Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

BAVICHA mnatumia akili kweli? Kwa hyo mnategemea mabadiliko kwa tume hii ya Uchaguzi? Kwa katiba hii?
 
Juzi tu hapa geita alipokuja kinana walimwambiaa kabsa samia hapendwi, mwanzoni kabsa mwa mwaka huu alikuja putin shaka akasema samia mitano tena wananzengo tena akina mama a ccm wakasema NDOHOOOOO nilishangaa sana.
Ni nadra sana makamu anayerithi kiti cha urais kushinda uchaguzi unaofuata. Mifano ipi kibao
 
Yani wanaccm wameshiba ulaji harafu wawape ulaji chedema
 
2025 CDM inapaswa kugombea bila kujali kuna katiba mpya au tume huru ya uchaguzi
 
Hakuna cha habari nyingine wala nini... CCM kushinda ni lazima
Yaliyotokea 2020 ndo ilikuwa uthibitisho kuwa CCM ndo waizi wa SANDUKU la KURA Nchi nzima.

Wananchi hawaliamini tena SANDUKU la kura kama njia ya HAKI kuwapata viongozi wawatakao.

Bila TUME huru ya UCHAGUZI na KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA,

Hapatakuwa na UCHAGUZI wowote.

Amen, Amen, Amen.
 
Mitano tena kwa samia, kura zikipelea tunajazilizia za maruhani.
 
Tangu nianze kufuatilia siass za nchi hii, sijawahi ona kiongozi wa CCM alie madarakani akikataliwa, kupingwa na kuongezewa vivyo sivyo kama Mama yetu wa leo.

Kwanini hali hii?

1. Mama kulinganishwa na Mwendazake

Mama kulinganishwa na Mwendazake na hapa ndipo hata baadhi ya wana-CCM wanapoungana na watanzania wengine kumuhukumu na kumuona hatoshi na wanaona ni bora 2025 watafute mgombea mwingine vinginevyo ni bora wachague mpinzani.

Kwanini Mwendazake anamgharimu?
Wakati wa Mwendazake, kuna kundi kubwa la watanzania waliamini wizi na ufisadi vilikuwa vimekomeshwa/ vimedhibitiwa jambo ambalo halikuwa kweli kwa asilimia 100.

Mwendazake alidhibiti vyombo vya habar, alidhibiti Bunge, mitandao na vyanzo vingine vya kupashana habari matokeo yske tuhuma za wizi na ufisadi Wakati wa Mwendazake havikupata nafasi.

Kingine ni Mwendazake kutumia media kuendesha propaganda za kumsifu na kumtukuza mambo ambayo sasa hayapo kwa kiwango kile na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimtazamo kati ya Mama na Mwendazake.

2. Kundi la Sukuma gang
Hili kundi ni kundi la watu wanaonekana kuwa na chuki dhidi ya huyu Mama na ndio wanachangia sana kuonyesha kuwa Mama hatoshi sababu tu hawampendi. Ni kama hawakuta Mama amridhi Mwendazake na hivyo kutumia madhaifu ya Mama kummaliza kisiasa mbele ya umma.

Na kama Mama angeshindwa kuendeleza miradi iliyoachwa na Mwendazake, basi hili kundi lingepata cha kusema na lingekuwa kinara katika kuwaongoza watu wamkatae Mama hiyo 2025.

Mama akijitahidi kukamilisha Miradi yote iliyoachwa na Mwendazake, basi atafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu za hili kundi mitandaoni na kwingineko

3. Madai kuwa Mzee wa Msoga ana influence katika uongozi wake
Madai haya ni moja ya mambo ambayo yanamgharimu sana Mama hasa ikizingatiwa Mzee wa Msoga anachukuliwa kama mtu alieacha rushwa na ufisadi vikatamalaki sana katika nchi hii.

Hivyo, madai kuwa Mama anafanya baahi ya mambo kwa influence ya Mzee wa Msoga, madai haya yanamgharimu sana kisiasa na 2025 atakuja kuona matokeo yake.

4. Madhaifu binafsi ya Mama
Madhaifu haya ni kama kukidhiri kwa tozo katika awamu yake, kauli za kuruhusu watu wale kulingana na urefu wa kamba zao, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kuhamisha wamasai kule Loliondo, safari za mara kwa mara nje ya nchi, kauli zake za majukwaani na mambo mengineyo.

