Rais Samia amkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Hati ya Kiwanja

Rais Samia amkabidhi Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Hati ya Kiwanja

Kwa Position na majukumu ya TLS kuna vitu lazima waviepuke hasa hivi vya kutafuta huruma kutoka kwa watawala.

Wanashindwa kuchangishana kununua kiwanja? Ni hadi wangoje kupewa kama zawadi?

Hii zawadi haitaenda bure lazima TLS wailipe in kind,Hati ya kiwanja haijatolewa bure no free Lunch.

Sasa kama wabobezi wa sheria wana fanya hsys vipi sisi tusio kuwa hata ns ABC za sheria? hii ni Tassisi inayo paswa kusaidia kusimamia haki nchi hii wamepewa zawadi na watawala unategemea nini?

TLS ni watalamu wa sheria wanaweza vipi kukubali vitu rahisi kama hivi vya zawadi za kiwanja?

Nimeshangaa sana kwa hili na sitarajii hawa jamaa kuwa na mstari wa mbele tena kupigania haki kwenye nchi hii binafisi nimewadelete kuanzia leo.

Law Society of Kenya(LSK) huwezi pata picha wakiwa wamepiga na watawala hata pia Viongozi wa Upinzani kwa kifupi hawana upande wanacho angalia ni ukikwaji wa wazi wa katiba ya Kenya na hawawezi itwa Ikulu wakakubali kwenda make wanajua impact yake kweny kupigania haki.Hawa TLS yetu ni full njaa.

Hawa TLS wetu kitendo tu cha kuona picha wakiwa Ikulu na pia wakikabidhiwa kiwanja nikajua ndio kazi kwisha hawa ni watalamu wa sheria wameisha fika bei na mbaya zaidi Watawala wamefanya timing ya kungoja kwenye hili sakata la DP ndio wawape zaiwadi ya kiwanja.

Usitarajie kuwasikia wakitoa negative statment dhidi ya watwala tena.
Ulitaka wakatae ili iwejeee
 
Kiwanja walipewa siku nyingi sana, leo wamekabidhiwa hati tu.
 
Wanasheria siyo maadui au mahasimu wa serikali. Wajibu wao ni kuisaidia serikali iendeshe shughuli zake kwa mujibu wa sheria.

Sasa kama serikali inawapa kiwanja cha kujenga ofisi za chama chao, ni jambo jema linaloonesha kuwa serikali inataka kutenda kisheria zaidi.

Hata hivyo, ni muhimu sheria ziwe za haki hivyo serikali haitakiwi kufanya hivyo kama njia ya kuwafanya wanasheria wasisimamie haki.
 
Wamekuwa outsmarted mbele ya kadamnasi ili wasigomee zawadi kama wale "walimu" waliogomea teuzi.Na hawapewi nafasi ya kuijadili zawadi.
 
Kiwanja walipewa siku nyingi sana, leo wamekabidhiwa hati tu.
Hata kama still ni ujinga, hawa wanashindwa wao kumiliki kiwanja chao? Vipi wapigania Uhuru na wao wangeanza kupewa vitu kama hivi unazania Uhuru ungepatiakana?

TLS wanapaswa kusimami haki, wanapo anza kuhongwa viwanja tambua hakuna kitu tena wanaweza fanya, na watakuwa na msosi wamepiga kabisa kule Ikulu
 
Wanasheria siyo maadui au mahasimu wa serikali. Wajibu wao ni kuisaidia serikali iendeshe shughuli zake kwa mujibu wa sheria...
Vipi kama Serikaki haifuati katiba unazani kuna watakacho weza kufanya? Wafuatilie Law Society of Kenya uone kazi zao hawana muda wakujikomba kwa watawala.
 
Hata kama still ni ujinga, hawa wanashindwa wao kumiliki kiwanja chao? Vipi wapigania Uhuru na wao wangeanza kupewa vitu kama hivi unazania Uhuru ungepatiakana...
Sasa hayo yako mengine mimi siwezi kuwajibia. Kwanini hauwapigii simu ukawauliza?
 
Ni tabia za wabongo kupenda vya dezo
 
Mkuu kwa akili za Wabongo unazani kuna kitu wana ng'amua ? sijui ni Mungu akitupiga upofu au ni basi tu.
Kuna taasisi zinapaswa kuheshimiana,kujadiliana na hata wakati mwingine kukubaliana kutokukubaliana mambo.Hakuna ulazima wa kupeana "zawadi" au "misaada" itakayoumba kutokuaminika hasa na jamii inayowatazama.
 
Back
Top Bottom