Rais Samia amsimamisha kazi Ole Sabaya, Mkuu wa Wilaya ya Hai ili kupisha uchunguzi wa tuhuma dhidi yake

Sabaya amesimamishwa kazi sababu ya tuhuma. Na wanaofurahia kusimamishwa kwake kazi ni wanachama wa CHADEMA. Watu wenye upeo wa kufikiri tunajiuliza maswali mengi na machache kati ya hayo ni haya :
1- tuhuma zinazomkabili Sabaya sio za leo wala jana, ni tuhuma za kuanzia mwaka jana kurudi nyuma. Sasa je, wakati Sabaya anatuhumiwa, huyu Madam SSH yeye hakuwa Makamu wa Rais? Alichukua hatua zipi dhidi ya Sabaya kwa nafasi aliyokuwa nayo?
2- Madam SSH akisema kipindi hicho hakuwa na sauti, Je, sasa hivi akiwa kama Rais yuko tayari kuchukua hatua dhidi ya kila tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwa viongozi au Serikali anayoiongoza sasa hivi?
Hata chama chake CCM kinatuhumiwa sana kwa udanganyifu na wizi wa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Je, Madam SSH yuko tayari kufanyia kazi hizo tuhuma kwa kuruhusu uchunguzi huru dhidi ya chama chake na ikiwa itathibitika kuwa kweli waliiba kura, Je, atakuwa tayari kujiuzulu na kupisha uchaguzi mwingine ufanyike?
3- Spika wa Bunge, Job Ndugai anatuhumiwa sana kuisigina katiba ya nchi, Je, Madam SSH yuko tayari kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine maana mamlaka hayo anayo.
4- Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatuhumiwa kudhulumu haki za kuishi za baadhi ya watu, Je, Madam SSH yupo tayari kupisha uchunguzi huru dhidi ya Makonda?
5- Usalama wa Taifa wanatuhumiwa kuhusika na tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu, Je, Madam SSH yupo tayari kuruhu FBI wafanye uchunguzi wao kama walivyotaka kufanya baada ya tukio na kuzuiliwa?
Ikiwa Madam anasikiliza tuhuma za mitandaoni, Je, sio sahihi kwa yeye kusikiliza na kuchukua maamuzi dhidi ya tuhuma hizo nilizoziainisha hapo juu??

Na hapo sijataja tuhuma za utekaji watu, kupotea kwa baadhi ya watu kama Azory n.k.
Au Watanzania mnapenda sana kushabikia vitu pasipo kufikiri kwa kina? Hamjui kwamba wanasiasa wote wamejaa unafiki?
Madam SSH yeye siyo MALAIKA, yeye ni Mwanadamu tena mwanasiasa. Hana tofauti na aina za wanasiasa tuwajuao.
Kaa kwa kutulia mkuu! It is slowly but surely, Mama hawezi akashughulikia maswala yote kwa siku moja lakini lazima Hii nchi inyooke! Sukuma gang yote outt, Miungu-watu wote lazima wawajibishwe
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemsimamisha kazi Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili kuanzia leo, Mei 13, 2021

Aidha, Rais Samia amefanya teuzi za Viongozi mbalimbali ambao uteuzi wao unaanza leo

Habari ndo hiyo

Nawatakia Eid Njema.

====
Alizaliwa mwaka 1980 katika mkoa wa Arusha

Hayati John Pombe Magufuli tarehe 28 Julai, 2018 alimteua Sabaya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai

CHAMA: CCM

#NA SASA KAZI IMEANZA#

TAARIFA ZA ELIMU YAKE

SVISC. MASSACHUSET UNIVERSITY USA

BSC.ED ST JOHN UNIVERSITY DODOMA

UNED: SINIOUR SIX –BUGEMA HIGH SCHOOL-UGANDA.

FORM IV: IKIZU SEC SCHOOL

STD VII: SAMBASHA PRIMARY SCHOOL.

