Kinachoongelewa hapa ni chain of command kwenye Organisation Hierarchy, na si maslahi yanayotokana na nafasi ambayo kiongazi anakuwa amekasimishwa mamlaka na umma; kwamba kwenye chain of command, Waziri yuko juu na anaripoti kwa Rais wa nchi moja kwa moja wakati RC yuko chini ya Waziri na anaripoti kwa Waziri wa Tamisemi. Kwa hali hiyo Waziri ni mkubwa kwa RC.
Hata hivyo tukirudi kwenye upande mwingine wa maslahi ikiwa ni pamoja na autonomy, unaweza ukawa uko sawa. Tuseme kwa mfano, mimi hapa ukiniambia nichague kati ya Uwaziri na Ukuu wa Chuo Kikuu tuseme Mzumbe; uwezekano mkubwa ni kwamba nitachagua Ukuu wa Chuo Kikuu na si Uwaziri, kitendo ambacho kinaendana na idea yako hii ambayo umeiwasilisha hapa