Rais Samia ameshinda, watanzania tumeshinda, Taifa limeshinda na tunamaliza mwaka kwa ushindi

Ndio Tunaitegemea Mvua za Mwenyezi MUNGU,Hata tupewe mashine za umwagiliaji lakini hatuwezi kuacha kujinyenyekeza mbele za Mwenyezi MUNGU ili Atupatie Neemaa ya Mvua inayoonyesha na kumwagilia kila eneo,Mvua Ni bAraka na ni Neema na Tutaendelea kuomba Neema hiyo kuwepo kwa wakati nchini kwetu ili hata misitu yetu iwe ya kijani na kupendeza vizuri,
Misitu unayozungumzia tunaifyeka wenyewe kwa ujinga wetu; halafu tunajinynykeza kwa Mungu atuletee mvua?!
 
Ndugu Zangu,

Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema kuwa kwa hakika Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Ameshinda katika mapambano ya kulijenga Taifa letu na kuwaongoza watanzania katika ujenzi wa Taifa letu kwa mikono yetu wenyewe na Taifa letu limeshinda kwa kubaki likiwa Imara na Tulivu.

Rais Samia na serikali yake ameipigana kwa uhodari,ujasiri na ushupavu mkubwa Sana Vita ya kuliletea Maendeleo Taifa letu,Amekuwa Ni Askari mzalendo na mvumilivu katika mapambano haya ya kulipa heshima Taifa letu kiuchumi,Amekuwa mstari wa mbele katika kujenga uchumi shirikishi unamgusa na kumnufaisha kila mmoja wetu pasipo kumwacha mtanzania yeyote nyuma.

Rais Samia Na serikali yake ameweka Alama katika kila Secta utakayo kwenda unakuta kazi kubwa imefanyika,unakuta Rais Samia ameirejesha Kodi na Tozo za mtanzania zikafanye kazi za kugusa maisha ya watanzania,kwa kutatua kero na changamoto zinazokuwa zinawakwamisha watanzania katika maisha yao ya kila siku pamoja na kujenga miradi mbalimbali inayomnufaisha mtanzania,

Rais Samia amemshika mkono kila mtanzania aliyehitaji kushikwa mkono na serikali yake,Rais Samia amezibeba secta zote na kuzipa umuhimu wa kipekee kwa kutambua kuwa watanzania wapo kila secta na hivyo kupuuza secta yoyote ni sawa na kuwapuuza watanzania na hivyo kuwadidimiza na kuwadhoofisha kiuchumi watanzania.

Kila mtanzania amefikiwa na kuguswa na juhudi za mh Rais,kila eneo limeguswa na kubebwa katika mikono na mabega ya mh Rais,kila sehemu kumefikiwa na kutazamwa na jicho la mh Rais ,kila mahali kumepitiwa na kupewa ufumbuzi,kila Kona ni matumaini kwa kesho iliyo Bora Zaidi ya leo.

Watanzania wamesikilizwa na kusaidiwa mahali walipo na wanapofanyia kazi na kuishi, watanzania wamepewa sikio la Rais kuwasikiliza na kuwapa majibu, Rais Samia Amezunguka Kanda zote na kutoa majibu kwa changamoto zinazotukabili,ametoa usuluhishi kwa migogoro, Amatufikisha hapa kwa Amani na utulivu.

Watanzania Tumeshinda kwa kufika hapa tukiwa wamoja na wenye ushirikiano,Tumeungana na serikali yetu na kusimama nayo katika nyakati zote,Tumempa ushirikiano na kumuunga mkono Rais wetu wakati wote alipotuhitaji kufanya Hivyo,Umoja wa kitaifa umekuwa mkubwa na wenye Afya kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Taifa letu,Hatujatoa Nafasi kwa Adui yeyote aliyejaribu kutugawa na kutuchonganisha, Tumekuwa wavumilivu katika changamoto zote tulizozipitia Kama Taifa kwa kutambua na kuona juhudi kubwa zilizofanywa na Rais wetu mpendwa pamoja na serikali yake,

Ni matumaini yangu kuwa umoja huu tulioujenga Sasa tutaingia nao mwaka mpya na Kuendelea na kazi ya kulijenga Taifa letu litakalokuwa Bora Zaid ya hapa tulipo hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Tumejaliwa na Mwenyezi MUNGU kuwa na Rasilimali nyingi ambazo zinatutaka kutumia akili na maarifa katika kuzitumia ili zisibadilike na kuwa Kama laana kwetu kwa kutuacha tukiwa maskini na fukara katikati ya utajiri wa Asili.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
Umeshinda nini???Vita!Magonjwa!Njaa!Ujinga! au neema.
 
