Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

Rais Samia amvaa Ndugai. Asema, "Huwezi kuamini mtu mzima ana-argue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3"

TOZO siyo kwa matumizi walioyasema bali ni za kulipia hayo matrilioni plus interest of course.
Yaani mkuu umenivuruga balaa...! Sasa kama Tozo inaweza kulipa deni halisi na interest yake juu, kwa nini tukakope!!
 
Katika Mikopo yote tuliyowahi kuchukua …huu wa 1.3 trillion ndio una uwazi zaid-Jemedari Job Ndugai 3rd Jan,2022
Ni aibu kuishi kwa mikopo,Unakopa kujenje tundu la choo, Madarasa? Tunaweza na Tutajenga bila mikopo.
 
Masikini unaepukaje aibu?
Kipi bora…kukosa kabisa madarasa na tundu la choo au kuwa nayo kwa pesa za kukopa?
Ni aibu kuishi kwa mikopo,Unakopa kujenje tundu la choo, Madarasa? Tunaweza na Tutajenga bila mikopo.
 
Mama leo amepiga kwenye mshono.
Ndugai leo 'kavuliwa nguo' na jana alijisahau 'akavua nguo yake ya ndani', sasa leo hana nguo kabisa!!!
Kwa hiyo jana alitoa Pichu akabaki na kanzu...mama kalitoa na kanzu lenyewe😁😁😁
 
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni Uhuru wa Mtu kusema chochote, lakini inashangaza Mtu anayetegemewa kushirikiana na Serikali kwenye safari ya maendeleo 'kuargue' kuhusu Tozo na Mkopo wa Trilioni 1.3 kwasababu taarifa zote za Uchumi zinapita kwake akisema, "Ni homa (fever) ya 2025, wasameheni"

Ameongeza, "Huwezi kuamini mtu mzima na unaenda kuargue tozo na mkopo wa Trilioni 1.3 kama kwamba ndio kwamba inatokea Tanzania wakati toka tunapata Uhuru ni Mikopo kwenda mbele. Na katika Mikopo yote huu ni mkopo mzuri zaidi"
Kaongea Utopolo hadi aibu tuna head of state infant kwa hali hii ni hatari sana, anapelekeshwa ataweza siasa n.a. mihadhara Huyu? CCM tutaumbuka
 
Mwanzoni kabisa niliwasikia watu wakisema bunge ni dhaifu.


Spika kaongea kidogo tu watu wamemvaa tena.


Kwahiyo mnataka nini??


Halafu suala la Rais wa nchi kuendelea na hili suala la mikopo ni ufinyu wa akili.

Mtu ameshaomba radhi.

Yeye bado kashikilia bango.

Poor thinking capacity.
Legacyyy
 
Ndugai alitakiwa kubaki na msimamo wake, kama kuvurugana wavurugane kila mmoja aoneshe makali kwa nafasi yake aliyopi

Naungana na wewe ; kafanya kosa kubwa snaa kuomba msamaha. Alitakiwa akae kimya asi comment chochote .

Angeonekana mwanaume zaidi . Kuomba msamaha means he is dumb na Hana stand, damn it.

Mwanaume kujiamini na ametoa mawazo yake huru ambayo yalikuwa ni mazuri Tu; hii Mikopo ni ya kipuuzi maana asilimia kubwa ya hii mikopo huliwa kifisadi na Hiyo ni report ya SHIRIKA LA FEDHA LA DUNIA.

Sasa yeye angebaki hapo hapo ; kuwa kama tumekopa , tozo ishushwe zaidi .

Samia Mwenyewe na kundi lake ni fisadi tu na ni Upenyo wa rushwa, unamuomba Samahani ya Nini , kwani yeye nani , atatoka kwenye kiti kama walivyotoka wengine , I can’t pleading for my thoughts and stand , ni upumbavu

Kuweka tozo ni failure ya mama , mbona tuliishi na Ngosha bila tozo

Job sio mwanaume yule , coward , mwanaume misimamo kwa unachoamini , na mwanaume hueshimika kwa misimamo yake. Ndio maana JPM ni rais bora wa maisha.

TISS wamemshauri kuomba msamaha na yeye kaomba kweli , leo mama kamtia kidole cha nyuma na msamaha wake. Haya ndio madhara ya kukosa stand. Mwanaume kujiamini hata ukibaki alone kwenye mawazo yako, poa tu ; ipo siku some people will understand you !

Maana mm najiuliza kaomba msamaha kwa kosa gani? Africa bwana

Yaani ukitoa mawazo yako kinzani, ni kosa Dah

Pole ndungai, kumbe we lofa tu
Nimekudharau sana
 
Wanawake wanajua sana kumchamba mtu, ndio hapo wanapopata huruma kwa watu..ila uhalisia unabaki vile vile
 
Kutokana na kuwaza zaidi kuhusu 2025 na matarajio yake kupotea Ndugai amejiweka pabaya huenda hata bunge likamwondoa maana amekuwa wazi kabisaa kuonesha dharau kubwa Sana kwa Mh Rais niliwahi kuleta post hapa huyu ndugai anakilichojificha mbeleni hakuamini iKama ile IWE ISIWE NA KUPORA PESA ZA MATIBABU YA LISSU KUNA SIKU MUNGU ASIYELALA ATARUDISHA TUU NA HUU NDIO WAKATI WA NDUGAI KUWAMBWA MSALABANI yeye alitibiwa kwa zaidi Billion 2 hakuona mwenzake kuwa anahitaji matatibabu hayo halafu na mwendazake akashangilia wote hawa Mungu amewaandalia fungu mahali pao hakuna rangi hawataona wakati wa Mungu ukifika

Si kuwa tunapaswa kuwa na mkakati wa vita badala ya ushabiki tu?

1. Minyukano ndani ya CCM haitusaidii kupata katiba mpya.
2. Kuwa na agenda za kudumu si maadui.
3. Makando kando yao tukashughulika nayo baada ya katiba mpya kwenye "haki na maridhiano."

Huoni hiyo itatusaidia kupiga hatua mbele ndugu mjumbe?
 
vile mwanaume ukingia katika vita ya maneno na mwanamke. pole sana ndugai. umepata ulichostahili.
giphy.gif
 
Iko hivyo.

Ukijishusha kuomba msamaha hadharani halafu uliyemkosea anaibuka na chembe kidevu lazima ujione BOYA.

Hako kajamaa kanafiki mno nasikia kana hadi Kinga dhidi ya mashtaka.

Kama vipi wakaondolee.
 
Msamaha alio omba SPIKA ni msamaha wa kinafiki kila mtu mwenye AKILI amelijua hilo ukitizama ile body language ya spika alivyo kuwa anaongea tu utafahamu hakuwa ana omba msamaha bali alikuwa ana igiza ....... ukiachana na msamaha ulio ombwa na Spika pia SPIKA amefanya makosa makubwa sn kutokana na NATURE YA UTAWALA WA TANZANIA ULIVYO TENGENEZWA.lugha rahisi naweza kusema SPIKA hakuwa na HEKIMA wala BUSURA sasa apambane na hali yake asipo angalia anaweza hata kusimamishwa UWANACHAMA wa CCM.

Sent from my SM-G975F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom