Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Tangu nianze kufuatilia siass za nchi hii, sijawahi ona kiongozi wa CCM alie madarakani akikataliwa, kupingwa na kuongezewa vivyo sivyo kama Mama yetu wa leo.

Kwanini hali hii?

1. Mama kulinganishwa na Mwendazake

Mama kulinganishwa na Mwendazake na hapa ndipo hata baadhi ya wana-CCM wanapoungana na watanzania wengine kumuhukumu na kumuona hatoshi na wanaona ni bora 2025 watafute mgombea mwingine vinginevyo ni bora wachague mpinzani.

Kwanini Mwendazake anamgharimu?
Wakati wa Mwendazake, kuna kundi kubwa la watanzania waliamini wizi na ufisadi vilikuwa vimekomeshwa/ vimedhibitiwa jambo ambalo halikuwa kweli kwa asilimia 100.

Mwendazake alidhibiti vyombo vya habar, alidhibiti Bunge, mitandao na vyanzo vingine vya kupashana habari matokeo yske tuhuma za wizi na ufisadi Wakati wa Mwendazake havikupata nafasi.

Kingine ni Mwendazake kutumia media kuendesha propaganda za kumsifu na kumtukuza mambo ambayo sasa hayapo kwa kiwango kile na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimtazamo kati ya Mama na Mwendazake.

2. Kundi la Sukuma gang
Hili kundi ni kundi la watu wanaonekana kuwa na chuki dhidi ya huyu Mama na ndio wanachangia sana kuonyesha kuwa Mama hatoshi sababu tu hawampendi. Ni kama hawakuta Mama amrithi Mwendazake na hivyo kutumia madhaifu ya Mama kummaliza kisiasa mbele ya umma.

Na kama Mama angeshindwa kuendeleza miradi iliyoachwa na Mwendazake, basi hili kundi lingepata cha kusema na lingekuwa kinara katika kuwaongoza watu wamkatae Mama hiyo 2025.

Mama akijitahidi kukamilisha Miradi yote iliyoachwa na Mwendazake, basi atafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu za hili kundi mitandaoni na kwingineko

3. Madai kuwa Mzee wa Msoga ana influence katika uongozi wake
Madai haya ni moja ya mambo ambayo yanamgharimu sana Mama hasa ikizingatiwa Mzee wa Msoga anachukuliwa kama mtu alieacha rushwa na ufisadi vikatamalaki sana katika nchi hii.

Hivyo, madai kuwa Mama anafanya baahi ya mambo kwa influence ya Mzee wa Msoga, madai haya yanamgharimu sana kisiasa na 2025 atakuja kuona matokeo yake.

4. Madhaifu binafsi ya Mama
Madhaifu au mapungu haya ni pamoja na haya na kukithiri kwa tozo katika awamu yake, kauli za kuruhusu watu wale kulingana na urefu wa kamba zao, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kuhamisha wamasai kule Loliondo, safari za mara kwa mara nje ya nchi, kauli zake za majukwaani na mambo mengineyo.

5. Jinsia yake
Ukweli mwingine unatokana na mila na desturi zetu plus mtazamo potofu wa jumla kwa baadhi ya watu kuwa Mwanamke hafai kushika nafasi kama hio hivyo ni bora wakati ukifika, tumuweke mtu mwingine

6. Wanawake kutopendana

Madai kuwa wanawake huwa hawapendani, yanaweza kuchangia anguko la Mama na Wanawake wengi kwa sasa ni miongoni mwa watanzania wanaomuo Mama hatoshi.

Hivyo, kwa ujumla hayo ndio mambo yanayomgharimu Mama kwa sasa na ndio yatamgharimu vibaya sana 2025 na anaweza asipate hata asilimia 30 ya kura zote.

Ukitaka kuamini haya nayosema juu ya kukubalika au kutokubalika kwa Mama, fanya tu kautafiti kasiko rasimi kwa kuhoji tu watu mbalimbali utagundua wengi wanampinga na kutorodhishwa na uongozi wake wakiwemo hata watu wa chama chake.

Hivyo, wapinzani wakijipanga vizuri 2025 na tukawa na Tume Huru, basi uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi ni mkubwa mno kuanzia kwenye uraisi mpaka ubunge.
 
Badili kichwa cha habari kwanza ili uzi wako uwe na maana kwa msomaji. Mama anatekeleza miradi huko mikoani.

Nasikitika kukwambia kwamba hao wanaopata madarasa mapya hawasomi uzi kama wa kwako. Hawa wanaopata umeme huko vijijini ndani ya muda huu hawana muda wa siasa za maji taka kama hizi.

Kuna watu wanaguswa moja kwa moja maisha yao, hao hawana muda wa kusoma ulichoandika achilia mbali kuwa na muda wa kukitafsiri kwa kina.
 
Juzi tuu hapa geita alipokuja kinana walimwambiaa kabsa samia hapendwi, mwanzoni kabsa mwa mwaka huu alikuja putin shaka akasema samia mitano tena wananzengo tena akina mama a ccm wakasema NDOHOOOOO nilishangaa sana
SSH anaweza kuchukiwa kwa sababu ya jinsia yake lakini hana tofauti na JPM tena yeye anakwenda mbali zaidi kwa kuwa karibu na dunia nzima kwa ujumla.

Huku Dar wale wapangaji wa kwenye majengo ya Masaki na maeneo mengine wameshaanza kurudi maana yake upo mzunguko wa pesa kwa sasa.

Hao kina mama wa vijijini wenye nongwa za yule jamaa yao aliyekuwa akichanganya lugha majukwaani na wanamuelewa na kucheka wanajitafutia tu maumivu ya mioyo na kununa kusiko na sababu.
 
Atapita kwa tabu ccm
IMG_20221006_221309.jpg


Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Mawazo kama haya ndio yalinifanya niache kujishughulisha na upinzani

2020 niliwaambia wagomee uchaguzi kutokana na mazingira yalivyokuwa ama wataishia kuumizwa bure na kupoteza fedha, ila wengi walikuwa na mawazo kama haya na matusi juu

Kilichowakuta hadi leo bado wapo mahakamani kutumia fedha na muda zaidi kufukuzwa wabunge 19
Unahitaji uvumilivu sana kuongozwa na watu wenye akili fupi kiasi hiki
 
Tangu nianze kufuatilia siass za nchi hii, sijawahi ona kiongozi wa CCM alie madarakani akikataliwa, kupingwa na kuongezewa vivyo sivyo kama Mama yetu wa leo...
Unatafutwa na Wasiojulikana kutoka kwa TULIA, Hajatulia!
 
Happy kwenye utafiti, ni kwamba watanzania wengi wanataka mabadiliko anzia kipindi Cha Mrema wa NCCR.

Watu wengi wa CCM hakipendi hicho chama kwa sababu walishagundua wamegawanjwa kimakundi. Kuna kundi la high table hili ni kwa ajili ya uongozi, kundi la wapambe na kundi la mavazi. Hili kundi la vitenge, kofia, kanga na matisheti ndio ukiongea utapata ukweli kuwa wapo ili kubahatisha bahati lakini chama hakipo rohoni.

Samia ni ngumu kutoboa kwa sababu malengo yao yanafeli wakati wengine wananeemeka.
 
Umeandika 2020, ilishapita.
 
Kwenye mazingira haya ya kisiasa, Katiba iliyopo, na Tume ya uchaguzi, sitashangaa kama akigombea akashinda, regardless ya hali ya kisiasa aliyonayo.

Kikwete 2010 ilikuwa almost hivi hivi, nchi iliongozwa kwa "auto pilot" muda mrefu, kila mtu kujichumia, akachokwa haswa, lakini tulipokwenda kwenye uchaguzi, akashinda, hata kama alishinda kwa wizi.
 
Badili kichwa cha habari kwanza ili uzi wako uwe na maana kwa msomaji. Mama anatekeleza miradi huko mikoan...
Mzee upo Tanzania hiihii au ndio kujitoa ufahamu kwasababu unatumia Phillipo Bukililo unaamini kabisa kwamba jina lako litaonekana somewhere!?

Maana nashindwa kukuelewa!!??...Jamaa ameongea point zilizopo kabisa na mtaani hali halisi ndio hiyo au mwenzetu sio mtz?!?.

Ni kweli kabisa Samia kuna mambo mazuri kafanya(anafanya) na anajitahidi kwa kiasi chake ila kwa sababu zilizotajwa na muanzisha thread ni kweli kabisa zinamfanya achukiwe.

Njoo mtaani huku uone watu wanavyomuongelea kiufupi hawamuelewi kabisa nenda hata facebook upate maoni ya raia kiukweli watu wamekataa kabisa kumuelewa na yeye anajua hilo pamoja na kwamba kajenga madarasa na blahblah kibao ila watu HAWAMUELEWI
 
Back
Top Bottom