Rais Samia ameua Mhimili wa Bunge, bado kumalizia wa Mahakama. Haya si ya kushangilia

Rais Samia ameua Mhimili wa Bunge, bado kumalizia wa Mahakama. Haya si ya kushangilia

Amelichuma janga muache alile.
Ndugai aliyeongoza kikao cha bunge kumpaka matope na kumdharirisha CAG prof ASSAD ndo huyu huyu ambaye kikao kijacho wanashuka naye jumla jumla.
Muosha huoshwa malipo tunalipwa hapa hapa dunia.
Lakini binafsi sijapenda alichofanyiwa ndugai na atakachofanyiwa japo naye alikuwa na mapungufu san
 
SUKUMA GANG hao!
Kwa aliyoyasema gwajima jana huyo ndugai wenu mnafiq na fitina tu. Kama suala lililetwa bungeni kwako ukalipitisha then unaenda kwenye media unamponda rais lengo lako nini? Alafu unashupaza shingo kwa sababu ya kukopa kwani huyo mama ndio wa kwanza? Ndugai kafanya mangapi ya kulimaliza bunge kabla hata huyo mama hajawa rais? Mbona mnachuki sana na mama nyie watu.?
 
Ndugai kakosa hekima na kutanguliza makasiriko mbele na hofu pia.. Kasemwa kidogo kajiuzulu ANGEKOMAA[emoji23]
Hoja ya Job kukomaa ingekuwa na mashiko kama asingekuja kuomba msamaha. Kitendo chake cha kuomba msamaha ambao hata yeye hakujua a naomba wa nini ndo kilimchomtafuna. Yeye alivokutana na wagogo kala chakula cha Kigogo ambacho hajala kwa muda kwa kuzoea mapocho pocho dish liliyumba akaanza kuropoka. Sasa ajiandae kupambana na stress na sukari. Ed yeye wakati anachomoa betri alipata farijiko kutoka Chadema. Job simuoni akienda kuombea ubunge tena. Namwona akiwa ni mhanga wa afya zaidi.
 
Haya yote yanayotokea na kushangiliwa hayana lolote katika ustawi wa Taifa hili.

Tunakwenda kuangamia. Jana/Juzi kitendo cha kumkemea Ndugai hadharani akajiuzulu, maana yake Bunge limesalimu amri kwa Executive. Kinachofuata ni kumalizia Mahakama maana alishaianza kuiua.

Matokeao yake unaweza usiyaone leo, lakini inaweza kuleta hata vita ya wenyewe kwa wenyewe baada ya kuwepo makundi ya KUONEA na KUONEWKun

Kuna makundi yatakataa kuonewa na yataungwa mkono na mataifa yanayo-advocate HAKI.

Tumkemee mtawala huyu! Tupaze sauti kuua Muhumili wa Bunge! pamoja na kuwa Ndugai alkuwa shetani, nunda mla watu.
Ndugai alipoambiwa bunge dhaifu akaanza bifu na waliomwambia ukweli. Sasa ngoja avune alichopanda. Kwanza bunge lenyewe limejaa wabunge haramu.
 
Umesema vyema. Huyu mama adhibitiwe kidogo. So far ana mema mengi kafanya ila ili la kushurutisha muhimili mwingine sio afya kwa demokrasia
Nani wa kumdhibiti? Ngedere wanaoshangilia miti kuungua?
 
Ndugai kakosa hekima na kutanguliza makasiriko mbele na hofu pia.. Kasemwa kidogo kajiuzulu ANGEKOMAA[emoji23]
Mmmhh mkuu sema ulitaka akomae ili uendelee kufaidi filamu! Lkn kujiuzulu kwake ndo ni kma filamu umeishia Kati Kati Kwa wengi
 
Hii nchi hata waziri wa mambo ya ndani mwenye siri zote za kivita aliwahi pigwa chini na maisha yalisonga.

Sembuse job.

Waziri wa mambo ya ndani ana siri za kivita? Kama ni hivyo je Waziri wa Ulinzi atakuwa na siri za nini sasa[emoji3][emoji3]
 
Mstaarabu kubaka bunge?
Kwani ndugai aliyasema yale akiwa bungeni? Au spika anakua na kinga ya uspika hata nje ya bunge?
Hilo bunge lenyewe lishabakwa kitambo sana wewe ulisikia wapi bunge lenye wabunge wasio na chama?
 
