Rais Samia ameshazidiwa na wapigaji suala la bei ya petroli?

Rais Samia ameshazidiwa na wapigaji suala la bei ya petroli?

"...Wakati Mwiguli anasoma bajeti pale bungeni nyie mlikuwa busy kusaini petition ili Diamond atolewe kwenye tuzo za BET,!"
By Crimea
[emoji23][emoji23][emoji23]Nawashangaa sana kujifanya wanashtuka saa hii!
 
Kweli Hawa jamaa jeuri Sana,waliwahi kuipa serikali ya Kikwete siku tatu lol. Kwa vile wameona style ya mama ni ileile ya Kikwete wameanza Tena.
 
Bei ya Petroli kwa lita
Zambia 1800
Rwanda 1800
Kenya 2000
Tanzania 2400

Naona Mama keshaanza kuzidiwa mapema sana na wapigaji
Oil cartel hii imeshasambaza 'hela'za kutosha huko Ewura na kwingineko now
Wana panga bei wanavyotaka...

Hii Cartel ina watu jeuri Sana waliwahi kumgomea Kikwete kushusha bei kama mnakumbuka. Wanataja sababu zao za kupandisha bei lakini ukitazama nchi jirani ambazo zingine mafuta yanapitia kwetu unashindwa kabisa kuelewa.Ewura wanaitumikia serikali na wananchi au wanawatumikia hawa Oil cartel.

Kenya kwa kulazimisha big oil companies ziwe listed Stock exchange imewasaidia Sana transparency na kuwadhibiti..

Sisi niliona Magufuli alikuwa anajaribu TPDC wauze mafuta kwa kuwa na vituo kila mkoa lakini naona now hiyo policy nayo itakufa na sidhani kama ingesaidia sana.

Dawa ilikuwa kuwalazimisha kama Kenya wawe listed kwenye soko la hisa.

Na serikali inunue hisa kwa baadhi ya hizo kampuni kulazimisha transparency.

Otherwise naona Mama washamzidi na Ewura isharudi mifukoni mwa hawa wapigaji...
Mkuu ni kweli kabisa tunaoishi tunduma tunaenda kujazia mafuta nakonde(Zambia) then tunaludi
 
Kuna vitu tunashindwa kuelewa ndani ya bunge kumejaa makundi tofauti ,kuna watu wapo kwaajili ya kupendekeza mambo yao yasoge mbele, kuna watu wapo kwaajili ya posho , kuna watu wapo kwaajili ya uongozi n.k

Ndio maana kuna wananchi tumezama kwenye mtego kushindwa kuelewa nini maana ya KATIBA.

Leo Dubai, Sheikh Zayed Road, maeneo ya Business Bay. Mji wenye wenyeji ambao hawana muda wa porojo. Mji ulikuwa jangwa sasa ndio hivyo tena, wana rasilimali moja tu, petroli,yote inaenda kwenye mji na wananchi wake. Tusione vinaelea, vimeundwa.

Hospitalini hakuna dawa, shuleni hakuna viti, wabunge mishahara haitoshi nchi unahitaji kujengwa yaani sh 100 HAITOSHI! Wafanye hata 500. Maana wananchi wenyewe vichwa vigumu kuelewa.
Kuwa na Katiba Mpya isiyotekelezwa is useless.
 
Wamepunguza kodi kwenye betting wanaweka kwenye mafuta halafu watu ni member wa economic forum!!
Huhuhu mpaka naogopa.
Ukizungukwa na wapiga deal....eti wafurahisha watu..utavuna mabua.
 
Kuna mtu alisema humu, hawa ma-CAG wanatoa ripoti kulingana na ulaji wake na mamlaka iliyomteua.

Kinachofanyika kwa sasa ni kuruhusu kila mtu afanye kwa namna yake bila kuingiliana kwenye reli, kama awamu ya nne tu; usimshike mtu mkono.

Akili iliyotumika kuharibu, haiwezi kutengeneza.

Tumia akili
'thestate' inaongozwa na wa msoga?
Nchi imerudi awamu ya nne(John-walker).
 
