Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Wakimfukuza wanakuwa wamemhukumu na hivyo kupata escape route, lengo la kumsimamisha ni ili kumkondesha kwanza, na aonyeshe network yake yote na hatimaye ajinyonge, mwenyewe
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
Eti 'kumkondesha kwanza'.
 
Huyu Madam SSH anafanya kazi au anafanya maamuzi kwa kusikiliza kelele na porojo za mitandaoni.

Ni hatari sana kuwa na Rais anayesikiliza umbea, udaku na mihemuko ya mitandaoni kisha anachukua maamuzi ili kuwaridhisha followers wake.
Kaaazi kweli kweli!!!

Unahisi kakosea kukutoa
 
Huyu alikuwa wa kumfukuza kazi kisha kukusanya udhahidi dhidi ya maovu yake mbali mbali ya kupora watu, kuwadhalilisha kwa namna mbali mbaliu, kuwalawiti na kuwajeruhi nadhani pia kuna tuhuma za mauaji dhidi ya huyo dhalimu.
Nafikiri kusimamishwa kupisha uchunguzi maana halisi ni kuwa kama kuna matukio ya jinai atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.

Maana kama angetengua tuu hiyo ingekuwa imetoka basi na kusahaulika.
Tunawaomba wote wenye ushahidi wa maovu yake wasisite kujitokeza kutoa ushahidi
 
Mungu ni mwema wakati wote.

Ni vema DC Ole sabaya akamwomba radhi mama Mghwira kwa namna yeye na DC mstaafu wa Moshi mh Kippi walivyokuwa wanamdharau kwa sababu tu ametokea kwenye chama cha upinzani.

Hawa vijana wawili walimpa wakati mgumu sana Dr Mghwira na zaidi Ole aliutamani uRC.

Eid Mubarak!
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili kuanzia leo, Mei 13, 2021

Aidha, Rais Samia amefanya teuzi za Viongozi mbalimbali ambao uteuzi wao unaanza leo
View attachment 1783582

Habari ndo hiyo

Nawatakia Eid Njema.

====
Alizaliwa mwaka 1980 katika mkoa wa Arusha

CHAMA: CCM

#NA SASA KAZI IMEANZA#


TAARIFA ZA ELIMU YAKE


SVISC. MASSACHUSET UNIVERSITY USA

BSC.ED ST JOHN UNIVERSITY DODOMA

UNED: SINIOUR SIX –BUGEMA HIGH SCHOOL-UGANDA.

FORM IV: IKIZU SEC SCHOOL

STD VII: SAMBASHA PRIMARY SCHOOL.

OTHERS: IST: PRESIDENT ST. JOHN’S UNIVERSITY DODOMA 2007.

CHAPEL PREFECT BUGEMA HIGH SCHOOL UGANDA.

CEO: TANZANIA YOUTH DEVELOPMENT CENTRE

SEMINARS BSYMPOSIUM: S. KOREA YOUTH CONFERENCE ,SOUL

YOUTH SUMMIT COMMISSIONED BY HON. PINDA TYDC:2010

CAPRIPOINT YOUTH EMPOWERMENT 2014

View attachment 1783581
Huyu tulimwambia mahojiano na Clouds hayata mwacha salama. Sasa akachambie rungu.
Maana uchunguzi lazima umpeleke mahakamani.
Jambazi, muuaji, ajue kuna watu wanao sali.
Asante Mungu kwa kujibu sala zetu.
Tujitokeze kwa wingi Arusha na Moshi kutoa ushahidi.
 
Ukizingua Mama anakuzingua, haya ndo masalia ya Bwana yule yaliyozidi kujimwambafai hata katika awamu ya sita! Mama Hongera, hii inaonesha jinsi ulivyo msikivu tofauti na Bwana Yule!

Mama Samia Suluhu Hassan, Mungu akupe maisha marefu
Salamu tosha kwa kina Ndugai na genge lake. Jana nilimtaka Saa Mbaya awatake radhi wote aliowakosea. Hakunielewa. Chala mguu sawa. Kaskazini hadi Kusini.
 
Hapo mwisho hapana mkuu huko ni kumdhalilisha Rais wetu na kumtweza kusikohimilika tuwe na staha
Ukiwa kiongozi mwenye maono muite na muulize tatizo ni nini? Baada ya hapo tafuta mbinu ya kusikiliza upande unaolalamika baada ya hapo fanya maamuzi, tofauti na hivyo huu ni mwendelezo wa Rais anae sikiliza maoni ya watu pasipo kujiridhisha.
 
Back
Top Bottom