Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Ningekuwa mmiliki wa gazeti kesho lingetoka hivi. "NDUNGAI MTU MZIMA HOVYO" by...
 
Sijaona sababu ya maneno yote haya yaliyomtoka mama, mtu ameomba msamaha tena hadharani lkn bado amemkalia kooni tu, mie sio mfuasi wa Ndugai lkn kikawaida mtu akiomba msamaha asamehewe, Samia alipaswa kutangaza msamaha ila kama kuna mengine waliapswa wayamalize ndani huko kwenye vikao vyao......
 
Reactions: nao
Sio lazima spika wa bunge awe kibaraka wa rais.
Nchi inaweza kusonga mbele vizuri kama bunge likiacha urafiki na serikali.
Bunge lipi unazungumzia? Tanzania kuna vikao vya CCM hakuna bunge nchi hii. Madhara ya kuuminya upinzani ndio haya sasa nyama zinatokea mbavuni.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ulifikiria kuwa kwa kuomba tu msamaha ule lingeweza kuisha?kwanza anasema kuwa hiyo clip ilitengenezwa!!tayari heshima yake ndio imeisha potea, na kuanzia hapa wale waliokuwa wameanza kumpogeza kwa kuomba msamaha, kwa msimamo huu wa leo wa mama, hutawasikia tena!!na sasa ameahakuwa mzee wa GUNDU!!mungu anatisha sana yaani ni huyu Ndugai ambaye miaka 6, nyuma alikuwa anajifanya ni mungu mtu??
 
Ndugai sio serikali kaka
Mama anapaswa kuwa na kifua na sio mtu mmoja anamkimbiza hivi
Inavoonekana yawezekana hata alilolifanya leo haikuwa kwenye ratiba zake

Kaitisha ili tuu kumjibu ndugai.
Anapotaka kumwadhibu ndugai aangalie asije kimbiza mwizi wa mitego akaacha mlango wazi

Najua anatambua kabisa ccm ishakuwa chakavu ndio maana haya yanatokea
Asilimia kubwa ya walio mzunguka wote ni wachumia tumbo na wanafiki. Asifikiri katika uadui wa mmoja tuu
 
Hii nafikiri hufanywa kuwatisha wengine wasijaribu kufanya Ndugai
 
Reactions: ram
Masikini unaepukaje aibu?
Kipi bora…kukosa kabisa madarasa na tundu la choo au kuwa nayo kwa pesa za kukopa?

Bora kujenga sisi wenyewe. Sio gharama kubwa kivile. Tukiamua, tunaweza Itasaidia kulipa Mshahara wako na wapambe wenzako gharama tutakazoziokoa.
 
Tatizo ni kwamba mama mwenyewe hii inshu imekuwa ya kushtukizwa na yeye

Wakati anakimbia alijua yuko nao kumbe wamesimama wanamwangalia tuu

Hajui nyuma ya ndugai kuna kina nani

Asifikiri vita ya siasa za ndani ya chama ni maneno.
Akataka kujisahau na kumshikia kiuono aseee yani alitoka kabisa kwenye mudi


Hapo ndio Ndugai ajue nguvu ya bunge, serikali inaliogopa bunge siku zote
 
sina mahaba na ndugai wala ccm.

ila usimlaumu kwa kukurupuka kwake kuomba msamaha.

pressure kutoka ndani ya ccm ilikuwa kubwa sana na jamaa akawa hana namna. alibanwa kwenye crempu.

na ukute hata kundi lililokuwa nyuma yake lilimuacha apambane kivyake.

shida ni kwamba amemuomba msamaha mwanamke, mbaya zaidi ni mwanamke mwenye asili ya pwani. wanawake wa pwani na vichambo ni pete na kidole.

kichambo alichopewa leo sidhani kama alikitarajia. angalau leo yale maccm yenye tamaa ya kiti cha urais, yamejua rangi halisi ya mama.
 
Hamna nyoka unatakiwa kumponda kichwani ukipiga kiunoni ukajidanganya kafa akikuvizia anakumaliza, hapa wanajaribu kumwekea mama mazingira magumu 2025 sasa kashtuliwa mapema acha awamalize tuu kila mbuzi ale urefu wa kamba yake.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hii nafikiri hufanywa kuwatisha wengine wasijaribu kufanya Ndugai
Ukumbuke vita ya siasa za kugeukana ni kama vita ya magenge ya uhalifu? Wani misitike minzi dethi

Sasa hapa aone tuu namna waliomzunguka ambao wako nyuma ya ndugai ni akina nani?
 
Kassim majaliwa na ndungai wamepewa ujumbe kuwa wanatakiwa wajiuzulu.

Vita ya 2025 imeipasua CCM vipande-vipande.

Pambaf.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…