Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

Haijalishi, ukweli uwekwe wazi. Sio Samia tu, wengi walifanya kazi na Magufuli kwa taabu sana. Labda kina Sabaya, Makonda, and the like ndio waliokua conformable.
 
Wanawake hao huwezi kuwalinganisha na huyu wa kwetu.
Wamekuwapo wa shoka kama kina Margaret Thatcher, Golda Meir, Angela Merkel, Indira Gandhi, Benazir Butho nk.

Wanawake nao ni watu tu ambako pia hata aina za akina Lusinde, Msukuma au Gwajiboy nako wapo.
.
 
Sasa hivi hawataki maendeleo?
Halafu hapo nikekutajia nchi kama Liberia iliyokuwa na migogoro na Vita kibao Kisha ikaongozwa na mwanamke ikatulia na kupata maendeleo

Haya mawazo ya kijima Sana,
Hizo nchi kwa sasa zina mifumo Bora, akija yoyote anaongoza kwa kufuata hiyo mifumo.

Liberia vita viliisha kabla ya Hellen kuwa raisi,, japo umaskini ulibaki wa kutisha hadi leo hii.
 
Damn pole kijana.

Itakuwa sipo Tanzania asee,  kapiga hatua gani mkuu ambazo huku nilipo siziju

mkuu, amepiga hatua gani huyu bibi?
hatua ni nyingi lakini mada ya hapa ilikuwa ni Covid-19, tunasema mama samia ameliona hili gonjwa kama ni hatari tofauti na mtu aliyepita ambaye alikuwa anakebehi na hakutaka kuchukua hatua zozote.,
 
Usifikiri kuwa Vp ni Kama kibarua kwa Patel, kwamba unaweza ukaamka na kusema sasa sitaki tena kazi. Hiyo moja, pili Samia angekurupuka kuacha kazi we ungeweza kumpa ajira? Alivumilia sana, na imemlipa, leo ndiye no. 1.
 
Hizo nchi kwa sasa zina mifumo Bora, akija yoyote anaongoza kwa kufuata hiyo mifumo.

Liberia vita viliisha kabla ya Hellen kuwa raisi,, japo umaskini ulibaki wa kutisha hadi leo hii.
Kwa hiyo wanaume ndio wasiovuruga mifumo? Kati ya Samia na Magufuli Nani kavuruga zaidi mifumo?

Hiyo Liberia ilikuwa ikitulia kidogo inaingia kwenye machafuko, kipindi Cha Sirleaf ndio kukawa na utulivu stable

Sasa hiyo Liberia na nchi zenye umasikini za Africa si zimeongozwa na wanaume zaidi? Unamlaumu Rais mmoja wa like kutokutoa umasikini wakati wanaume wote waliomtangulia hawakuweza?
 
Hilo jibu alimaanisha, matendo yake dhidi ya mapambano na Uviko-19 yapo tofauti kabisa kulinganisha nanyale ya mtangulizi wake...
 
Unajua tatizo kubwa lipo kwenye kulinganisha, hakuna niliposema wanaume wote Ni viongozi wazuri.
Ila kupo niliposema wanawake wengi sio viongozi wazuri.
Mfano; ukiacha Liberia, nchi nyingine iliyokua na vita mbaya ni Sierra Leone, Rwanda, ivory coast, n.k, lakini nao kuwa na amani hadi leo aliongoza mwanamke?
 
Kasema ukweli mchungu kwa wengine, asinge chanja nk. Hivi angeweza kuvaa barakoa kama afanyavo sasa kutwa nzima mbele ya Marehemu JPM?!
 
Nadhani unajichanganya mwenyewe

Unaposema viomgozi wengi wanawake wanakuwa sio wazuri, yapaswa kutoa na sample kadhaa za kuunga mkono, sio Samia, ukimtaja Samia tu na Mimi nitakutajia wanaweke wengine waliokuwa vizuri kuliko


Mfano kama Mobutu anasemwa alikuwa kiongozi mbaya kwa nini hoja hapa isiwe jinsia yake Ila ikitokea Rais mwanamke akafanya vibaya (japo wapo waliofanya vizuri) hoja inakuwa ni jinsia yake?
 
Kuna vitu nimekubaliana na ww hapo mwanzo, Ila naona tunarudi tena nyuma
 
Kasema ukweli mchungu kwa wengine, asinge chanja nk. Hivi angeweza kuvaa barakoa kama afanyavo sasa kutwa nzima mbele ya Marehemu JPM?!
Kwanini asiwalazimishe watanzania wavae barakoa kama kweli ndo njia nzuri, ni wapi watanzania wanavaa barakoa. Kuvaa Barakoa ni utumwa wa fikra kama haipo katika uhalisia wa wananchi unaowatawala
 

Kwani ni uongo? Hakuwahi kuwaita mawaziri wake wapumbavu?
 
Popote penye uovu ni vyema kukemea kila inapowezekana. So kama mama kakemea jambo ambalo halifai baada ya kupata fursa ya kufanya hivyo ni jambo jema.
 
Hakuwa na msimamo wowote kwani mbona mikutano yake mingi ameonekama havai barakoa. Kama kweli alikuwa anapingana katika mtazamo huo angeonyesha hata kwa yeye kuvaa barakoa bila kuhamasisha wengine.
Ni njia tu za kumsigina mwenzako ili kutaka misaada.
 

Tz tulishazoea kuambiwa uongo na watawala wetu. Ikitokea mtu akasema ukweli basi huyo ni msaliti.
Tuvumiliane tuu. Mama anaupiga mwingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…