikali ya Chama cha mapinduzi.

Wananchi: wakapiga ndelemo na makofi!



Jana 4th January 2022 tena akasema tuliharibiwa. "Tulihariniwa katikati hapa kwa kusema, kila mwananchi ataungiwa umeme kwa shilingi Elfu 27, Sio hivyo".

Siku akikutana na ESCROW na DOWANS ndio atajua hajui.
Mkuu umenivunja mbavu leo, nanukuu Wananchi wakapiga ndelemo na makofi! hapa kidogo umesahau pia wakaongezea kwa kusema kwa ndelemo tano tena kwa mama. Hivi hizi bei za Tanesco ndio hizo hizo na kule Zanzibar? kwa maana jamaa huwa wanagoma kulipia umeme ati. Tano tena kwa mama hah hahaaaaa. Hizi ni sarakasi za mpigaji February Marope na wahuni wenzake, uhuni huu umekuja mara tu baada ya yeye kuwa mkuu wa umeme. Nilijua tu huyu aliyekuu muuza ving'amuzi mr mabeans Tanesco ni maji marefu sasa ugali wote umekuwa uji,maji yamezidi unga.
 
Hapo wanamtuhumu Kalemani wakati ilikiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM na wao wakainadi..Sasa wakati CCM wanashusha hawakujua kuwa hawanahera?
Uhuni wote huu umetokea baada ya Kalemani kuondoka, wahuni wanarudi tena kwa kasi ya 5G kwenye sekta ya umeme, huu ukweli ndio hata Ndugai anaujua,sasa wahuni wametengeneza mazingira ya kuanza kufanya biashara ya faida kwa asilimia 100.
 
Mimi naomba kama ameona hivyo aondoe ile tozo ya REA tunayotozwa kwenye luku na mafuta
Ni kweli maana lengo lake ni kupunguza makali ya gharama za kuunganisha umeme.
 
Kinachofuata ni kupandisha bei ya unit za umeme
 
Anayefaham gharama za kuvuta umeme Zanzibar aziweke hapa tulinganishe.
 
Ukweli nikwamba kuunganishiwa Umeme kwa 27 elfu ni hasala kwa Tanesco,maana lazima tujue kwamba hivyo vitu vina nunuliwa .
.
Hata hivyo inafaa kuweka Bei nafuu kiasi ,mfano nguzo si sahihi mteja kulipia sawa na mteja kulipia miundombinu ya simu ,Kama simu hatulipi inafaa na Tanesco kuondoa gharama hiyo .

Pili Meter luku isizidi tsh 150,000\=
Umeme ni huduma sio biashara kwa TAnesco na serikali, ilitakiwa waunganishe bure kwa wananchi wote kisha kukata pesa kidogo kidogo kwenye bill za Luku.
 
Back
Top Bottom