OTHERS: IST: PRESIDENT ST. JOHN’S UNIVERSITY DODOMA 2007.

CHAPEL PREFECT BUGEMA HIGH SCHOOL UGANDA.

CEO: TANZANIA YOUTH DEVELOPMENT CENTRE

SEMINARS BSYMPOSIUM: S. KOREA YOUTH CONFERENCE ,SOUL

YOUTH SUMMIT COMMISSIONED BY HON. PINDA TYDC:2010

CAPRIPOINT YOUTH EMPOWERMENT 2014

Sam , Kija na Simalenga inabidi tu irudishwe hela aliyowapa Sabaya na Sam ni wakulaumiwa kwani ndiye aliyemshawishi Sabaya afanye interview
 
Tuacheni siasa za kinafiki ambazo hazina tija kwenye jamii yetu. Kama mkuu wa nchi ambae unatakiwa kuleta ustawi wa jamii yetu unatakiwa usafishe kila kiongozi asiyefaa ili ulete ustawi wa jamii

Ok tuelezane ukweli bila kupepesa macho ni Sabaya pekee ambaye hafai?

Mbona wengi tu ambao hawafai. Ambao kama mkuu wa nchi unatakiwa uwaondoe mara moja.

Mfano, ondoa mkuu wa mkoa wa Mwanza huyu hafai kabisa maana ni ni kama doli tu. Na kibaraka wa kutetea uvunjifu wa haki za binadamu. Mkuu wa mkoa wa Mbeya ondoa kabisa maana hafai na wala maelezo hayahitajiki.

Ondoa wote wasiofaa bila kufuata mbinyo wa kisiasa.
 
nisaidie kuhufadhi hii coment yangu.utakuha kuelewa mbeleni huko kwa sasa demka.
Hahahaha... Unachonifurahisha tu ni jinsi ambavyo sasa hivi umechukua nafasi ya Bavicha kuwa mpinzani wa Serikali ya CCM.
 
Tuacheni siasa za kinafiki ambazo hazina tija kwenye jamii yetu. Kama mkuu wa nchi ambae unatakiwa kuleta ustawi wa jamii yetu unatakiwa usafishe kila kiongozi asiyefaa ili ulete ustawi wa jamii

Ok tuelezane ukweli bila kupepesa macho ni Sabaya pekee ambaye hafai?

Mbona wengi tu ambao hawafai. Ambao kama mkuu wa nchi unatakiwa uwaondoe mara moja.

Mfano, ondoa mkuu wa mkoa wa Mwanza huyu hafai kabisa maana ni ni kama doli tu. Na kibaraka wa kutetea uvunjifu wa haki za binadamu. Mkuu wa mkoa wa Mbeya ondoa kabisa maana hafai na wala maelezo hayahitajiki.
Usiwe na papara Mama amampenda kila Mtoto,aliyekosea atamwelekeza kadiri ya malezi ya Mama.
 
Tuacheni siasa za kinafiki ambazo hazina tija kwenye jamii yetu. Kama mkuu wa nchi ambae unatakiwa kuleta ustawi wa jamii yetu unatakiwa usafishe kila kiongozi asiyefaa ili ulete ustawi wa jamii

Ok tuelezane ukweli bila kupepesa macho ni Sabaya pekee ambaye hafai?

Mbona wengi tu ambao hawafai. Ambao kama mkuu wa nchi unatakiwa uwaondoe mara moja.

Mfano, ondoa mkuu wa mkoa wa Mwanza huyu hafai kabisa maana ni ni kama doli tu. Na kibaraka wa kutetea uvunjifu wa haki za binadamu. Mkuu wa mkoa wa Mbeya ondoa kabisa maana hafai na wala maelezo hayahitajiki.