Inshu sio EWURA, juzi wakati kodi ya mafuta inaongezwa mlikuwa mnashangilia, sasa leo tena mnaanza kulia!??hizo nchi ulizotaja miaka yote bei ya mafuta huko ni chini kulinganisha na TZ, na sio mafuta tu, hata sukari!!hizo polices ni za zamani kwa sasa haziwezi kufanikiwa kamwe, hicho kituo kilifunguliwa musoma mbona bei yake ya mafuta haikuwa na utofauti na vituo vingine??!!eti una shusha kodi ya pombe, unaongeza kodi ya mafuta unategemea nini si usanii tu kwani lazima kila kitu kitapanda tu.
Kata magufuli walimtandikia khanga na walilia Sana Leo wanamnanga hatari najiuliza Ni Hawa Hawa watanzania ?
 
The Boss,

Fuatilia bei ya mafuta kwenye soko la dunia, na utaona tangu mwezi wa 6 uanze, bei imekuwa ikipanda tu...

Kwa Zambia, siwezi kushangaa bei kuwa chini kwa sababu mwanzoni mwa mwaka huu kuna baadhi ya kodi waliziondoa kwa kampuni zinazoagiza mafuta!!

Sina uhakika na hiyo bei ya Rwanda ulikoitoa, lakini kwa mujibu wa mtandao wa Global Oil Price, inaonesha bei ya petrol Rwanda ipo juu tena pengine kuliko Tanzania.

Sipo Kenya, lakini kwa mujibu wa EWURA ya Kenya, bei ya petrol kwaMombasa ambayo tunaweza kuiweka kundi moja na Dar ipo KSH 124.72 ambayo ni zaidi ya Sh 2600 za Tanzania. Labda Manyan'au akina Tony254, Teargas, na MK254 waje ku-verify hizo bei za Kenya kutoka Energy & Petroleum Regulatory Authority ambapo inaonesha Nairobi, lita moja ya petrol (super) ni KSh. 127.14 ambazo ni takribani TSh. 2700/=

Je, wewe hizo bei umezitoa wapi?
Unatetea upumbavu
 
Kata magufuli walimtandikia khanga na walilia Sana Leo wanamnanga hatari najiuliza Ni Hawa Hawa watanzania ?
Nadhani hawa unaowasema wanamnanga na wale waliotandika kanga ni watanzania wa aina tofauti; watandika kanga wengi ama wote hawapo na hawana mpango wa kujibizana kwenye mitandao, pita mitaani usikie stori zao, harakati zao ndo utajua.

Hawa unaosema wanamnanga ndo wale kipindi fulani hupitia kuwashawishi watandika kanga kuchagua vyama fulani kwa malipo ya kanga, tshirt na kofia. We elewa tu, si wamoja!
 
Nyie watu mnapenda sana Magu kumpa sifa zisizo zake!!! Magu hakuwa na uwezo wa ku-control bei ya mafuta, bali ilikuwa ukiona ipo chini, basi bei hata soko la dunia ipo chini!!

Magu angekuwa na uwezo wa ku-control bei za soko la dunia basi angefanya hivyo hata kwa mazao ya wakulima!!
Wanaongelea mafuta bwana @ chige
 
Nchi hii hatutakaa tupate maendeleo chini ya tawala zinazofanya biashara

Unategemea nini kwa mpanga bei ya Mafuta ndiye mfanyabiashara ya mafuta.

Leo nimesikitika sana kuona dar es salaam mafuta 2400 Je mikoa ya Songwe, Katavi,Rukwa na Kigoma Bei itakuwaje?

Maajabu ni kuwa Zambia mafuta bei rahisi wakati mafuta yao yanapita hapa na wanatulipa kodi

Haya ni maajabu ya Dunia!.

Ewura na Bulk Procurement ni entities za serikali. Ina maana wao hawaoni shida iko wapi? Au sisi tunatunga matatizo sababu hatufahamu yanayoendelea ndani ya sector hiyo ya mafuta?
Hizo kodi zinazoomgezwa zina impact kubwa kiasi gani kwenye mafuta?
Nafikiri tunawasingizia makampuni ya mafuta. Sio kweli wanajipangia bei wenyewe
 
Rwanda, Burundi na Zambia wanaochukua mafuta hapa na bei zao zipo chini wao mafuta yao yanatoka soko tofauti na la dunia hii?
Nirudie mara ngapi?! Nimekuambia Zambia wameondoa matozo na kodi kwa kipindi cha miezi 6, kuanzia February hadi August!

