Rais Samia Analipeleka na kuliongoza Taifa katika Njia Sahihi na yenye kuleta Matumaini kwa Mamilioni ya Watanzania

Uzuri au ubaya nchi hii marais wote wamentoka ccm. Hebu panga top five yako hapa tujue nani ni bora na nani wa hovyo kuliko wote. Nakusubiri pale kwa mangi
Kila zama na kitabu chake.kila Masika na mbu wake. Changamoto zilizokuwepo wakati wa serikali ya awamu ya kwanza na kile serikali ilichokipigania na kupambana nacho ,siyo kinachopiganiwa na kuwa changamoto wakati huu wa serikali ya awamu ya sita. Kila Rais ametimiza wajibu wake kulingana na wakati wake na mahitaji ya wakati husika.
 
Mpango wa Elimu bure ni kazi ya Samia sio au anaendeleza mtangulizi wake alipofikia tamati?

Eti Samia ni mpango wa Mungu(yeah ni kweli,sasa rais yupi alikuwa mpango wa shetani?).

Anyway,kila la kheri katika kupigania ugali wako.Vipi lakini safari yake nyingine itakuwa nchi gani tena mkurugenzi
 
I know. But kadili ya huu uzi wako it seems like you have ranked Samia higher than her predecessors.
 
Mpango wa Elimu bure ni kazi ya Samia sio au anaendeleza mtangulizi wake alipofikia tamati?

Eti Samia ni mpango wa Mungu(yeah ni kweli,sasa rais yupi alikuwa mpango wa shetani?).

Anyway,kila la kheri katika kupigania ugali wako.Vipi lakini safari yake nyingine itakuwa nchi gani tena mkurugenzi
Rais wetu mpendwa alikuta Elimu bure mpaka kidato cha nne.lakini alipoona kuna watoto wanaotoka familia za kipato cha chini wanashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa ada akaamua afute kabisa ada za kidato cha tano na sita ,pamoja na kuongeza bajeti ya Elimu ya juu ili wanafunzi wote wenye sifa waweze kupata mikopo ya elimu ya juu.
 
Silipwi hata mia mbovu kwa ajili ya kuandika ukweli hapa jukwaani. Mimi napenda kuusema ukweli Daima. Tuwe na shukurani Watanzania wenzangu kwa serikali yetu kwa kazi kubwa inayoifanya katika kuinua uchumi wa Taifa letu na kumsaidia mtanzania kujikwamua kiuchumi.
bro watu wamekalia majungu tu badala ya kufanya kazi wao wanawaza ujinga tu ukiwaambia ukweli wanasema chawa wape ukweli dawa iwaingie
 
Rais wetu mpendwa alikuta Elimu bure mpaka kidato cha nne.lakini alipoona kuna watoto wanaotoka familia za kipato cha chini wanashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa ada akaamua afute kabisa ada za kidato cha tano na sita ,pamoja na kuongeza bajeti ya Elimu ya juu ili wanafunzi wote wenye sifa waweze kupata mikopo ya elimu ya juu.
bado hili wapo wahuni hawalion kuwa ni jema
 
bro watu wamekalia majungu tu badala ya kufanya kazi wao wanawaza ujinga tu ukiwaambia ukweli wanasema chawa wape ukweli dawa iwaingie
Nitaendelea kuwaelimisha mpaka waelewe tu na kuondoa upofu akilini mwao.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ni hatari sana kuwaongoza watu na kuwapeleka katika njia ambayo haiwapi matumaini ya maisha na wala haionyeshi kuleta unafuu wa maisha kwa watu wala uhakika wa kutimiza ndoto zao au kuinuka kiuchumi. Njia ambayo muda wote watu wanaona giza mbele yao,hawaoni wanakokwenda wala tumaini la huko waendako na muda wote kuona bora walikotoka kuliko wanakokwenda.

Leo Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan Analipeleka na kuliongoza Taifa katika njia inayowapa matumaini watanzania.ambapo watu Leo hii wanamatumaini ya kupata tiba bora na stahiki waendapo hospitalini ,kutokana na uwekezaji mkubwa katika Secta ya Afya.

Leo Mtoto akifaulu darasa la saba au kidato cha nne anakuwa na uhakika wa kuendelea na masomo hata kama anatokea familia maskini ,kwa sababu tu ya uwepo wa Elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita . Leo mkulima akilima anao uhakika wa kuaga umasikini kwasababu ana uhakika wa kupata soko la uhakika kwa mazao yake lakini pia pembejeo za kilimo hususan mbolea zinapatikana kwa wakati.