5. Jinsia yake
Ukweli mwingine unatokana na mila na desturi zetu plus mtazamo potofu wa jumla kwa baadhi ya watu kuwa Mwanamke hafai kushika nafasi kama hio hivyo ni bora wakati ukifika, tumuweke mtu mwingine

6. Wanawake kutopendana
Madai kuwa wanawake huwa hawapendani, yanaweza kuchangia anguko la Mama na Wanawake wengi kwa sasa ni miongoni mwa watanzania wanaomuo Mama hatoshi.

Hivyo, kwa ujumla hayo ndio mambo yanayomgharimu Mama kwa sasa na ndio yatamgharimu vibaya sana 2025 na anaweza asipate hata asilimia 30 ya kura zote.

Ukitaka kuamini haya nayosema juu ya kukubalika au kutokubalika kwa Mama, fanya tu kautafiti kasiko rasimi kwa kuhoji tu watu mbalimbali utagundua wengi wanampinga na kutorodhishwa na uongozi wake wakiwemo hata watu wa chama chake.

Hivyo, wapinzani wakijipanga vizuri 2025 na tukawa na Tume Huru, basi uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi ni mkubwa mno kuanzia kwenye uraisi mpaka ubunge.
Kwa mwenye akili timamu akisoma huu uzi anaona wazi kabisa umeweka deathwish kwa wanaompinga mama kwa sababu umeweka vigezo vinavyotabainisha hao ndiyo sababu halisi kwa nini mama hakubaliki.

Kikubwa elewa kwamba mama hakubaliki sana kwakuwa mpaka leo tija haionekani kwenye legacy yake.

Anakumbatia old politicians ambao ni kama anawafuta jasho kwenye teuzi zake. Kuruhusu ufisadi wa kutisha kama kifutajasho kwa waliokwapuliwa na serikali. Pia kuamu kuwazibia watu wa hali ya chini hasa wajasiriamali kufanya uchuuzi mdogo mdogo....

Kiufupi wewe ni mchonganishi
 
2025 CDM inapaswa kugombea bila kujali kuna katiba mpya au tume huru ya uchaguzi
CDM haitoshiriki Uchaguzi wowote, amueni kukubali Takwa la KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi,

Au tukubali kulala saa 12, maana tutakuwa tumekataa wenyewe kuheshimu matakwa na Utaratibu tuliojiwekea.

Policeee mnaowaaminia na wajeda ni ndugu, kaka na dada zetu, WATAKATAA kuwatii na hamtoamini.

Ameeeen.
 
BAVICHA mnatumia akili kweli? Kwa hyo mnategemea mabadiliko kwa tume hii ya Uchaguzi? Kwa katiba hii?
Tutapata KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA,

Hlyo ndo itazaa Tume huru ya Uchaguzi.
Pia elewa bavicha ni tone tu kati ya mamilioni ya Watanzania wanaodai KATIBA mpya.

So rudia tena kufanya calculation.

Ameeeen.
 
Juzi tu hapa geita alipokuja kinana walimwambiaa kabsa samia hapendwi, mwanzoni kabsa mwa mwaka huu alikuja putin shaka akasema samia mitano tena wananzengo tena akina mama a ccm wakasema NDOHOOOOO nilishangaa sana.
Ukizungumzia geita ni unazungumzia ndugu wa marehemu
 
Tangu nianze kufuatilia siass za nchi hii, sijawahi ona kiongozi wa CCM alie madarakani akikataliwa, kupingwa na kuongezewa vivyo sivyo kama Mama yetu wa leo.

Kwanini hali hii?

1. Mama kulinganishwa na Mwendazake

Mama kulinganishwa na Mwendazake na hapa ndipo hata baadhi ya wana-CCM wanapoungana na watanzania wengine kumuhukumu na kumuona hatoshi na wanaona ni bora 2025 watafute mgombea mwingine vinginevyo ni bora wachague mpinzani.

Kwanini Mwendazake anamgharimu?
Wakati wa Mwendazake, kuna kundi kubwa la watanzania waliamini wizi na ufisadi vilikuwa vimekomeshwa/ vimedhibitiwa jambo ambalo halikuwa kweli kwa asilimia 100.

Mwendazake alidhibiti vyombo vya habar, alidhibiti Bunge, mitandao na vyanzo vingine vya kupashana habari matokeo yske tuhuma za wizi na ufisadi Wakati wa Mwendazake havikupata nafasi.

Kingine ni Mwendazake kutumia media kuendesha propaganda za kumsifu na kumtukuza mambo ambayo sasa hayapo kwa kiwango kile na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimtazamo kati ya Mama na Mwendazake.

