Rais Samia ameshazidiwa na wapigaji suala la bei ya petroli?

Acheni huu ujinga Chini ya cccm hakuna kitu kitabadilika
 
Serikali haiwezi kufanya Biashara
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Yani wewe ukiona Magu anasifiwa unaumwa kabisa!

Magufuli katika kipindi chake hakuwahi kupunguza kodi za kubet na pombe alafu anaongeza kodi kwenye mafuta!

Ni katika kipindi hiki tu
 
One of the best reading of the pertaining situation, I would say.

"Tunafungua nchi",; na bado!

Unafungua nchi na hukuandaa chochote kukabiliana na ufunguzi huo, lazima upigwe tu.
Ngoja tusubiri kuona nani "atamzingua" mwingine, 'cartels' au Samia?
Ndugu kuweka MIKODI Mingi kwenye Mafuta mlitegemea nini?
 
Hii nchi ni ngumu sana!!wewe bajeti ya maendeleo ni 20%halafu matumizi ya kusimamia hayo maendeleo iwe 80% hapo kuna nini? Ndicho kinachopelekea kuumiza wananchi tu.
Kweli hapo kuna shida katika hiyo 80% ndio kuna mishahara na marupurupu ya wabunge waliopitisha hiyo bajeti

Kwa lugha rahisi hili bunge halina faida yoyote kwa wananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Yani wewe ukiona Magu anasifiwa unaumwa kabisa!

Magufuli katika kipindi chake hakuwahi kupunguza kodi za kubet na pombe alafu anaongeza kodi kwenye mafuta!

Ni katika kipindi hiki tu
The problem, unachukulia mambo too personal!!

Sasa unataka niseme "kweli, enzi za Magu ali-control bei ya mafuta" hata kama hakufanya hivyo! Na hakufanya hivyo sio kwa HAKUTAKA kufanya hivyo, bali kama nilivyosema, NO ONE can have a control on oil price unless tufute au kupunguza kodi!!

Au kama unataka nijitie upofu na kushangilia Magu alivyokuwa ame-control bei ya mafuta hata kama si kweli, je tumlaani pale bei ilipopanda soko la dunia, na hatimae Tanzania bei kuwa Sh 2,409? Na kama kufuta bei kwenye betting na kuongeza kwenye mafuta, mbona bado hiyo 2018 mafuta yalikuwa juu?!

Unajua tofauti yangu na wewe ni ipi?! Wakati wewe unachukulia mambo too personal, na kuwa tayari kupotosha ukweli kama pale uliposema Magu alihakikisha bei haivuki 2200, mimi nayaelezea kwa uhalisia wake!!

It doesn't matter mada husika iwe inamhusu Magu or anyone else!!! Lakini mara kwa mara inatokea kum-challenge Magu kwa sababu ni Wafuasi wa Magu ndio wenye tabia ya kumpamba Magu hata pale asipostahili!!

In short, nampa mtu kile anachostahili... Magu hatunae na sasa tunae Samia!! Huyu nae akifanya nisiyokubaliana nayo (haijalishi niwe nipo sahihi au hapana), nae tutamfanya kama Magu tu!!!
 
Ningekuona una akili kama ungeungana na wanaolalamikia bei kupanda badala yake unatetea tu ukilinganisha na kipindi cha Magu kwamba nako ilikuwa hivyo hivyo.

Yani wewe ukiona watu wanalalamika sasa hivi unahisi wanamuonea Samia na kumpa ujiko Magu! [emoji23][emoji23][emoji23]

Ndugu hiyo bei ya 2400 hata kwa Magu watu walilia!

Ungekuwa na akili zaidi ungeunagana nao na kujiuliza kwanini Zambia na Burundi na Rwanda wanaochukua mafuta hapa bei zao zipo chini kuliko sisi
 
Ndo maana wamegawa gesi kwa mchina ili waendelee kutupiga kwenye mafuta, na sasa wanatafuta kumpa bandari ya bagamoyo ili aue bandari zetu na akusanye kila kitu.......yaani tunajiweka rehani kwa mchina ili baadaye tuishi kwa kutegemea fadhila zake tu, baaaasi!
 
Mnyororo wa upigaji ni mrefu sana, ukute hata hao unaodhani watasimamia haki pia ni sehemu ya huo mnyororo wa upigaji!! Eleweni mnapoona watu wanaununia mradi wa standard gauge!!
 
Yaani unataka niongee kama nisiyejua ninachoongea, sio?! Yaani naona kabisa bei ya mafuta soko la dunia imepanda maradufu, halafu bado unatarajia nishangae kuona bei Tanzania imepanda?

As economist, mambo ya kiuchumi huwa naongea kiuchumi na sio kisiasa!!

Btw, unaweza kunionesha post yako ya kulalamikia kupanda kwa bei ya mafuta July 2018!!

Kwamba eti nikiona watu wanalalamika naona wanamuonea Samia, kuna mangapi nimemkosoa huyo huyo Samia?!

Halafu kama kawaida yako... tayari umeshaanza matusiin other way round, jambo ambalo mara kwa mara huwa napishana na wewe!!!
 
The Boss, bila shaka wewe ni Mtanzania. Ninasikitika sana kwamba sisi Watanzania hatujielewi au hatueleweki. Bajeti ilisomwa vizuri na kuainisha ongezeko la baadhi ya bidhaa ikiwemo mafuta kwa shilingi 100 na lengo likiwa limewekwa bayana. Je, tulitarajiwa huo mzigo utamwangukia nani kama sio sisi walaji Watanzania? Sasa hii hamaki inayokuja baada ya kuanza kutekelezwa kwa bajeti inatoka wapi? Tuache unafiki!
 
Rwanda, Burundi na Zambia wanaochukua mafuta hapa na bei zao zipo chini wao mafuta yao yanatoka soko tofauti na la dunia hii?
 
Hata Kama Watu Wataendelea Kubisha Ukweli ni Kwamba CCM ndo tatizo Nchi hii....
 
"...Wakati Mwiguli anasoma bajeti pale bungeni nyie mlikuwa busy kusaini petition ili Diamond atolewe kwenye tuzo za BET,!"
By Crimea
 
Wakati bajeti inasomwa wao walikuwa busy kushangilia Sabaya kupelekwa kisongo na kusaini petition ya kumtoa Diamond kwenye tuzo za BET
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…