Vijana wanaomaliza vyuo vikuu wanayo matumaini ya kupata ajira kwakuwa serikali ya Rais Samia kwa sasa inatoa ajira walau kila mwaka kwa kila Secta. Wafanyabiashara wanao uhakika wa kupata wateja kwa kuwa mzunguko wa pesa ni mzuri mitaani.

Kikubwa ni kuwa pamoja na hali ngumu ya kiuchumi iliyoikumba Dunia nzima kwa sasa,lakini juhudi za Rais wetu na serikali yetu tunaziona zikifanyika na ahueni ikipatikana ukilinganisha na majirani zetu. Hata katika suala la mfumuko wa Bei hususani chakula ukilinganisha Tanzania na majirani zetu unaona wazi kuwa Tanzania tuna unafuuu mkubwa sana hususani kipindi hiki cha mavuno.

Hata upande wa nishati ya mafuta ambayo ndio njini ya uchumi nako hali ni nzuri ukilinganisha na majirani zetu.ikumbukwe na kufahamika ya kuwa siyo serikali wala Rais ambaye anapandisha bei ya bidhaa kama nishati ya mafuta.bali Bei hupanda kutokana na kupanda katika soko la Dunia ambayo hutuathiri hadi sisi ambao hatuzalishi mafuta wala hatuna visima vya mafuta.

Kabla ya kulaumu au kuishutumu serikali yetu tuwe tunajaribu kufuatilia hali ya Dunia inavyokwenda,na kuangalia sababu ya kitu fulani au bidhaa fulani kupanda bei. kwa kufanya hivi tutaona na kugundua ya kuwa serikali yetu inafanya kazi kubwa sana kubeba mzigo wa gharama mbalimbali ili kumuokoa Mwananchi ,kwa kutoa au kupunguza kodi au kuweka Ruzuku katika bidhaa fulani kama ambavyo imekuwa ikifanya katika mbolea.

Natambua ni kweli hali ni ngumu lakini juhudi za serikali ni kubwa sana. Natambua serikali inatoa ajira kwa vijana lakini siyo vijana wote wanaopata ajira hizo, kwa kuwa vijana waliopo mitaani ni wengi sana ukilinganisha na nafasi zinazotolewa.ndio maana inaendelea kuipa nguvu Secta binafsi ili nayo izalishe fursa za ajira na kuweka mazingira wezeshi.

Natambua zipo changamoto za hapa na pale ambazo hata serikali yetu hukili hadharani, lakini tunaona na kujionea wenyewe watanzania namna serikali yetu inavyofanya kazi kwa nguvu zote kutatua changamoto hizo. Kwa hiyo tuache kutoa maneno machafu na lugha mbaya kwa serikali yetu. Tutoke nje ya mipaka ya nchi yetu tuangalie hali ilivyo,tusijifunge ndani ya mipaka. Tuwe watu wa shukurani kwa serikali yetu na kuitia nguvu kwa juhudi inazofanya badala ya kuikatisha tamaa na kushambulia kwa matusi ,lugha chafu na kejeli mitandaoni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
na kwakwli ndie mwana CCM, Rais pekee mwanamke Tanzania, ambae anakwenda kutimiza ndoto, matarajio na matamanio ya waTanzania kisiasa, kijamii na kiuchumi kwa uhakika na uwazi bila chenga mchana kwepeee 🐒

God bless our very loved President, comrade Dr Samia Suluhu Hassan
 
Rais wetu mpendwa alikuta Elimu bure mpaka kidato cha nne.lakini alipoona kuna watoto wanaotoka familia za kipato cha chini wanashindwa kuendelea na masomo kwa kukosa ada akaamua afute kabisa ada za kidato cha tano na sita ,pamoja na kuongeza bajeti ya Elimu ya juu ili wanafunzi wote wenye sifa waweze kupata mikopo ya elimu ya juu.
Sawa kiongozi nimekupata sema nimeuliza swali la kizushi kuhusu safari yake nyingine ni wapi tena hili akarejeshe mahusiano yetu na mataifa mengine.Maana muda sasa toka safari ya France sijasikia safari tena.

#Mama yupo kazini
#Mama anafungua nchi
#Kazi iendelee

HOVYO KABISA!
 
