Rais Samia ana hali mbaya kuelekea 2025, Wana-CCM wanatamani wapinzani wapewe nchi. Anaweza asipate hata 30% ya kura

Sasa Kinana huyo huyo eshajuwa njia nzuri zaidi za kuwabana wapinzani, nafuu hiyo ya kupata wabunge wengi itatoka wapi?
Kinana anazeeka sio yule wa zamani Uchaguzi ujao Wabunge 80 wa Chadema ni gerentii bro.
 
Chawa watu walishaamka muda mrefu, au unadhani matumizi ya vyombo vya dola yataendelea kuwa upande wenu kila siku? Machafuko tu ndio yatawaondoa madarakani nyie majizi ya kura.
Njoo ukichafue hapa kwangu
 
Ubaya au uzuri wa CCM hawa jamaa unaweza hisi hawapo hivi ila itapokuwa kurisk chama chao hio 2025 hutaamin watavyopambana kumuweka samia madarakani hata kwa bao la mkono
Pia upande wa Chadema bado naona wamelala na ukizingatia Mbowe anatoka 2024 bado simuoni mwanasiasa Wa kukimbiza CCM hii

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Hao watakuwa ni wabunge wasiotofautiana na wabunge wa CCM, ila kwa majina ya vyama vyao tu basi!
Watakuwa ni Wabunge machachari sana hili Bunge la Chama kimoko limezubaa sana.
 
Shortly hakubaliki ila upinzani wasahau kuchukua nchi
 
Mnyonge Mnyongeni ila SSH amefanya makubwa
1. Ajira.. sekata binafsi+ Serikalini zaidi ya Watu wenye sifa Laki 1 wameajiriwA... Certificate/ Diploma/ Graduate/ Postgraduate ( pitia ajira zetu/ Ajira portal 2020- 2022)
2. Elimu Bure std1 hadi F6
3. Zahanati ( Dispensary) + Vituo vya Afya ( Health Center) kwa kila kata+ Vijiji
4. Ukuaji wa Sekta ya Kilimo ( Ruzuku ya Pembejeo za Kilimo ( Mbegu+ mbolea) +masoko.. wakulima kuweza kuuza mazao ndani+ nje ya nchi bila kuingiliwa....
5. Ukuwaji wa sekta ya Utalii
 
Siku ukijua ukweli huu kuhusu uchaguzi hasa unaohusu mamlaka makubwa ya nchi hutapata tabu duniani kuhusu uchaguzi.

1:'The people who cast the votes don't decide an election, the people who count the votes do'. (Joseph Stalin)

2:'It is enough that the people know there was an election. '(Joseph Stalin)

Nb 1😀uniani kote kiongozi mkuu wa nchi huchaguliwa na kikundi kidogo sana cha watu(Elites).

Nb 2:Je, mimi na wewe tupo kwenye hilo kundi????

Nb 3: Mimi na wewe tunaingia kwenye msemo namba mbili hapo juu wa Joseph Stalin!!!!!!!
 
Hadithi hizo
 
5. Jinsia yake.

Hili nalo ni kujitetea tu, Jinsia Wala ht Si tatizo.

Pale Ethiopia ni JINSIA hiyo hiyo, mbona Yeye hakukimbilia Seat ya dirishani???

Alionyesha msimamo wote tumemkubali...
Dah
 
Tuendelee na matazamio walosema ni WA mpito tutarudi kuwauliza walitumia akili ipi na maandiko yapi, ila walimaanisha kweli. Wakati utaongea wenyewe
 
😅😅
 
Rais wa Ethiopia siyo mkuu wa serikali kikatiba bali ni mkuu wa nchi asiye na madaraka ya kuteua au kuunda serikali.

Huwezi kulinganisha rais wa Ethipia na Tanzania maana kimamlaka hawashabihiani kabisa
Iweje SA mwenye mamlaka madogo akafanya makubwa zaidi ya mwenye mamlaka makubwa.

Rudia tena kujenga Hoja!!!
 
1) Hij umeiweka kinadharia sana
2) Elimu bure kaikuta kusema std 1 mpaka form 6 sio sawa, ungesema kuendeleza form 5 na 6
3) Zahanati na vituo vya afya kila kata na Kijiji? Hii hata mwenyewe ukimwambia atakubishia. Kama ulitaka kusifia hapa ungesema labda kajenga vingi lakini sio kusema kila kata kila Kijiji.
4) Ukuajia sekta ya kilimo? Nilirudi kwa lengo la kuingia kwenye kilimo. Hakuna kilichokua. Kuhusu ruzuku hapa ndio kuna ujinga umefanyika mkubwa. Lakini hata hivyo mbolea haikuhitaji ruzuku kwa maana bei inayouzwa Tz sio halisia, ujanja upo kwenye uagiziji, angedeal napo hapo wala asingekuja na siasa za ruzuku.
5) ukuaji sekta ya utalii? Utalii umekua vipi? Kulikua na Corona, nchi ziliweka lockdown. Waliofanya booking za kuja huku wakahairishiwa na ndio hao unaona wamekuja safari hii japo pia namba bado ipo chini sana.

Natambua siasa Ina mengi na ina wengi ambao lazima waseme hivi ili mambo yaende vizuri kwa watawala Ila kwa vitu vinavyoonekana ni vigumu kuongopea watu. Ajitahidi sana Ila kwa haya uliyosema umeweka na uongo mwingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…