Rais Samia anunua ambulance mpya 700 tofauti na ambulance 540 za tangu uhuru

Mbona hakuzitoa tangu mwanzo wa kipindi chake 2021-2025?
Lakini kwa hela za nani?
Hiyo ni Rushwa sasa!
 
Ametolea wapi hela huyu mama za kununua haya magari!? Kodi za Watanganyika zinakuwaje pesa za wazanzibari?!
 
NIMEKUPATA SANA MKUU
 
Wakati wa uhuru Wagonjwa walikuwa wachache.
 
wewe nini kinakuuma?
Ujinga wako ndo unaliangamiza taifa!
Kila mtu anakatwa fedha zake za jasho, machozi na damu kupitia Kodi, tozo na ushuru mbalimbali...

Na hizo zinaingizwa Kwenye Bajeti kuu ya serikali.
Je, Bajeti kuu ya serikali ni fedha binafsi za SAMIA?
Kwanini wakati wa matumizi au miradi ghafla fedha ziwe za Rais?
 
Mama anatisha kusema ukweli
 
Hapo sasa ndio watu wajue umuhimu wa vyama vingi na siasa za ushindani.

Hivi mnajua kama kungekuwa na siasa za ushindani chama kingekuwa makini zaidi kuwahudumia wananchi kwa sababu ya kuogopa kupigwa chini?

Kungekuwa na siasa za ushindani zingenunuliwa ambulance nyingi zaidi ya hizo!
 
Pesa yako au za walipa Kodi, wakati wa uhuru tulikua wananchi wa ngapi na Sasa tupo wangapi? Na hata hizo 700 hazitoshi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…