Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

U afiki mtupukwa . Walioweka lock up walitoboa? Kwa taarifa yako kwenye handling ya covid magufuli ni kinara duniani. Utake usitake kwa webye akili wanatambua kwamba dunia nzima inatumia method ya magufuli kwasasa with some few modifications
Kwa hiyo dunia nzima wanajifukiza na kuagiza dawa madagascar
 
Kujibu maswali ya wanahabari nguli wa kimataifa na kukwepa mitego kwenye maswali yao inahitaji uwe na IQ kubwa kwerikweri...........siyo hizi IQ za kuunganisha na cello tape....
 
U afiki mtupu. Walioweka lock up walitoboa? Kwa taarifa yako kwenye handling ya covid magufuli ni kinara duniani. Utake usitake kwa webye akili wanatambua kwamba dunia nzima inatumia method ya magufuli kwasasa with some few modifications

Method ya Magufuli ipi?.
 
Nyerere alikua ni kibibi cha kizungu ubavuni, si kama alikua genius kiasi hiko. Mleta mada yupo sahihi, unapokua na wasaidizi wabovu lazima utakua unavurunda vurunda mara kwa mara.
Bila shaka hukumuona na humjui Nyerere
 
wanaomkosoa Rais walipaswa watuambie jee walitaka Rais aseme hakuwahi kutofautiana mawazo na Bosi wake?

kwanini tunataka Rais wetu awe muongo muongo?


sie tunataka dola za Wazungu mwacheni aseme lolote ambalo litarahisisha upatikanaji wa fedha

hata Comrade Kinana aliinanga sana Serikali ya Jakaya 2010-2015 ili kuingiza maboya wananchi tupate ushindi na kweli ushindi ukapatikana …mwanasiasa ili afanikishe lake hutumia 'silaha ' zote
Kama alitofautiana kwanini hakutuambia akiwa kwenye mukutano hapa nchini ameenda kujikomba akiwa kule. Issue hapo ni IQ tu.
 
Mbona kama kajibu hivyo amejibu safi sana, nyinyi wabongo mushazoea kusema uongo na kupambia pambia mabosi wenu na kuwatukuza viongozi muda wote hata wakienda mchomo, siku zile Corona imeshika muliwalazimisha watu nchi nzima Corona isiitwe Corona eti iite ugonjwa wa kuambukiza., mukijaribu kuifananisha corona na magonjwa ya kawaida ili ionekane Corona sio tishio kwa maisha ya watu, wakati watu wakiendelea kupoteza maisha kwa hiyohiyo corona.

Samia nampongeza huyu mama anatabia ya kusema ukweli, na sasa anaonyesha waziwazi kwamba mwendazake alikuwa anakosea sana kwenye uongozi wake lakini kipindi kile mazingira yalikuwa hayamruhusu kumchalenge kutoka na hofu ya woga ambayo mkuu aliijenga.
Samia alichokifanya kwa Ndugai unadhani kuna kukosolewa au challage tena kwenye utawala wake?
 
jibu ni rahisi

huwezi kujibu kama hukuulizwa

Hata Assad alisema Bunge ni dhaifu akiwa ughaibuni kwa kuwa huko ndio kaulizwa

huku maswali yetu ni ya kujipendekeza
Kama alitofautiana kwanini hakutuambia akiwa kwenye mukutano hapa nchini ameenda kujikomba akiwa kule. Issue hapo ni IQ tu.
 
Sio kosa lako, umeathiriwa na matatizo ya kusema uongo ili kulinda hadhi fulani. Tatizo la kutokusema ukweli ndio limetufikisha watanzania hapa tulipo. Mama kaulizwa 2+2 kasema ni 4, ulitaka aseme ni 5 kama tulivyozoeshwa hapa nchini?
Ila ni kweli mama ni msema kweli nakumbuka 2020 alishasema kuwa ccm lazima iwe madarakani tu hata mkipigia upinzani na kweli ikawa hivyo.
 
Okay siwezi kubisha maana sijui behind the scenes Nyerere alikuwa akijiandaa au la

Ila Nyerere alikuwa na umahiri wake na mapungufu yake, Samia nae ana umahiri wake na mapungufu yake

Pale kwenye mapungufu ndio tunashauri namna ya kurekebisha
Ebu nitajue huo umahir wa mcho mlemda jomba! Angalau hata mmoja tuu! Mana mm sioni umahir wowote zaid ya kuangalia macho yake tuu..
 
Unaweza vipi kumpa somo mtu ambaye hajui akienda kwenye interview ataulizwa nini?

Hili kwangu linahitaji uelewa binafsi wa mtu, ajue mwenyewe jinsi ya kujiongeza pale anapoulizwa maswali, uwezo wa kuchagua maneno ya kuongea awe nao wakati huo huo akihakikisha meseji aliyokusudia anaifikisha.

