Rais Samia amkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Hati ya Kiwanja

Rais Samia amkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Hati ya Kiwanja

Hiki chama nacho kisije kikawa tawi dogo la CCM.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Harold Sungusia Hati ya Kiwanja kilichopo Arusha kwa ajili ya Ujenzi wa Ofisi zao mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Harold Sungusia pamoja na ujumbe wake katika picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo yao Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya kumbukumbu na Wanasheria Wanawake wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) pamoja na Wanasheria Wanawake wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 14 Agosti, 2023.

Hawa TLS jina lao lina-ax eneo linaloleta valangati flani ktk ardhi hii. Wajumbe wake wengi ndo hao walojaa ktk mhimili wa mahakama. Kualikwa kwao itabidi kufuatiwe na cha
Madaktari, kilimo, waalimu na taaluma zngn zote. Nje ya hapo watu watajiuliza, "why TLS and not the others,
the timing ...etc". Kwngu mm kdgo na imani na hawa wanachama wa TLS. Sjui kama huyu M/kt wa ss kafika bei. Let's keep our fingers crossed. Time will tell. Ingekuwa ushauri, ningeomba Mama asifanye maamuzi ambayo, kwa muda huu, yataonekana kuwa na uhusiano na kilichoko mahakamani au mambo ya Bandari...nk
 
Back
Top Bottom