Rais Samia anatengenezewa Ajali za kisiasa

Rais Samia anatengenezewa Ajali za kisiasa

Rais aliporidhia awekwe mwekezaji ambaye ataziba mianya hii tena kwa mkataba wa miaka isiyo zidi 20 kwa kipindi renewable kundi hili likaona fursa, lika spinn na kuvujisha sehemu ya makubaliano na kuyaita uuzaji wa nchi, jambo amabalo sio la kweli, wanatia pressure ili Rais aachana na ubinafsishaji wa bandari waendelee kunyonya rasilimali kwa jina la uzawa.
Je kwanini yeye mwenyewe Rais hajajitokeza hadharani kusema mkatani wa miaka kadhaa na akaonyesha maandishi hayo wazi?
 
Mipango ya kuharibu bwawa la mwalimu nyerere ilmeandaliwa kifundi kabisa na sababu zitakazotolewa hazitakua kuharibiwa bali ikolojia ya eneo kushindwa kustahimili nguvu za bwawa ili kumuepusha mkandarasi na lawama maana wanajua anaweza kushtaki kuhujuliwa.

Wameshamlazimisha kuandika maelezo yanayoonyesha eneo hilo lina miamba dhaifu aridhini hivyo life span yake haiwez kuwa kubwa, kupasuka kwa bwawa kutazika matumaini ya umeme nafuu na kuzika kabisa matumaini ya Rais Samia kuchaguliwa tena.
In so saying ni kwamba Makumbusho imekula samaki aitwaye pono
 
Kwanza nianze kwa kuwapa starter moja muhimu sana maana Watanzania tumeumbwa kukumbuka ya leo, ya jana tunayasahau kirahisi sana.

Mnakumbuka Rais Samia alitangaza kuifungua nchi na watu wote tukashangilia? Mnakumbuka alisema atakamilisha miradi yote iliyoachwa na Hayati Magufuli na watu wote tukashangilia? Mnakumbuka aliwahi kusema yeye na Magufuli ni kitu kimoja na wote tukashangilia?

Rais Samia ametimiza yote hayo na anaelekea kuvuka matarajio ya wengi sana, wengi walidhani inawezekana akaishiwa pumzi mapema sana, ndio maana utaona ndani ya CCM kuna makundi mpaka sasa makubwa mawili yanayoamini Rais Samia hatafika 2025.

Dhana ya kundi la kwanza ni kuwa Rais Samia hatafanikiwa kuwaridhisha watanzania na kufikia approval rating zakumpa go ahead ya re-election, hivyo mgombea mmoja ameamini kwa kigezo hiki yeye akajiweka tayari kuwa mbadala.

Dhana ya kundi la pili ni kuwa hata akifanikiwa, kundi hili limejipanga kumwekea ajali za kisiasa ili ajikwae na kuanguka kisiasa, kundi hili lina nia ovu zaidi kwa kua linatumia hadi njia zisizoelezeka kwenye jukwaa hili maana ni njia haramu na za kijinai kumkwamisha Rais Samia na Mhe Rais analijua hilo.

Sasa baada ya utangulizi huo naomba niwaeleze jambo moja ambalo baada ya mihemko ya Bandari kuisha mtarudi hapa na kufanya thread hii kama marking scheme ya mambo mengi sana mnayoyaota.

Kuna ajali kubwa tano ambazo kundi la pili limeziandaa kwa Mheshimiwa Rais, na ajali mbili tayari zimeshakua executed systematically and very carefully

1. AJALI YA KISIASA KWA WAFANYABIASHARA
Kundi hili katili linalosaka urais 2025 na linaamini kwa 80% litaupata , liliandaa mgogoro wa wafanyabiashara wa soko la Kariakoo, na kuset up Rais achafuke kisiasa, lilifanikiwa vipi?

Watu hawa kwa kushirikiana na wafanyabiara waovu, walianza kudeclare mizigo inayopita bandarini kama kama vifaa visivyo na thamani , mfano mzigo wa Vigae unakua declared kama tissue paper, hivyo kulipiwa pesa kidogo bandarini, watu hawa wakawa wanatunza kwenye store mizigo hii na kulipa kodi kidogo za tissue paper kwa mzigo wa vigae.

Suprising, watu hawa wakajifanya wanamtonya Rais kuwa kuna uhujumu uchumi kwa wafanyabiashara, waambie TRA waanze kukagua Mizigo store utatuamini, Rais baada ya kuchunguza kweli akakuta ni valid case kuwa vigae vinapita kama tissue bandarini hivyo mizigo ikaguliwe store kukamata wahujumu hao.