Kama tafsiri ya uzalendo ni kuwa na akili za kipu.mbavu kama za huyu Lucas Mwashambwa basi uzalendo utafutiwe tafsiri mpya!

Uzuri hata anaowasifia wanajua kuwa sifa na uwezo wanaopewa na huyu Chawa hawana bali Chawa huyu anasukumwa na njaa tu!

Kama siyo njaa, anaweka namba za simu za nini?
Labda wehu unamsumbua.
 
Ndugu yangu tunasema kwa uhakika kwa sasa nipo mikoani, na watu waliandikiaha mahitaji yao ila hakuna kinachofofanyika nimepita mikoa 3 Hali ni hiyo hiyo Na kuna mkoa mmoja watu wanaokolewa na mbolea za tumbaku, tembea ndio uje kuchora humu na ushaidi upo wa kutosha ktk mikao hiyo 3.
Upo sawa mkuu.
Halafu mbaya zaidi mbolea za kufuata mjini yaani upande basi ndio ukachukue mbolea.
 
Anashindana na kupigana Vita dhidi ya maadui wa Ujinga ,Maradhi na Umaskini katika kuhakikisha maadui hao wanapotezwa na kusambaratishaa pasipo kuwaacha na uwezo wa kusimama
Kama anashindana na ujinga, maradhi na umaskini, mbona bado hajashinda
 
Upo sawa mkuu.
Halafu mbaya zaidi mbolea za kufuata mjini yaani upande basi ndio ukachukue mbolea.
Inauma sana ndugu yangu umepanda kitaalam unaambiwa baada ya siku 21 mpaka 30 uweke mbolea na watu wanakuja kukwambia mbolea ipo njiani inakuja kuwa mvumilivu utafikiri na siku zinasimama. Ki ukweli kuna siku tutatiana risasi hadharani.
 
Asante kwa mchango wako katika adhima nzima ya ujenzi wa Taifa letu,Pila napenda kukwambia kuwa huwezi unashindwa au kuogopa kufanya biashara fulani kwa kuwa tu Kuna mtu anafanya biashara hiyo,hapa utakuwa unafeli kabla ya kuanza biashara husika,maana biashara Ni ushawishi na mahusiano mazuri na wateja wako pamoja na ubora wa huduma inayotolewa ukilinganisha na mwenzio,Hatujengi reli yetu kwa kutegemea mizigo ya majirani pekee lakini tunategemea kuwa kwa malengo yetu ni kuhakikisha kuwa reli yetu inahudumia na mizigonya nchi jirani katika namna na ubora wa huduma ambao utafanya mfanyabiashara yeyote asijute kufanya biashara ya usafirishaji kupitia bandari yetu pamoja na Miundombinu yetu ya reli, Biashara Ni ushindani na tunaamini serikali yetu inalitambua Hilo ndio maana imekuwa na mikakati ya kuboresha huduma za usafiri kwa kupunguza vikwazo na changamoto ndogo ndogo.

Katika suala la uzalishaji kwa ajili ya ku safirisha nje ya nchi Napo serikali yetu inafanya vyema tu,ndio maana katika wizara ya kilimo Tumeona ongezeko la bajeti kutoka billioni Mia mbili na point Hadi kufikia billioni Mia Tisa na point,Hali itakayochochea uzalishaji lakini pia kuchochea maendeleo ya viwanda ambayo kilimo ndio injini yake katika kutoa malighafi, lakini pia serikali imejitahidi kuvutia wawekezaji kuwekeza katika secta hii ya kilimo iliyo tegemezi kwa watanzania ,Kama vile ujenzi wa viwanda cya mbolea ili kusaidia upatikanaji wa mbolea kwa Bei nafuu.

