The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 747
- 2,112
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili Ukumbi wa Mlimani City kuongea na Wazee wa Dar es Salaam
Tunakuletea updates hapa
Mwenyekiti wa Wazee wa Dar, Salum Matimbwa
Tumepata kadi za msamaha wa Bima, lakini Wazee hatupati baadhi ya vipimo na Dawa tukifika Hospitalini
Tunaomba Rais Samia tunapokuwa Hospitalini, tupate vipimo na dawa zote kadri ya Magonjwa yanayotusibu
Tunakupongeza kwa kusimamia Sheria na Utawala bora. Tunaomba juhudi ziendelee ili kushughulikia kero za Wananchi
Vyombo vya Ulinzi na Usalama vifanye kazi kwa Sheria, Kanuni na Utaratibu waliojiwekea. Inapobidi Wananchi washirikishwe ili kuondoa manung'uniko
Wazee tunaomba Vyombo vyote vya Usafiri wa Umma vitenge viti maalum vya kukaa wazee
Pia, vihimizwe kuhakikisha vinawabeba wajukuu zetu ambao ni Wanafunzi wanapokwenda na kurudi shuleni
Kuna uwakilishi wa makundi mbalimbali #Bungeni lakini Wazee hatuna uwakilishi
Hivyo tunaomba na sisi ikikupendeza Rais, tupewe nafasi hiyo ili tupate Watu wa kutusemea matatizo yetu kwenye Vyombo vya Mamlaka
Waziri wa Afya - Dkt. Dorothy Gwajima
Wazee wanazidi kuongezeka. Mwaka 2012 kulikuwa na Wazee milioni 2.5 sawa na asilimia 5.6 na hivi sasa wameshafika milioni 2.52.
Mauaji ya wazee yamepungua kutoka 577 mwaka 2014 hadi wazee 34 mwezi Desemba mwaka 2020.
Rais Samia Suluhu Hassan
Tahadhari dhidi ya Corona\uvaaji barakoa ukumbini
Naomba niwaombe radhi kwamba mtindo wa maisha umebadilika. Tumekuja na vikaba midomo ninyi pamoja na sisi
Kwasababu mkusanyiko huu ni mkubwa na Wazee ni rahisi kupata haya maambukizi, hatuwezi kujua nani anayo na nani hana. Sisi wenzenu tunazunguka sana
Wazee wameona mengi na wana uzoefu mkubwa. Ndiyo maana tumeona tuje kuzungumza nanyi ili tuone mnasema nini na mnatuambia nini
Ni utamaduni, toka tumepata Uhuru Viongozi wetu wamekuwa wakikaa na kuongea na Wazee. Mimi sina jambo ila nimekuja kuwasikiliza
Tiba kwa Wazee
Mbali na Sera, Ilani ya CCM inatutaka kufanyia kazi suala la tiba ya Wazee. Waziri wa Afya ametoa ahadi nzuri lakini nataka aisimamie leo na sio kesho.
Dunia ipo kwenye Corona na wahanga wakubwa ni Wazee. Kamati niliyoiunda wanakwenda vizuri na karibu wataleta majibu
Nakubaliana nanyi kuhusu kuwawezesha kiuchumi lakini tuna Mfuko wa TASAF na tutakwenda kwenye Wilaya zote na kuhakikisha kila Mzee mwenye sifa anapata nafasi
Jambo la kutoa pensheni kwa kila Mzee tulipiga hesabu tukaona ni gumu kutokana na hali ya Uchumi
Corona imeshusha Uchumi karibu wa Dunia nzima. Pamoja na kwamba tutajitutumua tukue lakini tuna miradi mikubwa ambayo inahitaji kukamilika
Naomba mnipe muda niangalie hali ya Uchumi inavyokua halafu nitalitolea maamuzi. Tujenge Nchi kwanza halafu tutagawana faida
Wito wa kuwatunza Wazee
Nitoe wito kwa Jamii ya Kitanzania tutunze Wazee, awe amekuzaa au hajakuzaa. Tuna kisingizio cha maisha magumu ila naona ni maadili
Shughuli ya kuchukua Wazee kuwaweka kwenye nyumba maalum inafanywa na wenzetu wa Magharibi, Serikali itawajengea nyumba ila tuwatunze
Onyo dhidi ya uhalifu
Leo nimesoma mtandaoni kwamba Dar kuna Watu wanajaribu kupima kina cha Maji, Viujambazi vimeanza kuja juu - Naomba nitoe meseji wasijaribu kina cha Maji. IGP upo hapa, Mitandaoni wanamtaja Afande mmoja alikomesha ujambazi wanasema Mama turudishie, kaliangalie hilo