PreGE2025 Rais Samia apandisha dau 'Goli la Mama' kwa Simba SC, kila Goli TSh. milioni 10 kwa mchezo wa CAF

PreGE2025 Rais Samia apandisha dau 'Goli la Mama' kwa Simba SC, kila Goli TSh. milioni 10 kwa mchezo wa CAF

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Ni matumizi tu mabaya ya kodi za wananchi, huku mtawala akiitegemea katiba mbovu na ambayo inampa haki na madaraka makubwa ya kufanya chochote kile! Na bado asishtakiwe.
 
Kuna hatua za mashindano zinahotaji uzalendo Zaidi.
Machi hii wachezeshwe magolikipa watanzania
 
Izo nipesa zinazo tokana na makato katika mechi ambazo timu zinapocheza.
Ni fedha inayo rudi kwa namna ya kuhamasisha.
Anajua ata aweke milioni hamsini kwa goli bado watashindwa kupata ata goli moja
Simba co utopwinyo ww
 
Uyu anataka kutuwekea nuksi Kesho tusipate matokeo mazuri
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelipa thamani goli la Mama analolitoa kwa timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya CAF ambapo kwa sasa Nchi yetu inawakilishwa na Simba Sc pekee kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Akithibitisha ongezeko la thamani hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema, "Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, anatambua umuhimu mchezo wa marejeano dhidi ya Al Masry hivyo kwa kuongeza motisha kwa wachezaji atanunua kila goli moja kwa shilingi milioni 10"

Simba Sc inahitaji ushindi wa magoli 3-0 siku ya jumatano ili kujikatia tiketi ya kusonga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo hawajafuzu kwa muda mrefu.

Aiseee tuna safari ndefu. Majuzi wanaosha magari kuchangisha pesa za kujenga shule ya maeneo fulani. Daahhhhh
 
Imagine, mtu anakuja kwako ana shida ya milioni1 unamkopesha, kisha katika pitapita zako unaenda uwanja wa mashindano ya ndondo unakuta uliemkopesha anajinadi "kila goli litakalofungwa na timu A nalipia laki1", utawaza nini?

Magoli ya mama huwa yanawachekesha sana wakopeshaji wa hii nchi, matatizo ya huduma za kijamii yapo chungu nzima pesa zinanunua magoli!
🙁
Mama anacheza ana akili za Mazezeta wa Hili Taifa,
 
Hizi timu zina watu wanapata hela kwa kuingiza hela.
Hii hela ya Goli IONDOLEWE au kila goli la timu yoyote likifungwa iwe kwa ajili ya madawati ya shule huko vijijini au dawa kwa wasiojiweza kulipia matibabu
 
Deni la taifa limeogezeka mpka trilion 97. Matumizi yasio na tija, ripoti ya CAG. (2025) Billion 371.42.
Tunaenda kwenye bunge la bajeti utasikia wahisani ni trilion kadhaa halafu matumizi ni kutapanya tu.

Vijana wapo mtaani hawana ajira hili Raisi halioni ila anaona goli ni mhimu kuliko maisha ya Watanganyika.
Tunahitaji safari ndefu kufika tunapotaka
 
Huyu mama akagombee uongozi Zanzibar tu changamoto za Bara hazijui
 
IMG-20250407-WA0017.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amelipa thamani goli la Mama analolitoa kwa timu za Tanzania zinazoshiriki michuano ya CAF ambapo kwa sasa Nchi yetu inawakilishwa na Simba Sc pekee kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Akithibitisha ongezeko la thamani hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema, "Mh. Rais Samia Suluhu Hassan, anatambua umuhimu mchezo wa marejeano dhidi ya Al Masry hivyo kwa kuongeza motisha kwa wachezaji atanunua kila goli moja kwa shilingi milioni 10"

Simba Sc inahitaji ushindi wa magoli 3-0 siku ya jumatano ili kujikatia tiketi ya kusonga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo hawajafuzu kwa muda mrefu.

Milioni hamasini ileee
 
Hiki ndio anacho weza kutenda kwa ufasaha. Hata akiambiwa afanye mwaka mzima yy sw. Ila Mambo muhimu yy HAPANA jw wamekaa mateka uko kwa m23 yy kimya tu mara barabara mbovu Daraja la somanga limekatika kwa masaa 72. Yy poa tu
KAZI ni kipimo cha utu
 
Back
Top Bottom