Samahani kwa kukwambia hili, UNAAMINI KWENUE THEORY SANA NA MAKARATASI, UHALISIA KWENYE GROUND HAUKO HIVYO..

Wanasiasa wa Africa na Tanzania ni wazuri sana kwa uongo wa majukwaani na kwenye makaratasi wakitafuta umaarufu wa kisiasa lakini ukirudi kwenye uhalisia mambo ni tofauti kabisa.

Unaujua uhalisia wa hali ya wakulima wa Tanzania huko mapolini vz hiyo 900bil budget, Unajua kwamba volume kubwa ya exportation ndiyo inaleta foreigner currency hasa dollar kwa wingi? hiyo volume iko wapi? na hizo dollar ziko wapi?.... Exportation inaonekana kwenye bandari zetu na mipaka yetu, meli nyingi zinakuja kuleta bidhaa na kuondoka tupu(huu ni uhalisia)... mpaka pekee uliobusy kwa exportation ya mazao ya kilimo ni Namanga, Horiri na Hororo kwenda Kenya, Pale tunduma kikubwa ni mizigo ya transit...kwingine kote ni dolo....

Msimu wa korosho miaka yooote pale Mtwara meli huja kubeba, hebu niambie msimu huu kipi kimeongezeka...tumezarisha korosha kiasi gani na kuexport kiasi gani?
Niambia volume ya mazao mengine ya kilimo yanayoreflect ongezeko la production na impact ya 900bil...

Unaweza kuinject 900bil kwenye kilipo zikaishia kwenye matumbo ya watu au zikawa kwenye makaratasi, tunapaswa kuona impact yake mtaani..

Unaweza kusema umeinject 3trilion kwenye uchumi lakini ikawa kwenye makaratasi, JE impact yake kitaa ipoje?....

TUNAPIMA IMPACT NA SIO MANENO, hata hii mikopo tunapima IMPACT SIO MANENO YA KWENYE MAKARATASI NA MAJUKWAA YA SIASA.
 
Inauma sana ndugu yangu umepanda kitaalam unaambiwa baada ya siku 21 mpaka 30 uweke mbolea na watu wanakuja kukwambia mbolea ipo njiani inakuja kuwa mvumilivu utafikiri na siku zinasimama. Ki ukweli kuna siku tutatiana risasi hadharani.
Inawezekana huko uliko kukawa na changamoto ndogo ndogo ya kuchelewa kufika kwa mbolea Jambo ambalo siyo kosa la serikali maana yenyewe inakuwa na tayari ilishatia pesa Kama ambavyo tulitangaziwa hadharani na serikali yetu ,masuala ya usafirishaji wa mizigo na kuitoa iliko huwa kuna jitokeza changamoto za hapa na pale,Hivyo kuwa mvumilivu na acha hasira za sijuwi kusema utampiga mtu risasi. Watanzania hatupo hivyo na Wala hatuna Roho za namna hiyo.

Kikubwa tunaishukuru serikali yetu kwa kutoa mbolea za Ruzuku hali iliyomsaidia mkulima kupata mbolea kwa Bei nafuu ukilinganisha na msimu uliopita
 
Samahani kwa kukwambia hili, UNAAMINI KWENUE THEORY SANA NA MAKARATASI, UHALISIA KWENYE GROUND HAUKO HIVYO..

Wanasiasa wa Africa na Tanzania ni wazuri sana kwa uongo wa majukwaani na kwenye makaratasi wakitafuta umaarufu wa kisiasa lakini ukirudi kwenye uhalisia mambo ni tofauti kabisa.

Unaujua uhalisia wa hali ya wakulima wa Tanzania huko mapolini vz hiyo 900bil budget, Unajua kwamba volume kubwa ya exportation ndiyo inaleta foreigner currency hasa dollar kwa wingi? hiyo volume iko wapi? na hizo dollar ziko wapi?.... Exportation inaonekana kwenye bandari zetu na mipaka yetu, meli nyingi zinakuja kuleta bidhaa na kuondoka tupu(huu ni uhalisia)... mpaka pekee uliobusy kwa exportation ya mazao ya kilimo ni Namanga, Horiri na Hororo kwenda Kenya, Pale tunduma kikubwa ni mizigo ya transit...kwingine kote ni dolo....