Btw, hizo bei za chini kwa Rwanda na Burundi, ni chini kulinganisha na nchi ipi, na hiyo bei ni ipi?! Huoni busara ingekuwa ni kutaja?!

Anyway, angalau tutumie figures za mtandao wa globalpetrolprice.com, ambao wanaanza kwa kusema:-
The differences in prices across countries are due to the various taxes and subsidies for gasoline. All countries have access to the same petroleum prices of international markets but then decide to impose different taxes. As a result, the retail price of gasoline is different. Use the drop menu to see the prices in gallons.
Na ndicho tumesema kinachotofautisha kati ya Zambia na majirani zake!!

Na kwa mujibu wa mtandao huo huo wa globalpetrolprice.com, wanasema as of June 28 (current available data), bei ya mafuta Rwanda inaonesha ni $1. 106 na Burundi ni $1. 208.

Nimekosa official data za Burundi, lakini Rwanda Utilities Regulatory Authorities (EWURA ya Rwanda) inaonesha ceiling price ni Rwf 1,088 kwa lita. Na kwa msaada wa Google's Currency Conveter, hiyo Rwf 1,088 ni takribani $1.10 ambayo ni karibu TSh 2,560; and therefore, I can conclude that, takwimu za globalpetrolprice.com zinaaminika, na kwahiyo inawezekana hata bei ya Burundi ikawa ndo hiyo ya $1.20!

Na nikukumbushe tu kwamba, hizo ni bei zilitangazwa mwishoni mwa mwezi May 21, na kwa maana nyingine, kuna uwezekano mkubwa ni bei kwa mafuta yaliyoingia nchini humo somewhere in May, huku yakiwa yametoka sokoni somewhere in April au March, kipindi ambacho bei yake soko la dunia ilikuwa cheaper kulinganisha na miezi iliyofuata!!
 
Wanaongelea mafuta bwana @ chige
Najua wanaongelea mafuta, tatizo wanataka kutuaminisha Mheshimiwa Magu alikuwa anadhibiti bei ya mafuta wakati ukweli ni kwamba, wakati over the past 5 years, bei zetu zimekuwa zikitegemea bei ya soko la dunia!!

Tatizo watu wana kumbukumbu mzuri ya bei ndogo mwaka 2020, lakini wanasahau corona ilifanya bei ya mafuta soko la dunia iporomoke sana, na hivyo kutufaidisha hadi sisi huku!!!
 
Nirudie mara ngapi?! Nimekuambia Zambia wameondoa matozo na kodi kwa kipindi cha miezi 6, kuanzia February hadi August!

Btw, hizo bei za chini kwa Rwanda na Burundi, ni chini kulinganisha na nchi ipi, na hiyo bei ni ipi?! Huoni busara ingekuwa ni kutaja?!

Anyway, angalau tutumie figures za mtandao wa globalpetrolprice.com, ambao wanaanza kwa kusema:-

Na ndicho tumesema kinachotofautisha kati ya Zambia na majirani zake!!

Na kwa mujibu wa mtandao huo huo wa globalpetrolprice.com, wanasema as of June 28 (current available data), bei ya mafuta Rwanda inaonesha ni $1. 106 na Burundi ni $1. 208.

Nimekosa official data za Burundi, lakini Rwanda Utilities Regulatory Authorities (EWURA ya Rwanda) inaonesha ceiling price ni Rwf 1,088 kwa lita. Na kwa msaada wa Google's Currency Conveter, hiyo Rwf 1,088 ni takribani $1.10 ambayo ni karibu TSh 2,560; and therefore, I can conclude that, takwimu za globalpetrolprice.com zinaaminika, na kwahiyo inawezekana hata bei ya Burundi ikawa ndo hiyo ya $1.20!

