PreGE2025 Rais Samia apandisha dau 'Goli la Mama' kwa Simba SC, kila Goli TSh. milioni 10 kwa mchezo wa CAF

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelipa thamani goli la Mama analolitoa kwa timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya CAF ambapo kwa sasa Nchi yetu inawakilishwa na Simba Sc pekee kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Akithibitisha ongezeko la thamani hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema, "Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, anatambua umuhimu mchezo wa marejeano dhidi ya Al Masry hivyo kwa kuongeza motisha kwa wachezaji atanunua kila goli moja kwa shilingi milioni 10"

Simba Sc inahitaji ushindi wa magoli 3-0 siku ya jumatano ili kujikatia tiketi ya kusonga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo hawajafuzu kwa muda mrefu.

1744110219917.png
 
Imagine, mtu anakuja kwako ana shida ya milioni1 unamkopesha, kisha katika pitapita zako unaenda uwanja wa mashindano ya ndondo unakuta uliemkopesha anajinadi "kila goli litakalofungwa na timu A nalipia laki1", utawaza nini?

Magoli ya mama huwa yanawachekesha sana wakopeshaji wa hii nchi, matatizo ya huduma za kijamii yapo chungu nzima pesa zinanunua magoli!
🙁
 
wAnaotoa misaada kwenye hz nchi inabid wajitafakar,haiwezekan hadi wateule wa rais wa kwenye mawilaya huko wana magari ya mil 400
 
Izo nipesa zinazo tokana na makato katika mechi ambazo timu zinapocheza.
Ni fedha inayo rudi kwa namna ya kuhamasisha.
Anajua ata aweke milioni hamsini kwa goli bado watashindwa kupata ata goli moja
 
Acha wivu kiredio.
 
10 x 10,000,000 = 100,000,000

Waarabu wakishakula goli 4 kabla ya dakika ya 60, wataloa mvua ya magoli.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelipa thamani goli la Mama analolitoa kwa timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya CAF ambapo kwa sasa Nchi yetu inawakilishwa na Simba Sc pekee kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Akithibitisha ongezeko la thamani hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema, "Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, anatambua umuhimu mchezo wa marejeano dhidi ya Al Masry hivyo kwa kuongeza motisha kwa wachezaji atanunua kila goli moja kwa shilingi milioni 10"

Simba Sc inahitaji ushindi wa magoli 3-0 siku ya jumatano ili kujikatia tiketi ya kusonga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo hawajafuzu kwa muda mrefu.

Mwambieni namdai malimbikizo ya mshahara
 
Back
Top Bottom