Kama umewahi kuishi Zanzibar(Unguja na Pemba) utaona kabisa uchumi wa Zanzibar ni bomu ambalo linaweza kulipuka muda wowote ila uwepo wa Tanganyika unasaidia kupunguza ukali wa maisha kwa Zanzibar.
1. Kasi ya kuzaliana ni kubwa na eneo la ardhi ni dogo.
2. Uchumi unategemea Utalii, na ukiangalia kwa makini wanaojenga mahoteli ya utalii ni hao hao wazungu ila wazawa akina Faki wanaishia kuwa wahudumu na madereva wa watalii
2. Zao la biashara ni Karafuu na Mwani hayo mashamba ya karafuu mengi ni ya urithi hivyo hakuna mashamba mapya kwahiyo kama hajarithi shamba ndio basi tena.
3. Ajira tegemeo kubwa ni serikalini ambayo uwezo wake wa kuajiri ni mdogo sana. Huko kwenye utalii na uvuvi bado hakuna ajira inayoeleweka labda ujiajiri. Wengi ya vijana wanaomaliza chuo hukimbilia Tanganyika kubahatisha ajira.
4. Masoko, soko la Zanzibar ni dogo sana hata ukianzisha viwanda vingi idadi ya watu ni around 2.5M haifiki hata nusu ya wakaazi wa DSM. Hizo bidhaa unamuuzia nani? Hapa tegemeo la soko ni Zambia, Congo, Zimbabwe na ili ufike huko lazima upite Tanganyika au uzunguke Kenya.
5. Watu milioni 2.5 wa Zanzibar wana wabunge 40+ wanaolipwa na serikali ya Tanganyika lakini watu milioni 6 wa DSM wana wabunge 7/8. Zanzibar ilivyo Ubungo ni jimbo, Mwenge ni jimbo, makongo ni jimbo, kijitonyama ni jimbo, Mikocheni ni jimbo.
6. Kitu pekee kitakachokuja kuiokoa