Rais Samia amtumbua Kamishna Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya

Rais Samia amtumbua Kamishna Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya

Ngusa Dismas Samike awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli aliwahi kuwa Mnikulu Ofisi ya Rais, Ikulu.


1678982212910.png



May 31st, 2022
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Ngusa Samike ameishauri Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba,TMDA kuongeza elimu zaidi kwa jamii kuhusiana na athari za matumizi ya bidhaa zitokanazo na Tumbaku.

_IMG_0615.jpg


30 December 2022
Ngusa Dismas Samike katibu tawala mkoa wa Lindi atembelea Kilwa kukagua miradi

 
Hivi mtu akitolewa kwwnye u Katibu Mkuu akafanywa Kamishna ni kupandishwa cheo? Na kutoka u Kamishna kuwa RAS ni kushushwa cheo? Ninavyojua cheo cha RAS ni sawa na KM kama vile RC alivyokuwa sawa na Waziri....
Siyo kweli kabisa!

Waziri ni senior kwa RC. Waziri anamuagiza RC kufanya kazi fulani lakini RC hawezi kuthubutu. RC anamuomba Waziri ili aweze kufanya kazi fulani lakini Waziri hawezi kumuomba RC ili aweze kufanya kazi fulani ndani ya mkoa wake.

Halikadhalika katibu mkuu ni senior kwa RAS kwa sababu kama nilizoeleza hapo juu!

RC na RAS wana-report kwa Waziri wa TAMISEMI wakati Mawaziri wana-report kwa Rais.
 
Yaani kabla mtu hajajifunza A na B anatimuliwa anawekwa mwingine

Ndio maana nchi inashindwa kuwa na muelekeo
Halafu tunauliza kwanini umeme unakatika ooh mbona hela zimeibiwa

Wataachaje kuiba wakati mnawabadilisha badilisha tu
 
Siyo kweli kabisa!

Waziri ni senior kwa RC. Waziri anamuagiza RC kufanya kazi fulani lakini RC hawezi kuthubutu. RC anamuomba Waziri ili aweze kufanya kazi fulani lakini Waziri hawezi kumuomba RC ili aweze kufanya kazi fulani ndani ya mkoa wake...
Not true. Waziri hawezi kumuagiza RC afanye kazi. RC ni mwakilishi wa Rais katika Mkoa na Waziri akiingia katika mkoa wake anatakiwa kwenda kusaini ofisini kwake.

RC ana mamlaka ya kumtia mtu ndani wakati waziri hana. RC atamuomba kitu waziri kwa sababu waziri anasimamia sekta husika na sio kwa sababu ni Boss wake.

RC akitaka barabara ijengwe mkoani mwake atawasiliana na waziri husika lakini haina maana kuwa yuko chini yake. RC na DC hawawajibiki kwa waziri wa Tamisemi. Mnakumbuka mara ngapi Jafo alikuwa anawalalamikia ma DC wakora bila matokeo yeyote. Lakini RC anaweza kumpa taabu DC.

Watu tunawaona mawaziri ni mabosi kwa sababu wanasimamia sekta fulani nchi nzima ( na hivyo kuwa na bajeti) na wamo katika Baraza la Mawaziri. Tunawadharau ma RC kwa sababu wanaishi sehemu kama Lindi na Mpanda. Makazi ya RC yanajulikana kama Ikulu ndogo na kama mkoa hauna makazi rasmi ya kufikia Rais huwa anafikia kwa RC.

Katibu Mkuu hivyo hivyo sio senior kwa RAS kwa sababu nilizozitaja hapo juu. Wote ni accounting officer. Katibu Mkuu anatamba kisekta lakini RAS kijiografia.

Amandla...
 
Huyu kamishina wa madawa ya kulevya alimteua yeye mwenye baada ya kumuondoa aliyekuwepo toka kipindi cha JPM

Kwa hiyo sasa ametengua uteuzi wake
 
Siku moja kabla ya kumbukumbu ya kifo cha Magufuli anamtumbua Samike katibu wake

20 Mar 2022
MSAIDIZI WA MAGUFULI AMLIZA MICHUZI, AELEZEA KWA UCHUNGU MAISHA YA MAGUFULI YALIVYOKUWA


Bw. Ngusa Dismas Samike, aliyekuwa msaidizi wa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, akimuelezea marehemu wakati wa Misa Maalumu ya kumbukizi ya mwaka mmoja wa kifo cha Dkt. Magufuli iliyofanyika kanisa la Kawekamo jijini Mwanza Jumapili Machi 20, 2022
 
Back
Top Bottom