Rais Samia ameshazidiwa na wapigaji suala la bei ya petroli?

Rais Samia ameshazidiwa na wapigaji suala la bei ya petroli?

Mkuu unanitafuta nini? Mimi dereva WA daladala bei ya mafuta inaniathiri sana nitafurahi nini sasa? Nifurahie njaa?!!
Nimecheka balaa eti dereva wa daladala. Ila wealthy people ndo mlivyo hampendi kujionesha onesha na misifa ya kijinga ingekuwa washika chenji kama kina kidukulio weeee
 
Ila CCM bana. Mwaka wa sita huu mishahara iko palepale ila kodi zinazidi kuongezeka wakati hao hao watumishi ndo wanapasuka kwa kuongezeka gharama za maisha. Unalipa income tax kubwa ukija mtaani mfanyabishara anampasua tena kwa bei za bidhaa. Ni kama unalipa kodi mara kumi kumi wangekuwa wanawafikiria watumishi wangeondoa kodi (income tax) kama mishahara wamegoma kuongeza
Hawa wapuuzi wanafikiri relief ya kupata pesa za kufanya ufisadi wao ni kuwakamua watumishi kwa namna yoyote ile, juzi kati wamewapiga watumishi kwenye salary slip ishu ya mikopo ya bodi......yaani ni mwendo wa kukatwa deni ambalo halipungui, wanachokitafuta watakipata tu.
 
Ulichoandika hapa Mkuu Boss ni sababu tosha ya kumkabili Maza na kupinga bajeti yake ambayo ina kodi kubwa sana kwa walipa kodi. Kama nchi zote zinanunua Petroli kutoka soko lile lile la iweje bei ya petroli nchini iwe kubwa sana kuliko nchi nyngine?
Unapingaje kitu ambacho kimeshapitishwa bungeni?


Wakati Mwiguli anasoma bajeti pale bungeni nyie mlikuwa busy kusaini petition ili Diamond atolewe kwenye tuzo za BET,!

Sikia! Wakati Mwigulu anasoma bajeti ya nchi uzi wake hapa ulikuwa na coments 90, uzi wa Sabaya ulikuwa na coments elfu 1 na ule wa kusaini petition ya kumtoa Mondi kwenye tuzo za BET ulikuwa na coments 800

Sisi ni [emoji205][emoji205][emoji205][emoji205]
 
Kuna sehemu moja ya kuuza supu na nyama za uchagani juzi nimemkuta pedejee Jack pemba nilipomuona tuu nikajua kama na yeye katoka marekani karudi basi nchi inarudi zama zile za mkwere.

Wapigaji wanarudi kama woteee. Mafuta mama hawezi kuchomoa wameshaupiga mwingi pamoja na zuga yetu ya Bulk procurement. Ila kwa ukweli Mama tumsaidie amalize ngwe yake hakuna maajabu atakayoyaleta isipokuwa utawala nusu wa sheria wa kutoka uamsho,kina ndama, mdude lakini wapo watumishi wa umma wameonewa na kuenguliwa sababu walikuwa karibu na mwendazake mama hajatia neno.
 
Ingekuwa vizuri awe na mtu kama CAG Assad ambaye anazijua namba kwa kina na athari zake kwa Taifa kwa namna moja au nyingine na pia atauliza maswali muafaka kabla hajamruhusu maza atie wino, vinginevyo itakula kwake.
Kuna mtu alisema humu, hawa ma-CAG wanatoa ripoti kulingana na ulaji wake na mamlaka iliyomteua.

Kinachofanyika kwa sasa ni kuruhusu kila mtu afanye kwa namna yake bila kuingiliana kwenye reli, kama awamu ya nne tu; usimshike mtu mkono.

Akili iliyotumika kuharibu, haiwezi kutengeneza.

Tumia akili
'thestate' inaongozwa na wa msoga?
 
Hovyo tu, alikuta mafuta shilingi elfu 1200 tu ikapaa mpaka 2200 kwa lita, saruji juu, mabati juu, mafuta ya kula juu

Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
Wewe ndio wa hovyo kabisa!

Magu alikuata mafuta yanauzwa kati ya 1900 hadi 2100 na alimaintain bei isivuke 2200 kwa muda wake wa miaka yote 5

Hiyo bei yako ya 1200 ni ya Mkapa!

Ni suala la muda tu tutaelewana tu
 
Ulichoandika hapa Mkuu Boss ni sababu tosha ya kumkabili Maza na kupinga bajeti yake ambayo ina kodi kubwa sana kwa walipa kodi. Kama nchi zote zinanunua Petroli kutoka soko lile lile la iweje bei ya petroli nchini iwe kubwa sana kuliko nchi nyngine?
Soon na wwe BAK utaanza kumuelewa Hayati Magufuli japokua is to late kwako!!
 
Bei ya Petroli kwa lita
Zambia 1800
Rwanda 1800
Kenya 2000
Tanzania 2400

Naona Mama keshaanza kuzidiwa mapema sana na wapigaji
Oil cartel hii imeshasambaza 'hela'za kutosha huko Ewura na kwingineko now
Wana panga bei wanavyotaka...

Hii Cartel ina watu jeuri Sana waliwahi kumgomea Kikwete kushusha bei kama mnakumbuka.
Wanataja sababu zao za kupandisha bei lakini ukitazama nchi jirani ambazo zingine mafuta yanapitia kwetu unashindwa kabisa kuelewa.Ewura wanaitumikia serikali na wananchi au wanawatumikia hawa Oil cartel..

Kenya kwa kulazimisha big oil companies ziwe listed Stock exchange imewasaidia Sana transparency na kuwadhibiti..

Sisi niliona Magufuli alikuwa anajaribu TPDC wauze mafuta kwa kuwa na vituo kila mkoa lakini naona now hiyo policy nayo itakufa na sidhani kama ingesaidia sana .
Dawa ilikuwa kuwalazimisha kama Kenya wawe listed kwenye soko la hisa.

Na serikali inunue hisa kwa baadhi ya hizo kampuni kulazimisha transparency.

Otherwise naona Mama washamzidi na Ewura isharudi mifukoni mwa hawa wapigaji...
Rais samia anahujumiwa kijanja sana ingawa yeye hajalijua hilo anawaamini kina mwigulu. Watu ambao nao wana uchu na urais kuliko kitu chochote
 
Back
Top Bottom