Muda wote huo watu hawa walikua calculative sana, wakawaandaa wafanyabiashara upande wa pili kuwa serikali inaanza kuwa harass msikubali, script ikatick Rais wakampigisha ajali ambayo Waziri Mkuu aliokoa dakika za jioni sana.

2. MAMLAKA YA SERIKALI MTANDAO E-GA KUBINAFSISHWA
Genge hili la pili, likaratibu pia ajali nyingine ambayo 70% imeiva soon wataiweka barabarani, kupitia viongozi waandamizi wapatao sita toka TAMISEMI, wizara ya fedha na mipango , BOT, TRA na wengine wako wizara mbali mbali, wameunda mbinu ya kudhoofisha ufanisi wa mifumo iliyotengenezwa na E-GA wanashawishi makampuni binafsi na mengine toka nje yaje kuendesha mifumo ya TEHAMA serikalini, na E-GA ibaki kama mwangalizi tu yaani regulator.

Watu hawa wameshaanza kufanikiwa, wameleta wataalamu wa mifumo toka nje na kulazimisha kuandika report zinazoonesha mifumo sio salama na inaweza kuingiliwa na mataifa ya nje kirahisi, hivyo makampuni binafsi yapewe kandarasi hio.

Lengo lao Rais Samia aridhie ili public outcry isikie kua anaua vipaji vya ndani na kuwapa wageni, set up imekamilika wanasubiri muda walipue .

3. BANDARI ZETU
Kundi hili hatari limefanikiwa kugeuza mjadala wa ubadhilifu bandarini na kufanya watanzania waone ubinafsishaji ni uuzaji wa nchi.

Duration ama urefu wa mkataba haujulikani publically kwa sababu maalumu, lakini kwa 100% sio wa milele wala sio wa miaka 100. Ilikuaje kundi hili lika set up trap hii?

Bandarini kuna wizi unafanywa na hawa tunaowaita wazawa, wa mpaka 200milion kwa week kwa mtu mmoja kwa baadhi ya government senior officials, wengi wanakula njama hizi kwa kushirikiana na TRA.

Wanasiasa wengi wanapitisha mizigo yao bandarini bure kabisa yenye thamani ya billions of money.

Rais aliporidhia awekwe mwekezaji ambaye ataziba mianya hii tena kwa mkataba wa miaka isiyo zidi 20 kwa kipindi renewable kundi hili likaona fursa, lika spinn na kuvujisha sehemu ya makubaliano na kuyaita uuzaji wa nchi, jambo amabalo sio la kweli, wanatia pressure ili Rais aachana na ubinafsishaji wa bandari waendelee kunyonya rasilimali kwa jina la uzawa.

Watanzania mngejua wachache wananyokula bandari mneandamana, Rais ameamua aweke watu serious, kundi lime spin taarifa na kulipa pesa nyingi sana wapinzani na baadhi ya vyombo vya habari kutia moto jambo hili.

4. BWAWA LA NYERERE
Bwawa hili limebeba hatima ya Rais samia re-election, kundi ovu limejipanga kuharibu kingo za bwawa hilo kabla ya vikao uchaguzi wa serikal za mitaa mwakani ili CCM ikose uungwaji mkono na kuonesha kua Rais hatoshi.

Mipango ya kuharibu bwawa la mwalimu nyerere ilmeandaliwa kifundi kabisa na sababu zitakazotolewa hazitakua kuharibiwa bali ikolojia ya eneo kushindwa kustahimili nguvu za bwawa ili kumuepusha mkandarasi na lawama maana wanajua anaweza kushtaki kuhujuliwa.

Wameshamlazimisha kuandika maelezo yanayoonyesha eneo hilo lina miamba dhaifu aridhini hivyo life span yake haiwez kuwa kubwa, kupasuka kwa bwawa kutazika matumaini ya umeme nafuu na kuzika kabisa matumaini ya Rais Samia kuchaguliwa tena.

Wameshaandaa mtu wao ambaye atakuja kama masiah ambaye katika ajali hizi wanamweka mbali systematically asiwe sehemu ya uovu wowote

5. AJALI YA 5 NI CONFIDENTIAL
Hii naomba kwa sababu za kiusalama wa nchi nisiiandike, lakini people are very serious, they are ready to to the unthinkable.

My Take: Idara yetu pendwa ya Makumbusho najua mvutano unaoendelea, am sad kwa sababu tumeanza kuchagua pande za wagombea .

Wazo la kutaka kumrudisha Kipilimba mngeliacha kwanza, aliyepo anatosha na anaye attempt ya kubadili DGIS ita spark unprecedented issues.

Rais Samia is so innocent, aachwe aongoze nchi

View attachment 2650494
Mkuu Kuna watu wa kutetewa lakini Samia kafeli sana,yeye mwenyewe anajikaanga na Mafuta yake mwenyewe kwa kurudisha wezi serikalini.
 
