Rais Samia anapaswa kupewa mbinu za kujibu interview, wasaidizi wake mmemuangusha

Sasa ulitegemea Samia aseme amemvua uspika Ndugai?
Samia alirespond baada ya Ndugai kukebehi kwamba nchi itapigwa mnada na yeye akajibiwa kwa uhalisia wake, sasa kujiuzulu aliwaza yeye mwenyewe ndugai, asubiri 2030 kama vipi
 
Mahojiano ya jana ya Rais Samia na Gazeti la New York Times alinukuliwa akisema alipata wakati mgumu kufanya kazi na Hayati Magufuli kutokana na msimamo wa Magufuli juu ya Covid-19.

Japokuwa simkubali Magufuli, lakini hii kauli haijakaa sawa, lakini nina uhakika Rais Samia hakudhamiria kusema hivyo, bali aliyekuwa akimhoji ndio alimbana na kulazimisha kusema hivyo.

Kwa wanaoangalia mahojiano ya viongozi na waandishi wa habari wa nchi za 'mbele' wanajua jinsi waandishi hao wanavyokuwa aggressive, mnakumbuka Tundu Lissu mwenyewe alivyobanwa na mwandishi wa BBC hadi kujikuta ametamka atawapa mashoga haki zao...! Baadae akaja kukana hakumaanisha hivyo, ila sikumlaumu maana unabanwa kwelikweli.

Sasa kwa mtu kama Rais ambaye ana wasaidizi wengi smart walitakiwa ku-anticipate maswali ambayo angeulizwa Rais, na Rais angekua namna ya kuyajibu kabla, kuna maswali mengine unaya-dodge tu badala ya kutoa majibu direct ambayo yataleta utata, ndivyo wanasiasa hufanya.

Wasimuache kama anaenda kuhojiwa TBC.

Nadhani hili halitajirudia tena.

Ndio dawa ya wanafiki, sasa wanageukana, wakati huo walikubaliana na ujinga woote.
Alidhani ni TBC ile.
 
Mambo mengine ni uwezo binafsi.

Swala hapa ni kutomuexpose na situations kama hizo.

Yaani wasaidizi wake wawe wajanja kumkwepesha na mazingira kama hayo. Itokee very rare kuwa anahojiwa na vyombo vikubwa kama hivyo.

Huko mbele watu wako ahead of us kwa karne kadhaa. Uwezo wao wa kufikiri ni mkubwa sana.
Huu ujinga aliuweza Jiwe tu, na ndio maana aliogopa kusafiri nje ya nchi baada ya kuchemka Uganda. Ukiwa rais huwezi kukwepa kuulizwa maswali kwa wenzetu huko, tena ya papo kwa hapo na sio ya TBCCM.
 
Samia alirespond baada ya Ndugai kukebehi kwamba nchi itapigwa mnada na yeye akajibiwa kwa uhalisia wake, sasa kujiuzulu aliwaza yeye mwenyewe ndugai, asubiri 2030 kama vipi
Mkuu hata hili nalo unataka kukomaa? Mbona jambo ambalo lipo wazi kabisa, haya tufanye basi Ndugai aliamua tu mwenyewe kujiuzulu bila shinikizo lolote.
 
Aila zake ndugai kina lukuvi hao ndio walimwambia sasa kwa ushavyolikoroga hutaweza tena fanya kazi na mama bora andika barua jiuzulu., mama baada ya kumjibu mwisho alisema msameheni
 
Una uhakika anao wasaidizi wenye IQ/akili njema?
Mahojiano ya jana ya Rais Samia na Gazeti la New York Times alinukuliwa akisema alipata wakati mgumu kufanya kazi na Hayati Magufuli kutokana na msimamo wa Magufuli juu ya Covid-19.

Japokuwa simkubali Magufuli, lakini hii kauli haijakaa sawa, lakini nina uhakika Rais Samia hakudhamiria kusema hivyo, bali aliyekuwa akimhoji ndio alimbana na kulazimisha kusema hivyo.

Kwa wanaoangalia mahojiano ya viongozi na waandishi wa habari wa nchi za 'mbele' wanajua jinsi waandishi hao wanavyokuwa aggressive, mnakumbuka Tundu Lissu mwenyewe alivyobanwa na mwandishi wa BBC hadi kujikuta ametamka atawapa mashoga haki zao...! Baadae akaja kukana hakumaanisha hivyo, ila sikumlaumu maana unabanwa kwelikweli.

Sasa kwa mtu kama Rais ambaye ana wasaidizi wengi smart walitakiwa ku-anticipate maswali ambayo angeulizwa Rais, na Rais angekua namna ya kuyajibu kabla, kuna maswali mengine unaya-dodge tu badala ya kutoa majibu direct ambayo yataleta utata, ndivyo wanasiasa hufanya.

Wasimuache kama anaenda kuhojiwa TBC.

Nadhani hili halitajirudia tena.
 
Ipo haja ya wasaidizi waje kurekebisha hili...nimeona mara nyingi matamshi yake yanatafsiriwa tofauti na kuleta sintofahamu mfano ni ile ya kula kwa urefu wa kamba nk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wenyewe twaona sifa Rais wetu kuhojiwa na vyombo vya levels za kidunia. Matokeo ya mahojiano hayatuhusu sana. Tuacheni tuendelee kuupiga mwingi.
 
U afiki mtupu. Walioweka lock up walitoboa? Kwa taarifa yako kwenye handling ya covid magufuli ni kinara duniani. Utake usitake kwa webye akili wanatambua kwamba dunia nzima inatumia method ya magufuli kwasasa with some few modifications
Kinara kwa kuwaaminisha watu kua haikua korona ni changahmoto ya kupumua???
 
Back
Top Bottom