Msimu wa korosho miaka yooote pale Mtwara meli huja kubeba, hebu niambie msimu huu kipi kimeongezeka...tumezarisha korosha kiasi gani na kuexport kiasi gani?
Niambia volume ya mazao mengine ya kilimo yanayoreflect ongezeko la production na impact ya 900bil...

Unaweza kuinject 900bil kwenye kilipo zikaishia kwenye matumbo ya watu au zikawa kwenye makaratasi, tunapaswa kuona impact yake mtaani..

Unaweza kusema umeinject 3trilion kwenye uchumi lakini ikawa kwenye makaratasi, JE impact yake kitaa ipoje?....

TUNAPIMA IMPACT NA SIO MANENO, hata hii mikopo tunapima IMPACT SIO MANENO YA KWENYE MAKARATASI NA MAJUKWAA YA SIASA.
Mkuu,unajitesa bure kumwelimisha huyu bwana mdogo.
 
Misitu unayozungumzia tunaifyeka wenyewe kwa ujinga wetu; halafu tunajinynykeza kwa Mungu atuletee mvua?!
Tunatakiwa sisi wenyewe Tuwe Walinzi wa misitu yetu shidi ya wachache watakao kuharibu misitu yetu, tupeana Elimu na kuelimishana juu ya umuhimu na faida ya uwepo wa misitu,Tusiharibu mazingira yetu Bali tuyatunze ili yatutunze watanzania
 
Ndugu Zangu,

Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema kuwa kwa hakika Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Ameshinda katika mapambano ya kulijenga Taifa letu na kuwaongoza watanzania katika ujenzi wa Taifa letu kwa mikono yetu wenyewe na Taifa letu limeshinda kwa kubaki likiwa Imara na Tulivu.

Rais Samia na serikali yake ameipigana kwa uhodari,ujasiri na ushupavu mkubwa Sana Vita ya kuliletea Maendeleo Taifa letu,Amekuwa Ni Askari mzalendo na mvumilivu katika mapambano haya ya kulipa heshima Taifa letu kiuchumi,Amekuwa mstari wa mbele katika kujenga uchumi shirikishi unamgusa na kumnufaisha kila mmoja wetu pasipo kumwacha mtanzania yeyote nyuma.

Rais Samia Na serikali yake ameweka Alama katika kila Secta utakayo kwenda unakuta kazi kubwa imefanyika,unakuta Rais Samia ameirejesha Kodi na Tozo za mtanzania zikafanye kazi za kugusa maisha ya watanzania,kwa kutatua kero na changamoto zinazokuwa zinawakwamisha watanzania katika maisha yao ya kila siku pamoja na kujenga miradi mbalimbali inayomnufaisha mtanzania,

Rais Samia amemshika mkono kila mtanzania aliyehitaji kushikwa mkono na serikali yake,Rais Samia amezibeba secta zote na kuzipa umuhimu wa kipekee kwa kutambua kuwa watanzania wapo kila secta na hivyo kupuuza secta yoyote ni sawa na kuwapuuza watanzania na hivyo kuwadidimiza na kuwadhoofisha kiuchumi watanzania.

Kila mtanzania amefikiwa na kuguswa na juhudi za mh Rais,kila eneo limeguswa na kubebwa katika mikono na mabega ya mh Rais,kila sehemu kumefikiwa na kutazamwa na jicho la mh Rais ,kila mahali kumepitiwa na kupewa ufumbuzi,kila Kona ni matumaini kwa kesho iliyo Bora Zaidi ya leo.

Watanzania wamesikilizwa na kusaidiwa mahali walipo na wanapofanyia kazi na kuishi, watanzania wamepewa sikio la Rais kuwasikiliza na kuwapa majibu, Rais Samia Amezunguka Kanda zote na kutoa majibu kwa changamoto zinazotukabili,ametoa usuluhishi kwa migogoro, Amatufikisha hapa kwa Amani na utulivu.