Mkuu Kuna watu wa kutetewa lakini Samia kafeli sana,yeye mwenyewe anajikaanga na Mafuta yake mwenyewe kwa kurudisha wezi serikalini.
Mkuu Butron ,hata mimi kuna muda niliwaza hivyo ,lakini kuna taarifa muhimu ukizipata utaogopa kaka,huyu mama kimsingi asingekuwa yeye kuna wasiwasi nchi ingekua chini ya jeshi.She is doing alot
 
Je kwanini yeye mwenyewe Rais hajajitokeza hadharani kusema mkatani wa miaka kadhaa na akaonyesha maandishi hayo wazi?
Mkuu ,wakati mwingine kwenye hizi siasa kuibuka mapema mapema ni kuingia kwenye mtego wa adui , Rais anapaswa awe wa mwisho kusema ,akisema inakua final call, imagine wananchi wamepewa muda wa kutoa maoni at the same time Rais naye aanze kuongea atakua anaharibu michango ya wananchi , She is right to keep quite for now
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Usimuwazie sana mkuu.
Ajali kazitega mwenyewe.

Anajua kila kitu. Wala hana haja na ushauri wetu
Mkuu nakuelewa ,lakini hii issue ina complexity za ajabu sana ,lau watu wangejua wangemuombea sana mama Samia
 
Mkuu nakuelewa ,lakini hii issue ina complexity za ajabu sana ,lau watu wangejua wangemuombea sana mama Samia
Hadi Abdul kutuwakilisha ug Kuna complexity ndugu mpiga mapambio?
 
Mkuu nakuelewa ,lakini hii issue ina complexity za ajabu sana ,lau watu wangejua wangemuombea sana mama Samia
Unamwombea mtu ambaye kila siku ni mikwara, vitisho na masimango?

Ana mtaji wa Watanzania zaidi ya milioni 61. Yeye amejisimika na kakikundi kadoogo ka watu ambao kila wanalomshauri linakuja kukwama kila baada ya muda mfupi. Tulimweleza kuhusu hii mitego ya kisiasa aliposimama na kufuta ile gharama ya kuunganisha umeme kwa Tshs 27k kwa vijijini na akamuweka Makamba pale na akaridhia biziness za majenereta..... ikaja Tozo akaziba masikio akasaini watanzania waishi kwa jasho lq meno, mitaji ya wajasiriamali ikafa huku akiendelea kutabasamu. Kama haitoshi akawaondoa wamachinga mijini huku akiwa hajawaandalia pa kuwapeleka na vijana wakarudi kwenye kukaba na kuiba huku akimwagiza Wambura awafyekelee mbali.

Kuliambia Taifa kuwa kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake, hapo aliidhinisha ufisadi kwenye kila kada bila kujali kama kauli ile ndo imepelekea madudu mengi kumulikwa na CAG.....

Anakuja hadharani anasema, ukimpinga atahakikisha hupati fursa yeyote. Mqana yake yeye amejiweka kwenye nafasi ya Mungu kwamba hakosei na wala hakosolewi.

Kila mtu ashinde mechi zake. Yupo Mtanzania ameandaliwa na Mungu kutukwamua kwenye huu mtanziko
.
 
Paragraph ya mwisho nimeielewa zaidi.
 
Hadi Abdul kutuwakilisha ug Kuna complexity ndugu mpiga mapambio?
Watu wanaspin issue za biashara binafsi za mtu , hii ni sawa na mtu uwe Rais halafu uambiwe hakuna ndugu yako anaruhusiwa kufanya biashara yeyote sio sawa
 
Kuna mazito yanakuja , the process is already rigged , namuonea huruma sana mama Samia , hajui uovu uliopandwa juu yake ,wanasubiri uote wamsulubu nao. Watanzania wangejua haya wangeshtuka usingizini wamsaidie Rais wao, magenge yanaenda kuivua nguo serikali the clock is ticking
Mungu atamwokoa kama sisi tumeshindwa, mwovu hutegwa na uovu wake mwenyewe...Hao waovu watasambaratika wenyewe pasikukua kilochowasambaratisha
 
Ninaamini hakuna njia bora ya kutatua mambo isipokua kwa weledi ,siamini kama kuna watu wanamhujumu Mheshimiwa Rais
 
Mungu amsaidie Mama yetu.
Sasa sijui hilo la bandari, TEC nao kuukataa huo mkataba wa DPW wana mkono katika kumwangusha Mama?
Kiukweli ukisikia ufisadi wa bandari unaogopa!
 
Back
Top Bottom