Wewe upo Serikalini bila shaka unapata ka Salary + Kuiibia serikali , huku ukisifia Ujinga ili wasikusitukie na ikiwezekana wakupe mamlaka pia 😂
 
Ndugu zangu Watanzania,

Ni hatari sana kuwaongoza watu na kuwapeleka katika njia ambayo haiwapi matumaini ya maisha na wala haionyeshi kuleta unafuu wa maisha kwa watu wala uhakika wa kutimiza ndoto zao au kuinuka kiuchumi. Njia ambayo muda wote watu wanaona giza mbele yao,hawaoni wanakokwenda wala tumaini la huko waendako na muda wote kuona bora walikotoka kuliko wanakokwenda.

Leo Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan Analipeleka na kuliongoza Taifa katika njia inayowapa matumaini watanzania.ambapo watu Leo hii wanamatumaini ya kupata tiba bora na stahiki waendapo hospitalini ,kutokana na uwekezaji mkubwa katika Secta ya Afya.

Leo Mtoto akifaulu darasa la saba au kidato cha nne anakuwa na uhakika wa kuendelea na masomo hata kama anatokea familia maskini ,kwa sababu tu ya uwepo wa Elimu bure kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita . Leo mkulima akilima anao uhakika wa kuaga umasikini kwasababu ana uhakika wa kupata soko la uhakika kwa mazao yake lakini pia pembejeo za kilimo hususan mbolea zinapatikana kwa wakati.

Vijana wanaomaliza vyuo vikuu wanayo matumaini ya kupata ajira kwakuwa serikali ya Rais Samia kwa sasa inatoa ajira walau kila mwaka kwa kila Secta. Wafanyabiashara wanao uhakika wa kupata wateja kwa kuwa mzunguko wa pesa ni mzuri mitaani.

Kikubwa ni kuwa pamoja na hali ngumu ya kiuchumi iliyoikumba Dunia nzima kwa sasa,lakini juhudi za Rais wetu na serikali yetu tunaziona zikifanyika na ahueni ikipatikana ukilinganisha na majirani zetu. Hata katika suala la mfumuko wa Bei hususani chakula ukilinganisha Tanzania na majirani zetu unaona wazi kuwa Tanzania tuna unafuuu mkubwa sana hususani kipindi hiki cha mavuno.

Hata upande wa nishati ya mafuta ambayo ndio njini ya uchumi nako hali ni nzuri ukilinganisha na majirani zetu.ikumbukwe na kufahamika ya kuwa siyo serikali wala Rais ambaye anapandisha bei ya bidhaa kama nishati ya mafuta.bali Bei hupanda kutokana na kupanda katika soko la Dunia ambayo hutuathiri hadi sisi ambao hatuzalishi mafuta wala hatuna visima vya mafuta.

Kabla ya kulaumu au kuishutumu serikali yetu tuwe tunajaribu kufuatilia hali ya Dunia inavyokwenda,na kuangalia sababu ya kitu fulani au bidhaa fulani kupanda bei. kwa kufanya hivi tutaona na kugundua ya kuwa serikali yetu inafanya kazi kubwa sana kubeba mzigo wa gharama mbalimbali ili kumuokoa Mwananchi ,kwa kutoa au kupunguza kodi au kuweka Ruzuku katika bidhaa fulani kama ambavyo imekuwa ikifanya katika mbolea.

Natambua ni kweli hali ni ngumu lakini juhudi za serikali ni kubwa sana. Natambua serikali inatoa ajira kwa vijana lakini siyo vijana wote wanaopata ajira hizo, kwa kuwa vijana waliopo mitaani ni wengi sana ukilinganisha na nafasi zinazotolewa.ndio maana inaendelea kuipa nguvu Secta binafsi ili nayo izalishe fursa za ajira na kuweka mazingira wezeshi.

Natambua zipo changamoto za hapa na pale ambazo hata serikali yetu hukili hadharani, lakini tunaona na kujionea wenyewe watanzania namna serikali yetu inavyofanya kazi kwa nguvu zote kutatua changamoto hizo. Kwa hiyo tuache kutoa maneno machafu na lugha mbaya kwa serikali yetu. Tutoke nje ya mipaka ya nchi yetu tuangalie hali ilivyo,tusijifunge ndani ya mipaka. Tuwe watu wa shukurani kwa serikali yetu na kuitia nguvu kwa juhudi inazofanya badala ya kuikatisha tamaa na kushambulia kwa matusi ,lugha chafu na kejeli mitandaoni.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wala hakuna ubishi
 
Back
Top Bottom