2. Kundi la Sukuma gang
Hili kundi ni kundi la watu wanaonekana kuwa na chuki dhidi ya huyu Mama na ndio wanachangia sana kuonyesha kuwa Mama hatoshi sababu tu hawampendi. Ni kama hawakuta Mama amrithi Mwendazake na hivyo kutumia madhaifu ya Mama kummaliza kisiasa mbele ya umma.

Na kama Mama angeshindwa kuendeleza miradi iliyoachwa na Mwendazake, basi hili kundi lingepata cha kusema na lingekuwa kinara katika kuwaongoza watu wamkatae Mama hiyo 2025.

Mama akijitahidi kukamilisha Miradi yote iliyoachwa na Mwendazake, basi atafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu za hili kundi mitandaoni na kwingineko

3. Madai kuwa Mzee wa Msoga ana influence katika uongozi wake
Madai haya ni moja ya mambo ambayo yanamgharimu sana Mama hasa ikizingatiwa Mzee wa Msoga anachukuliwa kama mtu alieacha rushwa na ufisadi vikatamalaki sana katika nchi hii.

Hivyo, madai kuwa Mama anafanya baahi ya mambo kwa influence ya Mzee wa Msoga, madai haya yanamgharimu sana kisiasa na 2025 atakuja kuona matokeo yake.

4. Madhaifu binafsi ya Mama
Madhaifu haya ni kama kukidhiri kwa tozo katika awamu yake, kauli za kuruhusu watu wale kulingana na urefu wa kamba zao, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kuhamisha wamasai kule Loliondo, safari za mara kwa mara nje ya nchi, kauli zake za majukwaani na mambo mengineyo.

5. Jinsia yake
Ukweli mwingine unatokana na mila na desturi zetu plus mtazamo potofu wa jumla kwa baadhi ya watu kuwa Mwanamke hafai kushika nafasi kama hio hivyo ni bora wakati ukifika, tumuweke mtu mwingine

6. Wanawake kutopendana
Madai kuwa wanawake huwa hawapendani, yanaweza kuchangia anguko la Mama na Wanawake wengi kwa sasa ni miongoni mwa watanzania wanaomuo Mama hatoshi.

Hivyo, kwa ujumla hayo ndio mambo yanayomgharimu Mama kwa sasa na ndio yatamgharimu vibaya sana 2025 na anaweza asipate hata asilimia 30 ya kura zote.

Ukitaka kuamini haya nayosema juu ya kukubalika au kutokubalika kwa Mama, fanya tu kautafiti kasiko rasimi kwa kuhoji tu watu mbalimbali utagundua wengi wanampinga na kutorodhishwa na uongozi wake wakiwemo hata watu wa chama chake.

Hivyo, wapinzani wakijipanga vizuri 2025 na tukawa na Tume Huru, basi uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi ni mkubwa mno kuanzia kwenye uraisi mpaka ubunge.
Chadema wamekunulia laptop, naona unapangilia maandiko vizuri.
 
Kwa mwenye akili timamu akisoma huu uzi anaona wazi kabisa umeweka deathwish kwa wanaompinga mama kwa sababu umeweka vigezo vinavyotabainisha hao ndiyo sababu halisi kwa nini mama hakubaliki.

Kikubwa elewa kwamba mama hakubaliki sana kwakuwa mpaka leo tija haionekani kwenye legacy yake.

Anakumbatia old politicians ambao ni kama anawafuta jasho kwenye teuzi zake. Kuruhusu ufisadi wa kutisha kama kifutajasho kwa waliokwapuliwa na serikali. Pia kuamu kuwazibia watu wa hali ya chini hasa wajasiriamali kufanya uchuuzi mdogo mdogo....

Kiufupi wewe ni mchonganishi
Na wewe ni mnafiki.
 
Juzi kati, nilisafiri toka Kyela kwenda Zanzibar via Dar, ulikuwa usafiri maalum, abiria sio zaidi ya 30.

Baada ya Konyagi kadhaa, huku safari ikiendelea mjadala wa siasa ukaanza! Zaidi ulikuwa ukilinganisha awamu ya tano na ya sita.

Wengi wa abiria walisimama na hoja ya kuwa awamu ya tano yapo ilikuwa fupi ilikuwa ni bora zaidi kuliko awamu zote.

