Rais Samia ameshinda, watanzania tumeshinda, Taifa limeshinda na tunamaliza mwaka kwa ushindi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu Zangu,

Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema kuwa kwa hakika Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Ameshinda katika mapambano ya kulijenga Taifa letu na kuwaongoza watanzania katika ujenzi wa Taifa letu kwa mikono yetu wenyewe na Taifa letu limeshinda kwa kubaki likiwa Imara na Tulivu.

Rais Samia na serikali yake ameipigana kwa uhodari,ujasiri na ushupavu mkubwa Sana Vita ya kuliletea Maendeleo Taifa letu,Amekuwa Ni Askari mzalendo na mvumilivu katika mapambano haya ya kulipa heshima Taifa letu kiuchumi,Amekuwa mstari wa mbele katika kujenga uchumi shirikishi unamgusa na kumnufaisha kila mmoja wetu pasipo kumwacha mtanzania yeyote nyuma.

Rais Samia Na serikali yake ameweka Alama katika kila Secta utakayo kwenda unakuta kazi kubwa imefanyika,unakuta Rais Samia ameirejesha Kodi na Tozo za mtanzania zikafanye kazi za kugusa maisha ya watanzania,kwa kutatua kero na changamoto zinazokuwa zinawakwamisha watanzania katika maisha yao ya kila siku pamoja na kujenga miradi mbalimbali inayomnufaisha mtanzania,

Rais Samia amemshika mkono kila mtanzania aliyehitaji kushikwa mkono na serikali yake,Rais Samia amezibeba secta zote na kuzipa umuhimu wa kipekee kwa kutambua kuwa watanzania wapo kila secta na hivyo kupuuza secta yoyote ni sawa na kuwapuuza watanzania na hivyo kuwadidimiza na kuwadhoofisha kiuchumi watanzania.

Kila mtanzania amefikiwa na kuguswa na juhudi za mh Rais,kila eneo limeguswa na kubebwa katika mikono na mabega ya mh Rais,kila sehemu kumefikiwa na kutazamwa na jicho la mh Rais ,kila mahali kumepitiwa na kupewa ufumbuzi,kila Kona ni matumaini kwa kesho iliyo Bora Zaidi ya leo.

Watanzania wamesikilizwa na kusaidiwa mahali walipo na wanapofanyia kazi na kuishi, watanzania wamepewa sikio la Rais kuwasikiliza na kuwapa majibu, Rais Samia Amezunguka Kanda zote na kutoa majibu kwa changamoto zinazotukabili,ametoa usuluhishi kwa migogoro, Amatufikisha hapa kwa Amani na utulivu.

Watanzania Tumeshinda kwa kufika hapa tukiwa wamoja na wenye ushirikiano,Tumeungana na serikali yetu na kusimama nayo katika nyakati zote,Tumempa ushirikiano na kumuunga mkono Rais wetu wakati wote alipotuhitaji kufanya Hivyo,Umoja wa kitaifa umekuwa mkubwa na wenye Afya kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Taifa letu,Hatujatoa Nafasi kwa Adui yeyote aliyejaribu kutugawa na kutuchonganisha, Tumekuwa wavumilivu katika changamoto zote tulizozipitia Kama Taifa kwa kutambua na kuona juhudi kubwa zilizofanywa na Rais wetu mpendwa pamoja na serikali yake,

Ni matumaini yangu kuwa umoja huu tulioujenga Sasa tutaingia nao mwaka mpya na Kuendelea na kazi ya kulijenga Taifa letu litakalokuwa Bora Zaid ya hapa tulipo hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Tumejaliwa na Mwenyezi MUNGU kuwa na Rasilimali nyingi ambazo zinatutaka kutumia akili na maarifa katika kuzitumia ili zisibadilike na kuwa Kama laana kwetu kwa kutuacha tukiwa maskini na fukara katikati ya utajiri wa Asili.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
 
Nadhani mikoani Na katika vijiji utajionea shida ya mbolea ni aibu kusema wameshida wakati MTU amelima ekari kumi za mahindi anapatia mbolea,mifuko 6 ya mbolea
Wakati tunajiandikisha kwa ajili ya maombi ya mbolea za Ruzuku Kuna kipengele kulikuwa kinaumiza unalima heka ngapi? Kwa hiyo haoi kila mmoja alikuwa anajibu kulingana na maandalizi yake na uwezo wake kiuchumi. Kwa hiyo huyo unayesmea sijuwi kapewa miuko sita ungemuuliza aliandika heka ngapi?
 
Ndugu yangu tunasema kwa uhakika kwa sasa nipo mikoani, na watu waliandikiaha mahitaji yao ila hakuna kinachofofanyika nimepita mikoa 3 Hali ni hiyo hiyo Na kuna mkoa mmoja watu wanaokolewa na mbolea za tumbaku, tembea ndio uje kuchora humu na ushaidi upo wa kutosha ktk mikao hiyo 3.
 
FB_IMG_16722346111999614.jpg
 
Kama tafsiri ya uzalendo ni kuwa na akili za kipu.mbavu kama za huyu Lucas Mwashambwa basi uzalendo utafutiwe tafsiri mpya!

