Rais Samia anarudisha mikutano ya hadhara ya vyama siasa

Rais Samia anarudisha mikutano ya hadhara ya vyama siasa

Sheria gani za nchi zinavunjwa chama kinapofanya mkutano wa hadhara?

Angesema ama kuweka wazi kuwa jambo hili ama lile ni uvunjaji wa sheria za nchi wakati wa mkutano wa hadhara.

Hata mikutano ilipozuiliwa hakuna aliyesema kuna sheria za nchi zinazovunjwa. Sana sana ni polisi wanakataa kutoa vibali.

Sasa hata vikao vya ndani vyenyewe vimepigwa marufuku. Sheria gani inakuwa imevunjwa?
Mama anazidi kujidhaliliaha anataka kuonesha kuwa hakuna kosa linalofanywa na vyombo vyake. Anataka kulazimisha watu waamini kuwa vyama vya siasa huwa vinavunja sheria
 
Tumejiwekea katiba na sheria ila vinawekwa pembeni kusubiri eti busara za mwemye mamlaka. Huu ujinga hautaipeleka Tanzania na Africa popote kimaendeleo.
 
Harudishi chochote

Arudishe ashindwe urais

Arudishe CCM itoke madarakani

Ni maoga sana haya mawanasiasa yaliyopata urais kama ajali maana sio haki yao kupata hicho cheo,sio wanasiasa bora TZ au humo CCM

Hakuna wanasiasa waoga kama hawa waliopata madaraka kiajali namna hii maana hawana uwezo
CCM wote waoga wa hoja. Hawawezi ruhusu hoja asilani. Wanaishi na kuongoza kwa mabavu. Hoja zikiwazidi wanajibu kwa risasi.
 
Ni kilio cha muda mrefu cha wanasiasa wa Tanzania hususan vyama vya upinzani. Wanataka kurudishwa kwa mikutani ya hadhara ambayo ni haki yao ya Kikatiba, lakini iliminywa wakati wa utawala wa awamu ya tano chini ya Hayati Rais John Pombe Magufuli.

Leo kwenye mkutano wa wadau wa siasa nchini unaoendelea huko Dodoma, Rais Samia Suluhu ametoa kauli yenye matumaini na kuonesha kwamba nia yake ni kuona vyama vya siasa vinafanya mikutano hiyo. Hilo linathibitika kupitia maelekezo aliyoyatoa kwamba mkutano huo lazima ujadili namna bora ya vyama vya siasa vitakavyoweza kufanywa kwa mikutano ya hadhara bila kuvunjwa kwa Sheria za nchi.

Rais amesema "Lengo la mijadala kama hii ni kujenga na si kubomoa. Hivyo niwasihi kwamba katika mijadala itakayoibuliwa kwenye mkutano huu leo, naomba pia mjadili namna bora ya vyama siasa vitakavyoweza kufanya mikutano ya hadhara bila kuvunjwa kwa sheria za nchi…naomna mjadili na mjifunge wenyewe hapa jinsi mtakavyokwenda kufanya mikutano ya hadhara. Nataka msajili, Jeshi la Polisi, kaeni na hawa watu muone. Kwa sababu ni haki yenu, ya Kikatiba zenu na Katiba ya nchi kufanya mikutano kunadi sera zenu, lakini mnaivunja ninyi wenyewe”

Rais amesisitiza kwamba ni vyema mikutano hiyo ifanyike kwa kufuata taratibu.

Bila shaka, Mkutano unaoendelea Dodoma utakuwa na majibu, na wale waliokwenda kule watakuwa wamefanya kazi kubwa ya kurejesha mikutano hiyo.

View attachment 2044931

Vyama vya siasa kufanya siasa (including mikutano ya hadhara) hakuvunji sheria wala Katiba. Kuvizuia vyama vya siasa kufanya siasa ndio kuvunja Katiba ya nchi na hapo hakuhitajiki mjadala wa msajili & polisi bali kufanya rejea kwenye vipengele husika vya Katiba kwa utekelezaji katika ngazi zote husika. Chief Hangaya asikwepe wajibu wake wa kuilinda Katiba kama alivyo apa!
 
Back
Top Bottom