Umesema vyema. Huyu mama adhibitiwe kidogo. So far ana mema mengi kafanya ila ili la kushurutisha muhimili mwingine sio afya kwa demokrasia

Tatizo yeye anaona sawa. Anakuwa anapenda kuchambana! Mipasho kwenye uRais jamani!
 
lengo ni kujenga UTAWALA ulio BORA unaofuata Sheria na katiba ya Nchi.
Sasa kama unaona Samia ameua basi ni vizuri amejulikana ,kuliko lingetendwa na wasio julikana,maana hata huyo ****** isingejulikana yupo wapi.

Samia anahitaji kusaidiwa na sio kubaki kipekee pekee kama Bwana Yule,Samia analihitajia Bunge,mahakama katika kutekeleza Utawala Bora.
Bunge lililokuwepo linajulikana limechaguliwa kwa matakwa ya Bwana Yule. Lilikuwa halina msaada wowote isipokuwa faida ya kupiga makofi na kugonga meza, Na zaidi lilijaa vichekesho na malumbano ya sio na tija kufikia kuitwa mazuzu,kufikia kuitwa dhaifu.

Nahisi Ndugai alikong'oli wrong button.

Systematically, Samia alivunje Bunge ili uwepo uwiano ndani ya Bunge ingawa ni jambo zito kwa sasa,awahi kuunda tume Huru ili wananchi wachague wanaemtaka pale bungeni.
 
Kwani ndugai aliyasema yale akiwa bungeni? Au spika anakua na kinga ya uspika hata nje ya bunge?
Hilo bunge lenyewe lishabakwa kitambo sana wewe ulisikia wapi bunge lenye wabunge wasio na chama?
Hoja zake zinakuwa valid akiwa bungeni pekee?
 
Wajinga wengi hawatakuelewa. Wanamtazama Ndugai kama MTU, wenye hekima wanamtazama Ndugai kama Bunge. Ni aibu sana kwa Serikali kujivika ukuu kuzidi Bunge na Mahakama. Mara nyingi Serikali za aina hiyo ni Serikali dharimu.

Hakuna tena Bunge la Wananchi. Serikali inayokataa mawazo na maoni ya Raia wake ni Serikali inayopoteza uhalali.
Nilishauri kwamba hili suala limalizwe kiungwana...lkn inaonekana ni suala la maslahi binafsi ya watu, wanalitumia Taifa kama kisingizio tu. Uchu na tamaa za madaraka zimewajaa wahusika.
Viongozi kupigana vijembe hadharani ni kukosa maadili ya Uongozi.
 
Inashangaza kuona baadhi ya watu wakishangilia kwa kuwa tu wanamchukia Ndugai.

Hili si anguko la Ndugai as an individual bali ni janga la kitaifa
 
Si mlimuita Rais wa mpito,wacha awanyonyoe adi mtie adabu.
 
Anayeteseka Ni Mgogo na sio Hangaya......mbona kipindi Cha jiwe hakutuletea huo ujumbe?Sasa ndio kawa mwema akapumzike tu
Mgogo atatesekaje?

Ujumbe wake ulimchoma sana Hangaya ndio sababu alipanic namna ile. Na utaendele kumtesa hadi 2025!

Mgogo hata baada ya kukosa hicho kiti cha uspika yeye bado anapata kila kitu.
 
Mungu tulipie kisasi wote wavurugane watiane hasira, si unajua mtu akiwaga na hasira anaropoka? Na anachoongea kwa wakati huo ndo ukweli, watueleze ilikuwaje siku ile. Am enjoying the movie.
Ameeeen...!
 
Kwa aliyoyasema gwajima jana huyo ndugai wenu mnafiq na fitina tu. Kama suala lililetwa bungeni kwako ukalipitisha then unaenda kwenye media unamponda rais lengo lako nini? Alafu unashupaza shingo kwa sababu ya kukopa kwani huyo mama ndio wa kwanza? Ndugai kafanya mangapi ya kulimaliza bunge kabla hata huyo mama hajawa rais? Mbona mnachuki sana na mama nyie watu.?
Kukopa kuneemesha zenj ndiyo habari ya mujini! subirini Tik!! tik !! tok!! tok!! timing bomb!
 
Back
Top Bottom