Uzuri hata anaowasifia wanajua kuwa sifa na uwezo wanaopewa na huyu Chawa hawana bali Chawa huyu anasukumwa na njaa tu!

Kama siyo njaa, anaweka namba za simu za nini?
 
Hivi huyu "mbuzi" anajua chini ya Serikali hii TRC chini ya kina Kadogosa wameokota Mabehewa huko ughaibuni na kuyapaka rangi na kutupiga zaidi ya bilioni 2.5 kwa kila behewa?!

Hivi huyu " mbuzi" anajua kama sasa Wakulima wa Alizeti na wenye viwanda vya kuzalisha mafuta ya kula vya ndani wanalia na kusaga meno baada ya kodi fulani kuondolewa kwenye imported " crude oil" na walamba asali sasa wamejificha wana import refined oil wakidanganya ni crude oil na kuuza kwa bei ya chini?!

Hivi huyu " mbuzi" anajua kuwa Serikali kwa sasa haina mkakati wowote wa uzalishaji na badala yake ni mikakati ya kukopa fedha nje na kubuni tozo tu!

Hivi huyu " mbuzi" kweli anajua tafsiri ya maneno " "kuna vijimaneno kuwa mwezi huu Serikalini hela hakuna, ni kweli hela hakuna kwa sababu mikopo imechelewa kufika "?!

"Mbuzi" kama huyu, Je anajua kwa muda mfupi kasi ya wizi na utoroshaji wa Madini Tanzania imeongezeka maradufu?!

Je, " mbuzi" kama huyu anayedai analima anajua kama Kenya ni miongoni mwa Exporters wakubwa Duniani wa Parachichi (Avocado), wakati sisi tuna maeneo mazuri na wakulima wazuri huko Njombe lakini Serikali imeshindwa kuweka Mazingira wezeshi kama miundombinu bora ya Usafirishaji na uhifadhi zao hilo?!
Je, "Mbuzi" huyu anajua kama wawekezaji wakubwa na matajiri kutoka nje wa Avocado wako Kenya badala ya Tanzania sababu ya ujinga wetu na hasa watu wenye akili za "mbuzi" kama huyu Lucas Mwashambwa ?!

" Mbuzi " kama hawa ndo wanafanya Watanzania tunadharaulika na Mataifa jirani kwamba hatuna smart brains!
 
Mimi mkoa niliko kila mtu anapewa mbolea ilimradi tu Anayo sms aliyorushiwa mwenye simu ambayo ilikuwa ndio Nambari unayokwenda nayo kwa wakala wa mbolea za Ruzuku
 
Kama tafsiri ya uzalendo ni kuwa na akili za kipu.mbavu kama za huyu Lucas Mwashambwa basi uzalendo utafutiwe tafsiri mpya!

Uzuri hata anaowasifia wanajua kuwa sifa na uwezo wanaopewa na huyu Chawa hawana bali Chawa huyu anasukumwa na njaa tu!

Kama siyo njaa, anaweka namba za simu za nini?
Mimi Ni mkulima hivyo suala la njaa Ni Vita nayo ipigana kwa kujishughulisha na kilimo
 
Hivi huyu "mbuzi" anajua chini ya Serikali hii TRC chini ya kina Kadogosa wameokota Mabehewa huko ughaibuni na kuyapaka rangi na kutupiga zaidi ya bilioni 2.5 kwa kila behewa?!

Hivi huyu " mbuzi" anajua kama sasa Wakulima wa Alizeti na wenye viwanda vya kuzalisha mafuta ya kula vya ndani wanalia na kusaga meno baada ya kodi fulani kuondolewa kwenye imported " crude oil" na walamba asali sasa wamejificha wana import refined oil wakidanganya ni crude oil na kuuza kwa bei ya chini?!

Hivi huyu " mbuzi" anajua kuwa Serikali kwa sasa haina mkakati wowote wa uzalishaji na badala yake ni mikakati ya kukopa fedha nje na kubuni tozo tu!

Hivi huyu " mbuzi" kweli anajua tafsiri ya maneno " "kuna vijimaneno kuwa mwezi huu Serikalini hela hakuna, ni kweli hela hakuna kwa sababu mikopo imechelewa kufika "?!

"Mbuzi" kama huyu, Je anajua kwa muda mfupi kasi ya wizi na utoroshaji wa Madini Tanzania imeongezeka maradufu?!

Je, " mbuzi" kama huyu anayedai analima anajua kama Kenya ni miongoni mwa Exporters wakubwa Duniani wa Parachichi (Avocado), wakati sisi tuna maeneo mazuri na wakulima wazuri huko Njombe lakini Serikali imeshindwa kuweka Mazingira wezeshi kama miundombinu bora ya Usafirishaji na uhifadhi zao hilo?!
Je, "Mbuzi" huyu anajua kama wawekezaji wakubwa na matajiri kutoka nje wa Avocado wako Kenya badala ya Tanzania sababu ya ujinga wetu na hasa watu wenye akili za "mbuzi" kama huyu Lucas Mwashambwa ?!

