Ukimsikiliza huyo Rais wa TLS Sungusa kuna kitu amekisema
'' Tupo tayari kutoa elimu ya sheria kuhusu KATIBA inayohusu mambo yanayowagusa Wananchi kiuchumi na kimaisha''
Si elimu ya Haki Jinai wala si elimu ya Mirathi au Elimu ya Ardhi. Ni elimu ya KATIBA
Hii kauli inaashiria kwamba TLS watapewa kazi ya kutoa elimu ya katiba kwa kushirikiana na ''Msajili wa vyama', Kamati ya Prof Mkandara na Tume ya Haki jamii. Yote hayo ni katika kutekeleza kile serikali inataka.
Si tuliambiwa TLS walikuwa na Kiwanja wakati wa Tundu Lissu halafu Fatma Karume na hata Hosea. Hivi walianzaje kujenga bila kuwa na hati? Mbona hatujasikia hati ya taasisi nyingine kama chama cha Injinia, Madaktari au Wahasibu vikitolewa Ikulu !
Nimesikia mtu mmoja akisema TLS ni '' Tanzania Lost Society'' !
JokaKuu Pascal Mayalla