Hapa ukiangalia siyo cartel ya wauza mafuta bali ni utitiri mkubwa wa kodi katika bidhaa ya mafuta. Mfano, mwezi huu pekee, CIF ya petroli ni TZS 1,216 hivi. Baada ya hapo kuna kodi baada ya kodi hadi imefika TZS 2,405
lita kwa Dar es Salaam kwa petroli pekee. Na ukisoma ukurasa wa nane wa tangazo la EWURA utaona utitori wa kodi hizo. Utakuta hata faida kwa wauza mafuta wamewekewa,mfano petroli ni kama shs 128 kwa lita. Sasa ukichukua bei ya rejareja kwa DSM utoe na CIF na faida kwa whole sellers na retailers inayobakia ni kodi na tozo mbalimbali.
Miaka ya nyuma serikali ilikuwa na kawaida ya kila budget kupandisha ushuru kwenye vinywaji hasa vileo na soda, sasa imeanzisha huu utaratibu kwenye bidhaa za mafuta. Ndiyo maana utaona hata enzi za Magufuli, petroli haijaweza kuwa chini kuliko inavyokuwa nchi jirani ambazo zinapitisha mafuta hapa kwetu.
Shida kubwa ya watoza kodi wetu siyo kupanua wigo mkubwa wa walipa kodi ikiwa ile stamilivu, ni kutoza kodi kubwa kwenye bidhaa zile zile bila kujali kuwa anayeumia ni mlaji wa mwisho.