Mbona kama kajibu hivyo amejibu safi sana, nyinyi wabongo mushazoea kusema uongo na kupambia pambia mabosi wenu na kuwatukuza viongozi muda wote hata wakienda mchomo, siku zile Corona imeshika muliwalazimisha watu nchi nzima Corona isiitwe Corona eti iite ugonjwa wa kuambukiza., mukijaribu kuifananisha corona na magonjwa ya kawaida ili ionekane Corona sio tishio kwa maisha ya watu, wakati watu wakiendelea kupoteza maisha kwa hiyohiyo corona.
Samia nampongeza huyu mama anatabia ya kusema ukweli, na sasa anaonyesha waziwazi kwamba mwendazake alikuwa anakosea sana kwenye uongozi wake lakini kipindi kile mazingira yalikuwa hayamruhusu kumchalenge kutoka na hofu ya woga ambayo mkuu aliijenga.