Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Mimi nilianza kuwashauri CDM wagomee uchaguzi 2015 Ili kushinikiza KATIBA mpya ipatikane kabla ya Kikwete kuondoka madarakani wakapuuza.

Enzi hizo walikuwa na wabunge wengi sana na nguvu kubwa,

Ukikaribia uchaguzi, wanasiasa Huwa wanakuwa kama wamerukwa na AKILI.

Wangesikiza ushauri, tusingekuwa hapa tulipo Leo kama TAIFA.
 
Kwa katiba hii, majungu yoyote, hila yoyote ni kujichosha kimwili.... as long as kaapa hakuna YEYOTE narudia tena HAKUNA YEYOTE wa kumgusa mama awe mwana CCM ama awe mpinzani ...as long as jeshi liko na yeye kaeni kimyaa.

Na ndiyo maana vyama vyenye akili linalijua hili na vimeanza kudai katiba mpya. Narudia tena hasa kwa wana CCM wenzangu msijichoshe kwa lolote, mnakumbuka kale kaundi ambako kiongozi wako aliangushiwa kitu kizito kichwani....? yupo wapi leo? ni mfano tu.
 
Wanasiasa wanajua wanachokifanya ndio kazi yao ila tatizo lipo kwa nyie wananchi, endeleeni kuwaamini na kuweka matumaini kwa hao wanasiasa.
 
Wanasiasa wanajua wanachokifanya ndio kazi yao ila tatizo lipo kwa nyie wananchi, endeleeni kuwaamini na kuwa kuweka matumaini kwa hao wanasiasa.
Time hii hawatoamini jinsi uchaguzi utakavyoyeyuka,

Wananchi wako makini kuliko wakati mwingine wowote.

Tusubiri.
 
nimepita kanda ya ziwa majuzi - Mwanza, Geita, Biharamulo, Kahama, Tabora, Shinyanga, Bukombe, Bukoba - aisee ni hali mbaya !! ila cha msingi nachotaka kusema ni kwamba kwa katiba hii narudia tena kwa katiba hii ndugu zangu majungu juu ya huyu mama ni kujichosha kiakili na kimwili.
 
5. Jinsia yake.

Hili nalo ni kujitetea tu, Jinsia Wala ht Si tatizo.

Pale Ethiopia ni JINSIA hiyo hiyo, mbona Yeye hakukimbilia Seat ya dirishani???

Alionyesha msimamo wote tumemkubali...
 
 
Mama anatosha mkifanya makosa mkampa nchi Wasukuma Kama Magufuli mtajuta!?
 
Ifike mahali tuache tabia mbaya ya kuwa tunawahujumu ma-Rais walioko madarakani kwa kudhani kuwa tumnamhujumu mtu kumbe tunaihujumu nchi!
 
Amridhi = amrithi, kukidhiri = kukithiri. Nakukumbusha tu kwama Mama Samia ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM ndo kateua wafuatao na anaweza akawapiga chini pia wakimzingua;
1. Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi.
2. Mkurugenzi wa uchaguzi.
3. Wakurugenzi wa wilaya (DED) ambao ndo wasimamizi wakuu wa uchaguzi kwenye wilaya.
4. IGP
5. Mkuu wa majeshi
6. Kamishna wa takukuru.
7. Gavana
8. Mkuu wa usalama wa taifa
9. Mkuu wa jeshi la magereza

Jiulize mpinzani atapenya vipi kwa hiyo nguvu ya kikatiba aliyo nayo mwenyekiti wa CCM? Penda usipende mgombea wa CCM hata angekuwa Gigy Money kushinda ni lazima.
 
Nini kifanyike kwa mtizamo wako?
 
5. Jinsia yake.

Hili nalo ni kujitetea tu, Jinsia Wala ht Si tatizo.

Pale Ethiopia ni JINSIA hiyo hiyo, mbona Yeye hakukimbilia Seat ya dirishani???

Alionyesha msimamo wote tumemkubali...
Alivyoanza mwanzo wenye jinsia na ya kwake walifurahi na kumpongeza ila sasa hali imebadilika tunasingizia tatizo jinsia.
 
Kama hayo ndo mawazo Yako, Pana haja Gani kufanya uchaguzi Kwa kutumia billions of money???

Kama unayosema ni Kweli, mbona Magu alikuwa anakata PUMZI, na kuweweseka muda wote wa kampeni.

Uchaguzi ni habari ingine, we isikie tu.
 
Kama hayo ndo mawazo Yako, Pana haja Gani kufanya uchaguzi Kwa kutumia billions of money???

Kama unayosema ni Kweli, mbona Magu alikuwa anakata PUMZI, na kuweweseka muda wote wa kampeni.

Uchaguzi ni habari ingine, we isikie tu.
Hakuna cha habari nyingine wala nini... CCM kushinda ni lazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…