" Mbuzi " kama hawa ndo wanafanya Watanzania tunadharaulika na Mataifa jirani kwamba hatuna smart brains!
Chini ya uongozi shupavu na imara wa mama Samia watanzania Tumeona namna mazingira ya kiuwekezaji yalivyoboreshwa na kuwa kivutio na chaguo Nambari moja Cha wawekezaji na wafanyabiashara wakubwa hapa nchini,

Pia usiwe unaandika pasipo kuwa na ushahidi wa kinyaraka,unaposena wamekata na kuokota mabehewa ungetwambia na kutuwekea ushahidi wako wa mahali ambako katika Dunia hii wanamwaga mabehewa na wengine wanakwenda kuokota Kama vichaa majalalani
 
Ndugu Zangu,

Hivyo Ndivyo unavyoweza kusema kuwa kwa hakika Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan Ameshinda katika mapambano ya kulijenga Taifa letu na kuwaongoza watanzania katika ujenzi wa Taifa letu kwa mikono yetu wenyewe na Taifa letu limeshinda kwa kubaki likiwa Imara na Tulivu.

Rais Samia na serikali yake ameipigana kwa uhodari,ujasiri na ushupavu mkubwa Sana Vita ya kuliletea Maendeleo Taifa letu,Amekuwa Ni Askari mzalendo na mvumilivu katika mapambano haya ya kulipa heshima Taifa letu kiuchumi,Amekuwa mstari wa mbele katika kujenga uchumi shirikishi unamgusa na kumnufaisha kila mmoja wetu pasipo kumwacha mtanzania yeyote nyuma.

Rais Samia Na serikali yake ameweka Alama katika kila Secta utakayo kwenda unakuta kazi kubwa imefanyika,unakuta Rais Samia ameirejesha Kodi na Tozo za mtanzania zikafanye kazi za kugusa maisha ya watanzania,kwa kutatua kero na changamoto zinazokuwa zinawakwamisha watanzania katika maisha yao ya kila siku pamoja na kujenga miradi mbalimbali inayomnufaisha mtanzania,

Rais Samia amemshika mkono kila mtanzania aliyehitaji kushikwa mkono na serikali yake,Rais Samia amezibeba secta zote na kuzipa umuhimu wa kipekee kwa kutambua kuwa watanzania wapo kila secta na hivyo kupuuza secta yoyote ni sawa na kuwapuuza watanzania na hivyo kuwadidimiza na kuwadhoofisha kiuchumi watanzania.

Kila mtanzania amefikiwa na kuguswa na juhudi za mh Rais,kila eneo limeguswa na kubebwa katika mikono na mabega ya mh Rais,kila sehemu kumefikiwa na kutazamwa na jicho la mh Rais ,kila mahali kumepitiwa na kupewa ufumbuzi,kila Kona ni matumaini kwa kesho iliyo Bora Zaidi ya leo.

Watanzania wamesikilizwa na kusaidiwa mahali walipo na wanapofanyia kazi na kuishi, watanzania wamepewa sikio la Rais kuwasikiliza na kuwapa majibu, Rais Samia Amezunguka Kanda zote na kutoa majibu kwa changamoto zinazotukabili,ametoa usuluhishi kwa migogoro, Amatufikisha hapa kwa Amani na utulivu.

Watanzania Tumeshinda kwa kufika hapa tukiwa wamoja na wenye ushirikiano,Tumeungana na serikali yetu na kusimama nayo katika nyakati zote,Tumempa ushirikiano na kumuunga mkono Rais wetu wakati wote alipotuhitaji kufanya Hivyo,Umoja wa kitaifa umekuwa mkubwa na wenye Afya kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya Taifa letu,Hatujatoa Nafasi kwa Adui yeyote aliyejaribu kutugawa na kutuchonganisha, Tumekuwa wavumilivu katika changamoto zote tulizozipitia Kama Taifa kwa kutambua na kuona juhudi kubwa zilizofanywa na Rais wetu mpendwa pamoja na serikali yake,

Ni matumaini yangu kuwa umoja huu tulioujenga Sasa tutaingia nao mwaka mpya na Kuendelea na kazi ya kulijenga Taifa letu litakalokuwa Bora Zaid ya hapa tulipo hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa Tumejaliwa na Mwenyezi MUNGU kuwa na Rasilimali nyingi ambazo zinatutaka kutumia akili na maarifa katika kuzitumia ili zisibadilike na kuwa Kama laana kwetu kwa kutuacha tukiwa maskini na fukara katikati ya utajiri wa Asili.

Kazi Iendeleee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu. 0742-676627
Lucas mwashambwa, tumeshinda nini iwapo familia 12 zinaiburuza nchi kadiri zitakavyo?
 
Aisee wewe sijui kaka, sijui baba umeamua kuwa chawa wa Mwanamke kabisa. Lima huko, teuzi za uchawa utaandika mabandiko 100,000 labda utafikiriwa kuwa katibu kata huko.
Mimi Ni mkulima Tayari,jembe langu ndio kalamu yangu,shamba langu ndio ofisi yangu,Na mabega yangu ndio begi langu, kwa hiyo usifikiri kuwa Mimi Sina kazi ya kufanya
 
Back
Top Bottom