Pre GE2025 Rais Samia ampa Sheikh wa Arusha Land Rover Discovery limsaidie kwenye shughuli za kidini. Hii si Rushwa kabisa?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
EEEeeeenHEEEEeeeeee!

Inabidi kucheka tu, sasa tufanyeje?

Hii nchi bhwanah; imekuwa kama hawa viongozi wanawaona wananchi wao kuwa wajinga wa kupindukia.

Nadhani ni huko huko Arusha kuliko fanyika mazingaombwe ya kurudisha ardhi ya Kanisa iliyo porwa, pamoja na Tsh 500 milioni, kama sikosei. Sasa hii.

Yote haya yatahakikisha ushindi wa kishindo toka kwa wajinga, waTanzania?

Ushindi ukisha patikana je! Hao wanao tununua sasa hivi ruhusa kwao kututia vidole? Gesi ya Ntorya naona hawakuwa na subira kusubiri uchafuzi upite kwanza, baada ya uchafuzi, tutegemee makubwa zaidi kuliko tuliyo wahi kuyaona?
 
Only inTz
 

Rais Samia Suluhu Hassan amemzawadia Sheikh wa Mkoa wa Arusha Sheikh Shaaban Bin Juma gari aina ya Land Rover Discovery 4 lenye thamani ya shilingi milioni 100 ili limsaidie kwenye shughuli zake za kidini.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amemkabidhi Sheikh Shaaban gari hilo leo Ijumaa baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa kwenye msikiti Mkuu wa Bondeni Jijini Arusha leo Oktoba 25, 2024.

Wakati wa kukabidhi gari hilo RC Makonda amenukuliwa akisema yafuatayo “Huyu Baba yetu na Sheikh wetu wa Mkoa alikuja siku moja pale ofisini nikamwambia Baba nikusindikize, tukaenda mpaka tukatoka kwenye geiti nje naitafuta gari sikuiona, mwisho nikamuona anahangaika kupiga simu ‘leta huku gari leta’......alivoleta ile gari nilivyoiona moyo wangu uliingia huzuni nikasema hii gari ndio itakua ya mwanzo na mwisho kuitumia”

“Nikasema kwakuwa mimi sina pesa lakini ninae Mungu anaeweza kuniwezesha, nikampigia simu Daktari Samia Suluhu Hassan akasema hivi Viongozi wa dini we Mtoto unawapenda eeh? sijakaa sawa siku ya pili akapatikana Kijana akaniletea pesa kwahiyo leo nimekuja kumkabidhi Sheikh wangu wa Mkoa gari lake atakalokuwa analitumia kama mali yake, namshukuru sana Daktari Samia” - RC Makonda.
 
"sijakaa sawa siku ya pili akapatikana Kijana akaniletea pesa" hii tungo tata tuanzie hapa kwanza
 
Hawawazi kufungua shule, hospital nk...awe anamuwekea na mafuta kabisa ikibidi
 
Ma shaa Allah.

Sheikh kawasilimishe Wamasai wengi wengi huko, wanaupenda sana Uislam.
 
Tukienda kwenye "byuro di chenji" hizo ni kura toka kwa waisilamu wa Arusha na watakaoguswa mikoa mingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…