Lakini pia, wakati mwingine tuwe tayari kukubaliana na hali halisi, kwa namna Magufuli alivyoongoza nchi, akaonekana "stubborn" mpaka nje ya nchi hasa kuhusu Corona, sijui ulitaka Samia aseme nini zaidi ya kile alichosema, au wewe ndio unataka kumfundisha kusema uongo?
Ukimuuliza Samia kuhusu ule uchaguzi wao wa 2020 unadhani atasema ukweli kwamba haukuwa uchaguzi bali ni uchafuzi?
 
Samia alichokifanya kwa Ndugai unadhani kuna kukosolewa au challage tena kwenye utawala wake?
Ndugai mwache yamkute huwezi kumkosoa rais kwa kebehi namna ile aliyofanya ndugai ilhali yeye ni spika ndani mfumo ule ule., alipaswa kuwasha gari lake hadi ikulu kwenda kuzungumza na rais kwa heshima juu ya kile anachokiona yeye na kushauriana na rais, lakini anaenda kumtovukia mama adabu mchana kweupe kwa sabab hakupendezwa
 
Kama unasema kulikuwa na hofu ya woga basi hufai kuwa kiongozi. Kiongozi unapaswa usimamie unachokiamini na si kuyumba, migogoro ya kimtazamo mara zote huzaa better solution.
Tanzania haikujengwa hivyo, huu ni utamaduni wenu inabidi ukae kimya kumtii aliye juu yako
 
Ndugai mwache yamkute huwezi kumkosoa rais kwa kebehi namna ile aliyofanya ndugai ilhali yeye ni spika ndani mfumo ule ule., alipaswa kuwasha gari lake hadi ikulu kwenda kuzungumza na rais kwa heshima juu ya kile anachokiona yeye na kushauriana na rais, lakini anaenda kumtovukia mama adabu mchana kweupe kwa sabab hakupendezwa
Demokrasia ni ngumu sana mkuu.

Kama Samia alikuwa anatofautiana na Mkubwa wake ila aliogopa kusema kwa kipindi chote ndio unadhani kuna kiongozi atakaye kuwa na ujasili wa kumkosoa Samia wazi wazi ilihali wameona kilichomtokea Ndugai kwa kutoa maoni tu.
 
Alichoeleza nisawa kabisa.
Hakuna Mtanzania yyt aliefurahi kuganya kazi na Magu, alikuwa na sifa ya Bully, katili n.k

Nadhani ulitaka amsifie Mag kule New york. Hao jamaa wana research ya kutosha kuhusu Magufuli kuliko unavyo dhania.
Samia angeendeleza Tabia ya Watanzania ya kusifisifia viongozi angesambaratishwa kwenye hiyo interview.

Alivyojibu vile maswali magumu yalipunguwa na haikuwasiri, sisi wote tunajuwa Magu alikuwa mtu mgumu kufanyanae kazi
Pia amesema yaliyomkuta kama msaidizi. Kuwa msaidizi katika ngazi ile ni sawa na kufunga pingu za maisha. Msaidizi bila msaada.
 
Bora kuwa mkweli siku zote utakuweka huru, atamsifia magu alipofanya vizuri lakini alipokwanga wacha amnange kisawasawa, damage ya kusema ukweli itachukua muda mduchu sana uongo ndio utakuathiri milele
Ukweli unasemwa baada ya mtu kufariki ila yeye alipoambiwa ukweli na Ndugai akamshughulikia.
 
Jibu alilojibu raisi linaonyesha Serikali haikuwa organized .Raisi kivyake makamu kivyake utafikiri Serikali ya Sudan kusini kati ya Raisi Salva Kiir na makamu wake Riech machar!! Hakukuwa na unit of command and purpose

Swali je sasa Serikali ya Mama Samia iko organized from bottom to the top? Hilo swali kawaachia homework wamarekani wafanye analysis wenyewe!!
Na hiyo ni tishio kubwa sana kwa investor, maana yake political risks iko juu sana. Maana yake ni kuwa kama yeye alikuwa haelewani na rais wake akiwa Makamu basi hata sasa Makamu wake watakuwa hawaelewani maana yake ikitokea Mama bahati mbaya yamemkuta ya Dkt Magufuli maana yake makamu wake ataondoa kila ambacho Mama Samia kakiweka na kuweka mazingira magumu kwa wawekezaji. Na ktk kipindi hiki wawekezaji wa kizungu watakuwa katili sana no money will be left in Tanzania. Kwa ufupi kauli ya Mama inatafasiri nyingi mno kiasi kwamba nadhani hata yeye imemchanganya.
 
Siyo siri kwamba mahusiano yetu na Marekani yalivurugika kipindi cha utawala uliopita ambao Rais wa sasa alikuwa sehemu yake kwa ngazi za juu kabisa. Kutegemea aende Marekani na kuondoka bila kuulizwa haya maswali au kuyajibu, kana kwamba kila kitu kilikuwa sawa, tuendelee tulipoishia 2010, ni kujidanganya. Haya maswali alitegemea kukutana nayo na sioni namna gani nyingine tofauti angeweza kuyajibu.

It is what it is
Akiulizwa kuhusu ule uchaguzi wa 2020 pia atajibu ukweli au atajibu kisiasa? Maana haijawahi kutokea uchaguzi kama ule.
 
Back
Top Bottom