Rais Samia amtumbua Kamishna Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya

Rais Samia amtumbua Kamishna Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya

View attachment 2553881

View attachment 2553882

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya baadhi ya viongozi kwa kuwateua Makatibu Tawala wa Mikoa watatu (3) na kuwahamisha vituo vya kazi wengine watatu (3). Aidha, Mhe. Rais amefanya uteuzi wa Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya. Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:-
Baada ya muda utakuja sikia hao hao waliostaafu kuteuliwa Tena katika nafasi nyinginezo, kama vile hakuna wenye sifa za kushuka hizi nafasi.

Wanaofauli vyuo wako lukuki na hata ndani ya Serikali vijana walioko kazini muda bila kupanda daraja wapo!
Nchi ngumu sana.

Ndio maana KATIBA KATIBA mpya muhimu. Punguza madaraka ya Rais na kuwepo na usaili au kupigiwa kura Kwa Hawa watu kwenye nafasi mbalimbali
 
Not necessarily, atapangiwa kazi nyingine!.

Ila pia ninanote demotions za kiaina!.

Mtu alikuwa KM, akapandishwa kuwa Kamishna, halafu sasa anashushwa na kuwa RAS!. It's not fair, kanuni za Utumishi wa umma zifuatwe. Ukimshusha mtu wa level ya PS, mtupe ubalozini!.

P
Maza kawaondoa vijana wote wa JPM(Wasukuma) 1. Mashimba, 2. Kalemani. 3. Dotto 4. Ngusa 5. Prof Makubi then kaweka waislam wenzake, kanda ya ziwa wakimchagua huyu maza watakuwa hawana akili
 
safi sn.
Dawa za kulevya kwa sasa zinauzwa kama njugu kama vile hakuna mamlaka ya kupambana na madawa ya kulevya.

Kwa sasa takwimu zinaonyeaha wauzaji na wasambazaji wameongezeka.
Kaji aliiweza sana ile nafasi lakini lile wimbi la 'mabadiriko' likamkumba.Akawekwa huyu naona maji yamezidi unga nae.Tumsubiri na Lyimo pia tuone atasurvive pale kwa muda gani.
 
Not necessarily, atapangiwa kazi nyingine!.

Ila pia ninanote demotions za kiaina!.

Mtu alikuwa KM, akapandishwa kuwa Kamishna, halafu sasa anashushwa na kuwa RAS!. It's not fair, kanuni za Utumishi wa umma zifuatwe. Ukimshusha mtu wa level ya PS, mtupe ubalozini!.

P
Nakubaliana na wewe
 
Not true. Waziri hawezi kumuagiza RC afanye kazi. RC ni mwakilishi wa Rais katika Mkoa na Waziri akiingia katika mkoa wake anatakiwa kwenda kusaini ofisini kwake.

RC ana mamlaka ya kumtia mtu ndani wakati waziri hana. RC atamuomba kitu waziri kwa sababu waziri anasimamia sekta husika na sio kwa sababu ni Boss wake.

RC akitaka barabara ijengwe mkoani mwake atawasiliana na waziri husika lakini haina maana kuwa yuko chini yake. RC na DC hawawajibiki kwa waziri wa Tamisemi. Mnakumbuka mara ngapi Jafo alikuwa anawalalamikia ma DC wakora bila matokeo yeyote. Lakini RC anaweza kumpa taabu DC.

Watu tunawaona mawaziri ni mabosi kwa sababu wanasimamia sekta fulani nchi nzima ( na hivyo kuwa na bajeti) na wamo katika Baraza la Mawaziri. Tunawadharau ma RC kwa sababu wanaishi sehemu kama Lindi na Mpanda. Makazi ya RC yanajulikana kama Ikulu ndogo na kama mkoa hauna makazi rasmi ya kufikia Rais huwa anafikia kwa RC.

Katibu Mkuu hivyo hivyo sio senior kwa RAS kwa sababu nilizozitaja hapo juu. Wote ni accounting officer. Katibu Mkuu anatamba kisekta lakini RAS kijiografia.

Amandla...
Kwa hiyo kwa kuwa mtendaji wa kijiji ana mamlaka ya kumtia mtu ndani basi ni mkubwa kuliko waziri?

RC ni mkuu wa ulinzi na usalama hivyo kumtia mtu ndani si ajabu. Waziri kwenda kusaini kwa RC ni utaratibu wa kumjulisha kwamba yupo mkoani ili aweze kutoa ulinzi lakini si kwamba wanalingana ki- seniority.

RC na DC wote ni wawakilishi wa Rais katika maeneo yao lakini hawako sawa ki- seniority.

RC hawezi kuomba barabara ijengwe sehemu fulani mkoani kwake kwa sababu hilo ni suala la kibajeti.

Kwa hiyo acha kupotosha waziri ni senior kwa RC.
 
Ngusa samike si alikua msemaji wa familia wakati wa msiba wa Magufuli. Au nafananisha??
 
Not necessarily, atapangiwa kazi nyingine!.

Ila pia ninanote demotions za kiaina!.

Mtu alikuwa KM, akapandishwa kuwa Kamishna, halafu sasa anashushwa na kuwa RAS!. It's not fair, kanuni za Utumishi wa umma zifuatwe. Ukimshusha mtu wa level ya PS, mtupe ubalozini!.

P
Mkuu kanuni za utumishi wa umma ni kama hazipo siku hizi. Mambo yanafanyika kienyeji tu..!
 
Not necessarily, atapangiwa kazi nyingine!.

Ila pia ninanote demotions za kiaina!.

Mtu alikuwa KM, akapandishwa kuwa Kamishna, halafu sasa anashushwa na kuwa RAS!. It's not fair, kanuni za Utumishi wa umma zifuatwe. Ukimshusha mtu wa level ya PS, mtupe ubalozini!.

P

Well said mkuu!

Maana inayumbisha issues za maslahi (benefits)
 
Not necessarily, atapangiwa kazi nyingine!.

Ila pia ninanote demotions za kiaina!.

Mtu alikuwa KM, akapandishwa kuwa Kamishna, halafu sasa anashushwa na kuwa RAS!. It's not fair, kanuni za Utumishi wa umma zifuatwe. Ukimshusha mtu wa level ya PS, mtupe ubalozini!.

P
Lakini KM na RAS si ni rank moja how come unasema ameshushwa?
 
Back
Top Bottom