Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Hili limefanyika kabla ya Eid,kweli mama amechukizwa na kusumbuliwa kwa wafanyabiashara wake
 
Chanzo cha habari [emoji848]
 
Yaani huyu mama anajua kumalizia sikukuu yangu vizuri kweli, hela sina Ila napata raha tu.

Walikuja kumsafisha humu tukawaambia katika mambo aliyobugi ni kufanya ile interview ya clouds, pale amemchokonoa pweza aisee. Mama akikaa kimya anatafuta namna ya kumuondoa kimya Ila amemlazimisha mama amuondoe kwa kashfa akazijibu.

Meaning ameshtakiwa kiuongozi aisee hii sio kutenguliwa amefukuzwa kwa kashfa. Ameharibu CV.

Sasa waliokuwa wanamtetea wakamsaidie kujibu tuhuma. Kenge wakubwa
 
Huyu alikuwa wa kumfukuza kazi kisha kukusanya udhahidi dhidi ya maovu yake mbali mbali ya kupora watu, kuwadhalilisha kwa namna mbali mbaliu, kuwalawiti na kuwajeruhi nadhani pia kuna tuhuma za mauaji dhidi ya huyo dhalimu.
Wakimfukuza wanakuwa wamemhukumu na hivyo kupata escape route, lengo la kumsimamisha ni ili kumkondesha kwanza, na aonyeshe network yake yote na hatimaye ajinyonge, mwenyewe
 
Ole Sabaya alikuwa Mungu mtu, alijifanya anajua kila kitu, ualimu yeye, udaktar yeye, u fanya biashara yeye, tajir yeye, usalama wa taifa yeye, fitina yeye. Alikuwa mtu hatar kuliko wote Kilimanjaro asiyeogopa kitu chochote na kiongoz yeyote.

Namshukuru MAMA, Rais wangu Samia hatuna cha kukupa nakuombea kwa Mungu akulinde na akupe busara uendelee kukupa hekima. Tumepoteza Ndugu zetu kwa sababu ya Ole Sabaya, Ndugu zetu wameumizwa mno na Ole Sabaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…