Rais Samia ameshinda, watanzania tumeshinda, Taifa limeshinda na tunamaliza mwaka kwa ushindi

Misitu unayozungumzia tunaifyeka wenyewe kwa ujinga wetu; halafu tunajinynykeza kwa Mungu atuletee mvua?!
 
Umeshinda nini???Vita!Magonjwa!Njaa!Ujinga! au neema.
 
Labda wehu unamsumbua.
 
Upo sawa mkuu.
Halafu mbaya zaidi mbolea za kufuata mjini yaani upande basi ndio ukachukue mbolea.
 
Anashindana na kupigana Vita dhidi ya maadui wa Ujinga ,Maradhi na Umaskini katika kuhakikisha maadui hao wanapotezwa na kusambaratishaa pasipo kuwaacha na uwezo wa kusimama
Kama anashindana na ujinga, maradhi na umaskini, mbona bado hajashinda
 
Upo sawa mkuu.
Halafu mbaya zaidi mbolea za kufuata mjini yaani upande basi ndio ukachukue mbolea.
Inauma sana ndugu yangu umepanda kitaalam unaambiwa baada ya siku 21 mpaka 30 uweke mbolea na watu wanakuja kukwambia mbolea ipo njiani inakuja kuwa mvumilivu utafikiri na siku zinasimama. Ki ukweli kuna siku tutatiana risasi hadharani.
 

Samahani kwa kukwambia hili, UNAAMINI KWENUE THEORY SANA NA MAKARATASI, UHALISIA KWENYE GROUND HAUKO HIVYO..

Wanasiasa wa Africa na Tanzania ni wazuri sana kwa uongo wa majukwaani na kwenye makaratasi wakitafuta umaarufu wa kisiasa lakini ukirudi kwenye uhalisia mambo ni tofauti kabisa.

Unaujua uhalisia wa hali ya wakulima wa Tanzania huko mapolini vz hiyo 900bil budget, Unajua kwamba volume kubwa ya exportation ndiyo inaleta foreigner currency hasa dollar kwa wingi? hiyo volume iko wapi? na hizo dollar ziko wapi?.... Exportation inaonekana kwenye bandari zetu na mipaka yetu, meli nyingi zinakuja kuleta bidhaa na kuondoka tupu(huu ni uhalisia)... mpaka pekee uliobusy kwa exportation ya mazao ya kilimo ni Namanga, Horiri na Hororo kwenda Kenya, Pale tunduma kikubwa ni mizigo ya transit...kwingine kote ni dolo....

Msimu wa korosho miaka yooote pale Mtwara meli huja kubeba, hebu niambie msimu huu kipi kimeongezeka...tumezarisha korosha kiasi gani na kuexport kiasi gani?
Niambia volume ya mazao mengine ya kilimo yanayoreflect ongezeko la production na impact ya 900bil...

Unaweza kuinject 900bil kwenye kilipo zikaishia kwenye matumbo ya watu au zikawa kwenye makaratasi, tunapaswa kuona impact yake mtaani..

Unaweza kusema umeinject 3trilion kwenye uchumi lakini ikawa kwenye makaratasi, JE impact yake kitaa ipoje?....

TUNAPIMA IMPACT NA SIO MANENO, hata hii mikopo tunapima IMPACT SIO MANENO YA KWENYE MAKARATASI NA MAJUKWAA YA SIASA.
 
Inauma sana ndugu yangu umepanda kitaalam unaambiwa baada ya siku 21 mpaka 30 uweke mbolea na watu wanakuja kukwambia mbolea ipo njiani inakuja kuwa mvumilivu utafikiri na siku zinasimama. Ki ukweli kuna siku tutatiana risasi hadharani.
Inawezekana huko uliko kukawa na changamoto ndogo ndogo ya kuchelewa kufika kwa mbolea Jambo ambalo siyo kosa la serikali maana yenyewe inakuwa na tayari ilishatia pesa Kama ambavyo tulitangaziwa hadharani na serikali yetu ,masuala ya usafirishaji wa mizigo na kuitoa iliko huwa kuna jitokeza changamoto za hapa na pale,Hivyo kuwa mvumilivu na acha hasira za sijuwi kusema utampiga mtu risasi. Watanzania hatupo hivyo na Wala hatuna Roho za namna hiyo.

Kikubwa tunaishukuru serikali yetu kwa kutoa mbolea za Ruzuku hali iliyomsaidia mkulima kupata mbolea kwa Bei nafuu ukilinganisha na msimu uliopita
 
Mkuu,unajitesa bure kumwelimisha huyu bwana mdogo.
 
Misitu unayozungumzia tunaifyeka wenyewe kwa ujinga wetu; halafu tunajinynykeza kwa Mungu atuletee mvua?!
Tunatakiwa sisi wenyewe Tuwe Walinzi wa misitu yetu shidi ya wachache watakao kuharibu misitu yetu, tupeana Elimu na kuelimishana juu ya umuhimu na faida ya uwepo wa misitu,Tusiharibu mazingira yetu Bali tuyatunze ili yatutunze watanzania
 
We boya hupumziki
 
Umeshinda nini???Vita!Magonjwa!Njaa!Ujinga! au neema.
Tumeshinda Vita ya mapambano yetu dhidi ya maadui zetu kwa kuwa tumewaelemea maadui zetu na kuwaweka katika udhibiti,Ndio maana unaona shule zikiwa zimeenea kila mahali huku Elimu ikiwa Ni bure Mpaka kidato Cha sita huku mikopo ya Elimu ya juu ikitolewa kwa wanafunzi karibu wote waliokidhi vigezo,Hii yote Ni katika kumshambulia Adui ujinga.

Lakini pia ujenzi wa zahanati ,vituo vya Afya, hospitali za wilaya na uboreshaji wa hospitali za rufaa ,Kanda Hadi Taifa zikiwa zinaendelea kuboresha ,lakini pia upatikanaji wa vifaa Tiba,madawa na uwepo wa wahudumu wa Afya Ni wa kuridhisha Sana,Hii yote Ni katika kusogeza huduma hii muhimu ili kuweza kuhakikisha watanzania wanakuwa wenye Afya na kupata huduma Bora za kiafya kusudi wawezi kushiriki vyema katika suala Zima la uzalishaji na ujenzi wa Taifa letu kiuchumi,

Umaskini nao unapigwa kimkakati kwa kuwekeza katika miradi ya kimkakati inayogusa maisha ya mtanzania,fedha nyingi zunawekezwa katika secta muhimu na zinazobeba watanzania wengi,mfano kilimo ambako watanzania wengi wamejiajiri unakuta serikali imewekeza mabillioni ya pesa ili kumkwamua kiuchumi mwananchi.

Serikali imefanya kazi kubwa Sana katika kupigana Vita ya kuwatokomeza maadui hao watatu
 
Kwani ilipandishwa bei na nani mpaka tuanze kuishukuru sirikali?
 
Kwani ilipandishwa bei na nani mpaka tuanze kuishukuru sirikali?
Ilipanda katika soko la Dunia,Baada ya hapa serikali yetu kwa kuwajali wakulima ikatoa Billion Mia moja hamsini Kama Ruzuku kwenye mbolea ili ishuke Bei ,Na kweli msimu huu mbolea imeshuka Bei ,mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…