Rais Samia anachapa kazi ila hazitangazwi ipasavyo. Wasaidizi wa Rais fanyeni kazi ipasavyo

umeongea kitu kikubwa ambacho nilkuwa na kiwaza. viongozi wengi hawasemi mamba yanayofanywa . mama awe makini sana
 
Kafanya mema 10 kavuruga 1 kwenye mkataba wa Bandari na wajomba zake Waarabu wa Dubai kaharibu kila kitu!
Tumepoteza Imani naye kwa kiasi kikubwa Sana, inaelekea ikibidi akae madarakani mpaka 2030 nchi hii kwishnei! [emoji848]
 
Zuhura Yunus,

Changamka, mama asikike. Usikae kusubiri kuandika wanaoteuliwa tu.

Watu wana hamu ya kujuwa heka heka zote za mama.
 
Unamshaurije wakati hayo unayomshauri ye alishayakataa;
1. Alisema hataki kumuona waziri akiwa na wapiga picha wa tv wala redio..leo husikii hata Ummy katembelea kituo cha afya na kutoa maendeleo ya kituo kilipofikia ama serikali kupeleke vifaa tiba(labda hakuna).
2. Zile ziara za kina Seleman Jafo za kukagua miradi mbalimbali nchini hakuna tena, sababu aliwakataa kina Jofu kwa kuona watapata umaarufu kuliko yeye.
3. We mwenyewe umeshuhudia kawatoa wapiga kazi kawaweka failures. Alimtoa Kalemani, akamtoa Lukuvi, akamtoa Ally Happi mchapakazi na akamkimbiza Polepole..ndio hao kina Makala kwake akaona wa maana..

Sie tuliliona hili toka mwanzo tukasema tukaitwa sukuma gang.

Miaka kadhaa enzi za JK ilikuwa hivi hivi, serikali ilikuwa haitoi taarifa. Simply tukaamini imelala. Baadaye wakaja kushtuka ndipo JK akaamrisha mawaziri watembee mikoani kueleza serikali imefanya nini..wee ile ziara kama sikosei ilianzia Mbeya na ikazikwa Mbeya, maana wananchi waliwapopoa na mawe ikabidi jamaa wasitishe.
 
bonde la mto msimbazi limemshindwa na mkopo keshakula.ni failure
 
Kama kuna kazi yoyote ya maana Samia anafanya basi kazi hizo zitamtangaza zenyewe na sio propaganda.
 
Nonsense
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…