Anna Nkya
Member
- Oct 21, 2021
- 69
- 341
Ni kilio cha muda mrefu cha wanasiasa wa Tanzania hususan vyama vya upinzani. Wanataka kurudishwa kwa mikutani ya hadhara ambayo ni haki yao ya Kikatiba, lakini iliminywa wakati wa utawala wa awamu ya tano chini ya Hayati Rais John Pombe Magufuli.
Leo kwenye mkutano wa wadau wa siasa nchini unaoendelea huko Dodoma, Rais Samia Suluhu ametoa kauli yenye matumaini na kuonesha kwamba nia yake ni kuona vyama vya siasa vinafanya mikutano hiyo. Hilo linathibitika kupitia maelekezo aliyoyatoa kwamba mkutano huo lazima ujadili namna bora ya vyama vya siasa vitakavyoweza kufanywa kwa mikutano ya hadhara bila kuvunjwa kwa Sheria za nchi.
Rais amesema "Lengo la mijadala kama hii ni kujenga na si kubomoa. Hivyo niwasihi kwamba katika mijadala itakayoibuliwa kwenye mkutano huu leo, naomba pia mjadili namna bora ya vyama siasa vitakavyoweza kufanya mikutano ya hadhara bila kuvunjwa kwa sheria za nchi…naomna mjadili na mjifunge wenyewe hapa jinsi mtakavyokwenda kufanya mikutano ya hadhara. Nataka msajili, Jeshi la Polisi, kaeni na hawa watu muone. Kwa sababu ni haki yenu, ya Kikatiba zenu na Katiba ya nchi kufanya mikutano kunadi sera zenu, lakini mnaivunja ninyi wenyewe”
Rais amesisitiza kwamba ni vyema mikutano hiyo ifanyike kwa kufuata taratibu.
Bila shaka, Mkutano unaoendelea Dodoma utakuwa na majibu, na wale waliokwenda kule watakuwa wamefanya kazi kubwa ya kurejesha mikutano hiyo.