Watanzania Tumeshinda kwa kufika hapa tukiwa wamoja na wenye ushirikiano,Tumeungana na serikali yetu na kusimama nayo katika nyakati zote,Tumempa ushirikiano na kumuunga mkono Rais wetu wakati wote alipotuhitaji kufanya Hivyo,Umoja wa kitaifa umekuwa mkubwa na wenye Afya kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Taifa letu,Hatujatoa Nafasi kwa Adui yeyote aliyejaribu kutugawa na kutuchonganisha, Tumekuwa wavumilivu katika changamoto zote tulizozipitia Kama Taifa kwa kutambua na kuona juhudi kubwa zilizofanywa na Rais wetu mpendwa pamoja na serikali yake,

Ni matumaini yangu kuwa umoja huu tulioujenga Sasa tutaingia nao mwaka mpya na Kuendelea na kazi ya kulijenga Taifa letu litakalokuwa Bora Zaid ya hapa tulipo hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Tumejaliwa na Mwenyezi MUNGU kuwa na Rasilimali nyingi ambazo zinatutaka kutumia akili na maarifa katika kuzitumia ili zisibadilike na kuwa Kama laana kwetu kwa kutuacha tukiwa maskini na fukara katikati ya utajiri wa Asili.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
We boya hupumziki
 
Umeshinda nini???Vita!Magonjwa!Njaa!Ujinga! au neema.
Tumeshinda Vita ya mapambano yetu dhidi ya maadui zetu kwa kuwa tumewaelemea maadui zetu na kuwaweka katika udhibiti,Ndio maana unaona shule zikiwa zimeenea kila mahali huku Elimu ikiwa Ni bure Mpaka kidato Cha sita huku mikopo ya Elimu ya juu ikitolewa kwa wanafunzi karibu wote waliokidhi vigezo,Hii yote Ni katika kumshambulia Adui ujinga.

Lakini pia ujenzi wa zahanati ,vituo vya Afya, hospitali za wilaya na uboreshaji wa hospitali za rufaa ,Kanda Hadi Taifa zikiwa zinaendelea kuboresha ,lakini pia upatikanaji wa vifaa Tiba,madawa na uwepo wa wahudumu wa Afya Ni wa kuridhisha Sana,Hii yote Ni katika kusogeza huduma hii muhimu ili kuweza kuhakikisha watanzania wanakuwa wenye Afya na kupata huduma Bora za kiafya kusudi wawezi kushiriki vyema katika suala Zima la uzalishaji na ujenzi wa Taifa letu kiuchumi,

Umaskini nao unapigwa kimkakati kwa kuwekeza katika miradi ya kimkakati inayogusa maisha ya mtanzania,fedha nyingi zunawekezwa katika secta muhimu na zinazobeba watanzania wengi,mfano kilimo ambako watanzania wengi wamejiajiri unakuta serikali imewekeza mabillioni ya pesa ili kumkwamua kiuchumi mwananchi.

Serikali imefanya kazi kubwa Sana katika kupigana Vita ya kuwatokomeza maadui hao watatu
 
Inawezekana huko uliko kukawa na changamoto ndogo ndogo ya kuchelewa kufika kwa mbolea Jambo ambalo siyo kosa la serikali maana yenyewe inakuwa na tayari ilishatia pesa Kama ambavyo tulitangaziwa hadharani na serikali yetu ,masuala ya usafirishaji wa mizigo na kuitoa iliko huwa kuna jitokeza changamoto za hapa na pale,Hivyo kuwa mvumilivu na acha hasira za sijuwi kusema utampiga mtu risasi. Watanzania hatupo hivyo na Wala hatuna Roho za namna hiyo.

Kikubwa tunaishukuru serikali yetu kwa kutoa mbolea za Ruzuku hali iliyomsaidia mkulima kupata mbolea kwa Bei nafuu ukilinganisha na msimu uliopita
Kwani ilipandishwa bei na nani mpaka tuanze kuishukuru sirikali?
 
Ilipanda katika soko la Dunia,Baada ya hapa serikali yetu kwa kuwajali wakulima ikatoa Billion Mia moja hamsini Kama Ruzuku kwenye mbolea ili ishuke Bei ,Na kweli msimu huu mbolea imeshuka Bei ,mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu
 
Back
Top Bottom