Dotto

Kakurwa

DPP

Polepole
 
Sabaya amesimamishwa kazi sababu ya tuhuma. Na wanaofurahia kusimamishwa kwake kazi ni wanachama wa CHADEMA. Watu wenye upeo wa kufikiri tunajiuliza maswali mengi na machache kati ya hayo ni haya :
1- tuhuma zinazomkabili Sabaya sio za leo wala jana, ni tuhuma za kuanzia mwaka jana kurudi nyuma. Sasa je, wakati Sabaya anatuhumiwa, huyu Madam SSH yeye hakuwa Makamu wa Rais? Alichukua hatua zipi dhidi ya Sabaya kwa nafasi aliyokuwa nayo?
2- Madam SSH akisema kipindi hicho hakuwa na sauti, Je, sasa hivi akiwa kama Rais yuko tayari kuchukua hatua dhidi ya kila tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwa viongozi au Serikali anayoiongoza sasa hivi?
Hata chama chake CCM kinatuhumiwa sana kwa udanganyifu na wizi wa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita, Je, Madam SSH yuko tayari kufanyia kazi hizo tuhuma kwa kuruhusu uchunguzi huru dhidi ya chama chake na ikiwa itathibitika kuwa kweli waliiba kura, Je, atakuwa tayari kujiuzulu na kupisha uchaguzi mwingine ufanyike?
3- Spika wa Bunge, Job Ndugai anatuhumiwa sana kuisigina katiba ya nchi, Je, Madam SSH yuko tayari kulivunja Bunge na kuitisha uchaguzi mwingine maana mamlaka hayo anayo.
4- Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatuhumiwa kudhulumu haki za kuishi za baadhi ya watu, Je, Madam SSH yupo tayari kupisha uchunguzi huru dhidi ya Makonda?
5- Usalama wa Taifa wanatuhumiwa kuhusika na tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu, Je, Madam SSH yupo tayari kuruhu FBI wafanye uchunguzi wao kama walivyotaka kufanya baada ya tukio na kuzuiliwa?
Ikiwa Madam anasikiliza tuhuma za mitandaoni, Je, sio sahihi kwa yeye kusikiliza na kuchukua maamuzi dhidi ya tuhuma hizo nilizoziainisha hapo juu??

Na hapo sijataja tuhuma za utekaji watu, kupotea kwa baadhi ya watu kama Azory n.k.
Au Watanzania mnapenda sana kushabikia vitu pasipo kufikiri kwa kina? Hamjui kwamba wanasiasa wote wamejaa unafiki?
Madam SSH yeye siyo MALAIKA, yeye ni Mwanadamu tena mwanasiasa. Hana tofauti na aina za wanasiasa tuwajuao.

Mkuu umeandika mengi mazuri tu, ila hapa hujatenda haki:

"Na wanaofurahia kusimamishwa kwake kazi ni wanachama wa CHADEMA."

Ukasahau kuwa wanaofurahia ni watanzania wazalendo. Wamo chadema na hata wasiokuwa Chadema, wengi tu.

Ukaenda mbele na kujitofautisha na hao unaowaita Chadema kwa kudai:

"Watu wenye upeo wa kufikiri tunajiuliza maswali mengi na machache kati ya hayo ni haya."

Kumbuka hakuna hati miliki ya kuwa na upeo wa kufikiri. Ndiyo maana waswahili walituasa kuwa "umdhaniaye siye, ndiye" na pia "ajidhaniaye kasimama na aangalie asije akaanguka."

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Mzee Mgaya anasema unaposikia kiongozi fulani amesimamishwa kazi na Rais wa JMT basi elewa tuhuma hizo zimeshafanyiwa kazi na kinachoendelea ni taratibu za kisheria tu.

Rais ni taasisi, hivyo ana uwezo wa kupata taarifa zote anazozihitaji kwa wakati muafaka, anasema Mgaya.

Kuongea na vyombo vya habari wakati Takukuru wanakusubiri kwa mahojiano nayo ni aina fulani ya dharau na kiburi, anatoa angalizo mzee Mgaya.

Eid Mubarak!
 
MATAGA hapa hautawaona
 
Back
Top Bottom