View attachment 2197392
===
Kunawakati nikimsikia mtu anamsema vibaya huyu Mama natamani kumpiga na kitu kizito kichwani,basi ni vile sheria tu,
Tangu tupate uhuru ni lini umewahi kuona Zahati 564 zinajengwa kwa mpigo nchi nzima?
Tangu tupate uhuru ni lini umewahi kuona vituo vya Afya 304 vinajengwa kwa Mpigo nchi nzima?
Tangu tupate uhuru ni lini tuliwahi kujenga hospitali 68 ikiwemo ya Mbagala kwa mpigo?
Hebu pitia kwa utulivu hii taarifa toka TAMISEMI, then umsikie mtu anamsema vibaya mama kama hujatamani kufanya ninayotamani Mimi,
=====
HUDUMA ZA AFYA YA MSINGI-TAMISEMI
27. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Ofisi ya Rais - TAMISEMI iliidhinishiwa Shilingi bilioni 28.20 kupitia ruzuku ya Serikali Kuu kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa
maboma 564 ya Zahanati katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Hadi kufikia Februari 2022, zimepokelewa Shilingi bilioni 23.32 sawa na asilimia 82.69 ya fedha zilizoidhinishwa. Ukamilishaji wa ujenzi upo katika hatua mbalimbali (Kiambatisho Na. 2).
28. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Shilingi bilioni 110.60 ziliidhinishwa kupitia ruzuku ya Serikali Kuu kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa
Vituo vya Afya 304.
Kati ya hivyo, Vituo 52 vilianza kujengwa Mwaka wa Fedha 2019/20 na Vituo 252 vimeanza kujengwa Mwaka wa Fedha 2021/22 ambapo Vituo 18 vimejengwa kwenye Halmashauri zenye Mapato madogo na Vituo 234 vimejengwa katika Tarafa zisizo kuwa na Vituo vya Afya na Kata za Kimkakati kupitia tozo za miamala ya simu.
Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 108.05 zimepokelewa sawa na asilimia 97.69 ya fedha zilizoidhinishwa na ujenzi unaendelea (Kiambatisho Na. 3).
29. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka wa Fedha 2021/22 Serikali ilitenga Shilingi bilioni 81.10 kwa ajili ya ku
endelea na ujenzi wa Hospitali 68 zilizoanza kujengwa mwaka 2018/19, Hospitali 31 zilizoanza kujengwa mwaka 2019/20 na kuanza ujenzi wa Hospitali mpya 28.
Hadi Februari, 2022 Shilingi bilioni 66.80 sawa na asilimia 82.36 zilikuwa zimepokelewa na ujenzi upo katika hatua mbalimbali (Kiambatisho Na. 3)
NB, Hizi Zahanati 564,Vituo vya Afya 304 na Hospitali 68 vyote hivi vinajengwa na TAMISEMI tu achili mbali vile vinavyojengwa na Wizara ya Afya sijaviorodhesha hapa,