JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi jioni ya Aprili 14, 2022 kama ifuatavyo:
Amemteua Rosemary William Slaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bohari ya Dawa (MSD), Bi. Slaa ni Afisa Mwandamizi katika Kampuni ya Picenaterhouse Coopers PWC.
Amemteua Mavere Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Tukai ni Kiongozi Mkuu wa Mradi wa USAID Global Health Supply Chain Technical Assistance.
Amemteua Raymond William Mndolwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mndolwa ni Mtaalam wa Operesheni, Kampuni ya STC Construction, Dar es Salaam.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus ni kuwa uteuzi huo unaanza mara moja.