Binafsi nikahoji ni ubora gani ambao wana zungumzia. Wengi wao wakaanza kutaja miuondo mbinu kadha wa kadha na wengine wakasema juu ya kudhibitiwa kwa ufisadi na rushwa.... uwajibikaki wa watendaji serikali na mengi kama hayo....

Nikauliza katika miradi hiyo ya kimkakati ni upi uliokwama ama kufutwa kabisa? Sikupata jibu la moja kwa moja, zaidi ya kusema pengine sasa ingekuwa imekwisha kamilika. Nikahoji juu ya ufahamu wao katika eneo hili, sikupata jibu sahihi au la moja kwa moja zaidi ya walivyosema awali.

Nikauliza tena juu ya ufisadi na rushwa. Je kuna ufisadi gani unaoendelea sasa na vipi kiwango cha rushwa katika awamu hii? Hapakuwa na jibu la moja kwa moja, zaidi ya kelele kwamba watu sasa wanafisadi zaidi kuliko awamu iliyopita. Nikawakumbusha kuwa tukiwa njiani kwenda Kyela na tulipofika Iringa tuliamriwa kulala hapo kwani muda wa kusafiri ulikuwa umekwisha. Ni hao hao walioanza kuwashawishi Polisi waturuhusu kwani tuna safari muhimu na maalum. Wengine wakapiga hata simu makao makuu ya jeshi la Polisi ili tu tuweze kuendelea na safari yetu!
Je hiyo haikuwa kutaka rushwa? Kwanini hatukutaka kufuata taratibu na sheria ya usafiri wakati wa usiku...! Sikupata jibu la moja kwa moja zaidi ya kelele tu! Huyu hatoboi 2025! Kwa nini hapana jibu!
 
Acheni kujifariji na kutafuta faraja kwa watu ambao walishawapuuza nyie wapinzani mliokosa Sera na ajenda na kubakisha ubabaishaji tu na kudandia vimatukio tu vya mpito Kama ukungu wa asubuhi, Nani mwenye Akili Timamu wakuweza kuwafikiria au kuwapigia kura nyie? Nani wakuwaunga mkono nyie upinzani? Kwa Sera na ajenda zipi mlizonazo? Kwa ushawishi gani mlio nao kwa watanzania? Hamuoni kuwa watanzania walishawapuuza na kuwadharau kwa Sasa? Hamuoni kuwa watanzania walishawatupa mkono? Hamuoni kuwa watanzania hawataki kuwasikiliza kwa lolote? Hamuoni hata namna ambavyo hamsikilizwi Wala kutiliwa maanani na watanzania kwa lolote mtakalo ongea na kuzungumza?

Nani awape nchi wasaliti wakubwa Kama nyie? Nani awaamini vigeu geu Kama nyie? Unazani watanzania wamesahau akili zenu za 2015? Nani awaamini watu Kama nyie wa upinzani mliokosa dira na muelekeo? Nani awape Imani watu Kama nyie ambao hamueleweki hata mnachosimamia? Nani awaamini nyie mliokosa mizizi ya kila kitu? Nani awaamini nyie mliokosa hata safu Bora ya uongozi wa kueleweka? Nani awaamini nyie ambao hata kuandaa mtu wa kugombea Urais mnasubili atoke kwetu CCM? Nani awaamini nyie mnaokosa hata uwezo wa kujiongoza na kujisimamia wenyewe?

Kwa Taarifa yako Ni kuwa Rais Samia Ndio chaguo la mamilioni ya watanzania, Ndio Tumaini la watanzania katika kuwaletea maendeleo, Rais Samia Ndio kiongozi aliyebeba Imani ya watanzania, Raisi Samia Ndio kiongozi anayekubalika na kuaminika na watanzania kwa matendo na kauli zake, Hakuna wa kumtikisa Wala kumyumbisha Rais Samia,

Naona mmeanza kupata kiwewe baada ya kuona Kiwango Cha kukubalika kwa Rais Samia kinazidi kuongezeka Zaid, mmepata kiwewe baada ya kugundua kuwa makundi yote yanamkubali na kumuunga mkono Rais Samia, mnataka kujaribu kutuchonganisha CCM ili mpate kupumua, lakini kwa Taarifa yenu Ni kuwa CCM Ni moja, wanaccm ni wamoja, wanachama Ni wamoja na sote tupo pamoja chini ya Mwenyekiti wetu na Rais wetu mh mama Samia suluhu Hassani

Kazi iendeleee Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
 
Tangu nianze kufuatilia siass za nchi hii, sijawahi ona kiongozi wa CCM alie madarakani akikataliwa, kupingwa na kuongezewa vivyo sivyo kama Mama yetu wa leo.