Na nikukumbushe tu kwamba, hizo ni bei zilitangazwa mwishoni mwa mwezi May 21, na kwa maana nyingine, kuna uwezekano mkubwa ni bei kwa mafuta yaliyoingia nchini humo somewhere in May, huku yakiwa yametoka sokoni somewhere in April au March, kipindi ambacho bei yake soko la dunia ilikuwa cheaper kulinganisha na miezi iliyofuata!!
Endelea kumtetea mama mkuu!
 
Bei ya Petroli kwa lita
Zambia 1800
Rwanda 1800
Kenya 2000
Tanzania 2400

Naona Mama keshaanza kuzidiwa mapema sana na wapigaji
Oil cartel hii imeshasambaza 'hela'za kutosha huko Ewura na kwingineko now
Wana panga bei wanavyotaka...

Hii Cartel ina watu jeuri Sana waliwahi kumgomea Kikwete kushusha bei kama mnakumbuka. Wanataja sababu zao za kupandisha bei lakini ukitazama nchi jirani ambazo zingine mafuta yanapitia kwetu unashindwa kabisa kuelewa.Ewura wanaitumikia serikali na wananchi au wanawatumikia hawa Oil cartel.

Kenya kwa kulazimisha big oil companies ziwe listed Stock exchange imewasaidia Sana transparency na kuwadhibiti..

Sisi niliona Magufuli alikuwa anajaribu TPDC wauze mafuta kwa kuwa na vituo kila mkoa lakini naona now hiyo policy nayo itakufa na sidhani kama ingesaidia sana.

Dawa ilikuwa kuwalazimisha kama Kenya wawe listed kwenye soko la hisa.

Na serikali inunue hisa kwa baadhi ya hizo kampuni kulazimisha transparency.

Otherwise naona Mama washamzidi na Ewura isharudi mifukoni mwa hawa wapigaji...
Mkuu huyo mama si alisema wameongeza kodi kwenye mafuta?

Ccm Wakiongeza kodi wafanyabiashara na ewura wafanye nini?
 
Nchi hii hatutakaa tupate maendeleo chini ya tawala zinazofanya biashara

Unategemea nini kwa mpanga bei ya Mafuta ndiye mfanyabiashara ya mafuta.

Leo nimesikitika sana kuona dar es salaam mafuta 2400 Je mikoa ya Songwe, Katavi,Rukwa na Kigoma Bei itakuwaje?

Maajabu ni kuwa Zambia mafuta bei rahisi wakati mafuta yao yanapita hapa na wanatulipa kodi

Haya ni maajabu ya Dunia!.
Lakini pia msisahau kwa Tanzania kodi kwenye mafuta zipo zaidi ya 10. Anayesababisha bei kuwa juu ni hii Serikali yetu ambayo wanaoiendesha uelewa wa uchumi ni zero.
 
Bei ya Petroli kwa lita
Zambia 1800
Rwanda 1800
Kenya 2000
Tanzania 2400

Naona Mama keshaanza kuzidiwa mapema sana na wapigaji
Oil cartel hii imeshasambaza 'hela'za kutosha huko Ewura na kwingineko now
Wana panga bei wanavyotaka...

Hii Cartel ina watu jeuri Sana waliwahi kumgomea Kikwete kushusha bei kama mnakumbuka. Wanataja sababu zao za kupandisha bei lakini ukitazama nchi jirani ambazo zingine mafuta yanapitia kwetu unashindwa kabisa kuelewa.Ewura wanaitumikia serikali na wananchi au wanawatumikia hawa Oil cartel.

Kenya kwa kulazimisha big oil companies ziwe listed Stock exchange imewasaidia Sana transparency na kuwadhibiti..

Sisi niliona Magufuli alikuwa anajaribu TPDC wauze mafuta kwa kuwa na vituo kila mkoa lakini naona now hiyo policy nayo itakufa na sidhani kama ingesaidia sana.

Dawa ilikuwa kuwalazimisha kama Kenya wawe listed kwenye soko la hisa.

Na serikali inunue hisa kwa baadhi ya hizo kampuni kulazimisha transparency.

Otherwise naona Mama washamzidi na Ewura isharudi mifukoni mwa hawa wapigaji...
Wote Wanajenga UCHUMI wacha Wapige Pesa
 
Back
Top Bottom