Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Genge la chato akili zenu bana
Kwa hiyo unasema rais hana vyanzo vya habari kuyajua majambazi?
 

Hadi lile genge lote la kabila letu pendwa lisambaratike lote. Kwani hamjijui?
 
Kama uko nae hapo bar amekuagizia bia basi acha kunywa sepa haraka.. Hawezi kulipia hiyo bia sababu ya mawazo.

Pole
 
Saa hizi anacheka tu, natamani nipate connection ya WhatsApp group ya CCM nione wanavyokorogana saa hizi

Nyie nanyi mnajitekenya na kucheka wewenyewe heheheeee

Alitumbuliwa Lowasa akiwa waziri, wakatumbuliwa mawaziri kina Lugola mkuu sembuse mkuu wa wilaya SabayaπŸ™„πŸ™„

Hiyo ndio CCM baba lao
 
Mbona huko clouds alisema ana miaka 35 na hapa kwenye CV kazaliwa 1980
Miaka 35 ni sahihi ,kipind anasoma Ikizu sekondari akiwa form four mi nilikuwa form one mwaka 2006...jamaa alikuwa mbabe Sana , alikuwa na kundi la wannyanyua vyuma , yeye alikuwa wa mwisho kuingia dining hall na kundi lake na haiwezekani kuruhusiwa Kula bila yeye na kundi lake hawajafika , ni mtu wa system pia , Baba yake by that time alikuwa ni mkuu wa wilaya ya Serengeti kama sikosei
 
Thanks mama,wewe ni kitu kimoja na mwendazake ila sio sawa sawa na mwendazake,hii uwe mwazo wa funzo KWA wateule wote na vijana kwamba ofis ni dhamana Kuna leo na kesho,THANKS MAMA
 
CCM wanajua Watanzania wengi wamejeruhiwa na Mwendazake, kilichopo saizi wanawaponya majeraha...2025 wanakuja na gia nyingine.

Kwa Hali hii ccm itatawala miaka mingi ijayo, maana wanajua kula na vipofu.
 
Hahahahahahaha lol! Waambie waangalie wasiuvae mkenge kwani kama wana uraia wa huko waliko basi wasije kulizwa.
Mimi nimeanza Kunywa tokea Asubuhi kuna Mabest wangu Wamerejea kutika Ughaibuni wamekuja Kuwekeza Nchini kwao.

Hizi habari zimetufanya tulipuke kwa furaha shangwe na Vigelegele
 
Ni Jambo kua na rais anayesikiliza,

Mama katumia busara Sana, kasema kasimamishwa kupisha uchunguzi.

Hajafukuzwa, atafukuzwa zikithibitishwa tuhuma zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…