Kwanini hali hii?

1. Mama kulinganishwa na Mwendazake

Mama kulinganishwa na Mwendazake na hapa ndipo hata baadhi ya wana-CCM wanapoungana na watanzania wengine kumuhukumu na kumuona hatoshi na wanaona ni bora 2025 watafute mgombea mwingine vinginevyo ni bora wachague mpinzani.

Kwanini Mwendazake anamgharimu?
Wakati wa Mwendazake, kuna kundi kubwa la watanzania waliamini wizi na ufisadi vilikuwa vimekomeshwa/ vimedhibitiwa jambo ambalo halikuwa kweli kwa asilimia 100.

Mwendazake alidhibiti vyombo vya habar, alidhibiti Bunge, mitandao na vyanzo vingine vya kupashana habari matokeo yske tuhuma za wizi na ufisadi Wakati wa Mwendazake havikupata nafasi.

Kingine ni Mwendazake kutumia media kuendesha propaganda za kumsifu na kumtukuza mambo ambayo sasa hayapo kwa kiwango kile na hivyo kuleta tofauti kubwa ya kimtazamo kati ya Mama na Mwendazake.

2. Kundi la Sukuma gang
Hili kundi ni kundi la watu wanaonekana kuwa na chuki dhidi ya huyu Mama na ndio wanachangia sana kuonyesha kuwa Mama hatoshi sababu tu hawampendi. Ni kama hawakuta Mama amrithi Mwendazake na hivyo kutumia madhaifu ya Mama kummaliza kisiasa mbele ya umma.

Na kama Mama angeshindwa kuendeleza miradi iliyoachwa na Mwendazake, basi hili kundi lingepata cha kusema na lingekuwa kinara katika kuwaongoza watu wamkatae Mama hiyo 2025.

Mama akijitahidi kukamilisha Miradi yote iliyoachwa na Mwendazake, basi atafanikiwa kwa kiasi kikubwa kupunguza nguvu za hili kundi mitandaoni na kwingineko

3. Madai kuwa Mzee wa Msoga ana influence katika uongozi wake
Madai haya ni moja ya mambo ambayo yanamgharimu sana Mama hasa ikizingatiwa Mzee wa Msoga anachukuliwa kama mtu alieacha rushwa na ufisadi vikatamalaki sana katika nchi hii.

Hivyo, madai kuwa Mama anafanya baahi ya mambo kwa influence ya Mzee wa Msoga, madai haya yanamgharimu sana kisiasa na 2025 atakuja kuona matokeo yake.

4. Madhaifu binafsi ya Mama
Madhaifu haya ni kama kukidhiri kwa tozo katika awamu yake, kauli za kuruhusu watu wale kulingana na urefu wa kamba zao, kushindwa kudhibiti mfumuko wa bei, kuhamisha wamasai kule Loliondo, safari za mara kwa mara nje ya nchi, kauli zake za majukwaani na mambo mengineyo.

5. Jinsia yake
Ukweli mwingine unatokana na mila na desturi zetu plus mtazamo potofu wa jumla kwa baadhi ya watu kuwa Mwanamke hafai kushika nafasi kama hio hivyo ni bora wakati ukifika, tumuweke mtu mwingine

6. Wanawake kutopendana
Madai kuwa wanawake huwa hawapendani, yanaweza kuchangia anguko la Mama na Wanawake wengi kwa sasa ni miongoni mwa watanzania wanaomuo Mama hatoshi.

Hivyo, kwa ujumla hayo ndio mambo yanayomgharimu Mama kwa sasa na ndio yatamgharimu vibaya sana 2025 na anaweza asipate hata asilimia 30 ya kura zote.

Ukitaka kuamini haya nayosema juu ya kukubalika au kutokubalika kwa Mama, fanya tu kautafiti kasiko rasimi kwa kuhoji tu watu mbalimbali utagundua wengi wanampinga na kutorodhishwa na uongozi wake wakiwemo hata watu wa chama chake.

Hivyo, wapinzani wakijipanga vizuri 2025 na tukawa na Tume Huru, basi uwezekano wa wapinzani kushinda uchaguzi ni mkubwa mno kuanzia kwenye uraisi mpaka ubunge.
Ccm watatumia goli la mkono
 
Back
Top Bottom